Afisi Kuu ya Habari: Angazo Maalum “Baada ya Miaka Ishirini ya Vita vya Msalaba, Afghanistan Yaelekea Wapi?!”

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Mnamo 07/10/2001 M, Amerika, kinara wa ukafiri, na mshirika wake Uingereza walianzisha vita vya kinyama dhidi ya Waislamu, waliishambulia kwa mabomu miji ya Afghanistan ya: Kabul, Kandahar, Jalalabad na mengineyo na makombora ya Tomahawk, na kurusha makombora na aina anuwai za silaha. zilitegemea anga, maji na ardhi za Waislamu ambazo ziliruhusiwa kwao na watawala wasaliti, haswa katika Pakistan na Uzbekistan. Hili liliendelea kwa wiki kadhaa mfululizo. Licha ya ujasiri mkubwa na ukakamavu wa hali ya juu ulioonyeshwa na Waislamu katika upinzani kwa wavamizi, kwa silaha hafifu walizokuwa nazo ikilinganishwa na nguvu za wavamizi, walakini ukali wa shambulizi la kikatili kutoka kwa wavamizi na usaliti wa watawala pambizoni mwa Afghanistan ulisababisha kuanguka kwa Afghanistan na kwenda mikononi mwa Amerika mnamo 2001 M.

Idadi ya vifo vya Waafghani katika robo karne iliyopita ilifikia zaidi ya milioni mbili, ikimaanisha kwamba idadi hii kubwa ya wahasiriwa ilishuka tu tangu uvamizi wa Urusi nchini Afghanistan mnamo 1979 M hadi baada ya uvamizi wa Amerika mnamo 2001 M. Kujitolea huku kukubwa kwa Afghanistan kulimalizika, na la kusikitisha sana, ni kuapishwa kwa Hamid Karzai kama mtawala kibaraka wa Amerika nchini Afghanistan.

Hati ya Bonn, ambayo ilianzisha katiba mpya ya Afghanistan mnamo 12/6/2001 M, ilisainiwa na Amerika kutoka Azimio la Baraza la Usalama Nambari 1883 kuiunga mkono, na katiba iliyomo kwenye waraka huo iliipa Amerika dori muhimu katika mavazi ya Umoja wa Mataifa katika kuamua mambo ya ndani na ya nje ya watu wa Afghanistan, na katika kusimamia kila jambo dogo na kubwa nchini Afghanistan, hati hiyo iliainisha uwepo wa Amerika katika kuanzishwa kwa chombo cha kikatiba, katika kuanzishwa kwa shirika la utumishi wa umma, katika kazi na mamlaka ya serikali, na katika mabadiliko yoyote yanayohusiana na sheria za kiutaratibu za taasisi zote za serikali, na katika ufuatiliaji wa tekelezaji wa nyanja zote za makubaliano, ikimaanisha kwamba Amerika imejiweka yenyewe kama mtawala halisi wa dola hii hadi atakapo Mwenyezi Mungu. Na hili ndilo linalodhihirisha siri za Amerika kwamba nia ni kulitawala eneo la Kiislamu, na wala sio kuwepo utawala (huru) kama inavyodai, bali kwamba vita vyake, ambavyo ilivitangaza kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, sio chochote isipokuwa mlango wa vita vya msalaba dhidi ya Uislamu na Waislamu, kukaza udhibiti juu ya nchi yao, na kuutenga Uislamu na maisha yao kama walivyofanya na wanafanya nchini Afghanistan na Iraq, na kama ilivyoandikwa katika mradi wao (Mashariki ya Kati Kuu). Ni vita vya msalaba ambavyo vilivyofichuliwa na amali za jeshi, kisiasa na kielimu zilizofanywa na Amerika ambapo zililipuka katika nchi za Kiislamu. Hakika, Bush Mwana alizifichua tangu siku za mwanzo za matukio ya 9/11, katika hotuba yake tarehe 16/09/2001, ambapo alitangaza kwamba vita vyake dhidi ya ugaidi ni vita vya msalaba, na haikuwa imepita ila siku nne tu tangu mlipuko huo mkubwa, ambazo hazitoshi kukamilisha uchunguzi wa tukio ambapo haiwezi hata kufikia ushuri yake, ambapo inaonyesha kile kilichofichwa katika hazina ya wanasiasa wa Amerika dhidi ya Uislamu na Waislamu. Na ingawa aliviita (vita vya msalaba) kwa kuwakusanya maadui wa Uislamu pambizoni mwake, aliwaleta Waislamu pamoja kumpinga. Na huu ndio upinzani nchini Afghanistan, ulioilazimisha Amerika kurudi nyuma na kutafuta njia mbadala nchini Afghanistan. Katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita, vikosi vya Amerika, pamoja na vikosi vya kimataifa (ISAF) na uongozi wa NATO, havikuweza kupanua ushawishi wa uvamizi (kikamilifu) isipokuwa tu katika mji mkuu, huku maeneo yote ya Afghanistan nje ya Kabul yakisalia mandhari ya silaha operesheni za kisilaha ambazo hazikukoma hata siku moja baada ya uvamizi wa Amerika wa Afghanistan.

Hasara ambazo Amerika ilipata wakati wa uvamizi wake wa Afghanistan zinathibitisha kwamba Amerika ilikuwa ikiondoka Afghanistan ikiburuta mkia wa kushindwa bila ya kutoka na mazungumzo ambayo yangeihifadhi kutokana na ushawishi ambao haingeweza kuufikia ndani ya vita!

Na sisi katika Hizb ut Tahrir tunatambua kwamba katika Taliban kuna ndugu ambao ni wakweli wenye ikhlasi basi ni kwa watu hawa ndio tunawaelekea kwa kuwaambia:

1- Sahihisheni jambo hilo na muache kujadiliana na Amerika, ili msiiwezeshe Amerika kufikia lile ambalo haingeweza kulifikia katika vita…

2- Na kinaikeni kuwa kadhia kuu ya Waislamu ni kuregeshwa kwa Khilafah baada ya kutoweka kwa muda mrefu, kwani ni faradhi ya Mwenyezi Mungu (swt) na utiifu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)…

3- Na jueni kuwa kushiriki katika utawala wa mchanganyiko wa Uislamu na usekula haukubaliki na Mwenyezi Mungu, kwani Al-Qaqiy Al-Aziz hakubali chochote isipokuwa kizuri …

Hii ndio haki ﴾فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ﴿ “Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?” [Yunus: 32]. Na kufuata haki ndio kutakakoikoa Taliban, nchi hii, na watu wake, na Waislamu wote … Hivi ndivyo Hizb ut Tahrir anakushaurini, kama tulivyokushaurini mwanzoni mwa utawala wenu kwa kutangaza Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Mkakataa kisha mkajua kuwa mumekosea kwa kukataa huko kama ilivyo pokewa kutoka kwa Mulla Omar Mwenyezi Mungu amrehemu katika mojawapo ya vikao vyake lakini baada ya kupita zama  … Sisi hapa tena tunaikariri naswaha je, yupo wa kuitikia?

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Ijumaa, 20 Dhu al-Hijjah 1442 H sawia na 30 Julai 2021 M

– Kufuatilia Angazo kwa Lugha Nyenginezo –

Kalima ya Video ya Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Muhammad)

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kuhusu Athari za Vita vya Msalaba nchini Afghanistan 

Jibu la Swali Lililotolewa na Hizb ut Tahrir:
“Athari za Kisiasa nchini Afghanistan”

Siku ya Arafah – Jumatatu 09 Dhu al-Hijjah 1442 H sawia na 19 Julai 2021 M

Ili Kusoma Bonyeza Hapa

– Alama Ishara za Angazo –

#أفغانستان      
#Afghanistan
#Afganistan      

Matoleo, Majibu na Vijitabu
“Athari za Kisiasa nchini Afghanistan”

Siku ya Arafah – Jumatatu 09 Dhu al-Hijjah 1442 H sawia na 19 Julai 2021 M

Wilayah Afghanistan

Kushiriki katika Mazungumzo ya Amani Kunapelekea Kushirikiana na Adui Mbaya Zaidi wa Uislamu na Waislamu

01 Jamada al-Thani 1440 H – 06 Februari 2019 M

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vita vya Uharibifu na Amani ya Fazaiko Ndio Urithi Mkuu wa Amerika nchini Afghanistan!

18 Dhu al-Hijjah 1442 H – 18 Julai 2021 M

Jamhuri ya Afghanistan Imegeuka kuwa Kichinjio; Je kuna Njia Yoyote ya Kutoroka?

28 Jumada I 1442 H – 12 Januari 2021

Wafuasi wa Machiavelli Hawawezi Kuondoa Ufisadi

11 Muharram 1442 H – 30 Agosti 2020 M

Lini Mujahideen wa Zamani watajifunza kutokamana na wao kudungwa mara kwa mara na Amerika?!

18 Rajab 1441 H – 13 Machi 2020 M

Jamhuri, Demokrasia na Chaguzi za Kidemokrasia Zimeshindwa Nchini Afghanistan; Muendelezo wowote wa Juhudi hii itakuwa ni marudio ya jaribio hili lililoshindikana

16 Rajab 1441 H – 11 Machi 2020 M

Makala na Habari na Maoni
Vita vya Afghanistan: Kutoka Kwenye Uongo wa Ubabaishi Hadi Kwenye Ukweli wa Wazi!

29 Ramadhan 1442 H – 10 Mei 2021 M

Ukiukaji wa Makubaliano; Tabia ya Kale ya Amerika!

27 Jumada II 1442 H – 09 Februari 2021 M

Mpango wa Khalilzad sio Kuleta Amani bali ni Kuisalimisha Taliban!

14 Jumada II 1441 H – 08 Februari 2020 M

Mbinu ya Amerika na Kupunguza Kisiasa Wanajeshi ndani ya Afghanistan

11 Jumada II 1441 H – 05 Februari 2020 M

Ahadi Tupu kwa Wanawake wa Afghan

27 Rabi ul-Awwal 1441 H – 24 Novemba 2019 M

Amali za Hizb ut Tahrir Kote Ulimwenguni

Video

 

Angazo la Vyombo vya Habari
“Athari za Kisiasa nchini Afghanistan”

Siku ya Arafah – Jumatatu 09 Dhu al-Hijjah 1442 H sawia na 19 Julai 2021 M