Alama za Mapenzi ya MwenyeziMungu Kwa Mja Wake

Mara nyingi,mahaba huarifishwa kuwa hisia zenye mvuto mkubwa na muambatanisho wa kimwehemko. Watu wengi hufunga maana ya mapenzi katika muktadha wa vitu na anasa na starehe za duniani. Kwa kuwa ni mapenzi ni mchakato wa maumbile ya mwanadamu, hivyo siajabu kuyaona mapenzi na upendo yamekita katika jamii ya kibinadamu. Mapenzi ya mume kwa mkewe, Baba kwa wanawe na mapenzi ya mtu ya sehemu anayoishi yote hii ni mifano tu michache inayothibitisha uwepo wa tunu hii kubwa ulimwenguni. MwenyeziMungu SWT alimuumbia mwanadamu sifa ya kupenda sana mali kama alivyobainisha katika suratul Aadiyat:

وَإِنَّهُ لِحُبِّ ٱلْخَيْرِ لَشَدِيدٌ

Kwa hakika kupenda kwake mali kukubwa mno.

Tafsiri hii ya mapenzi ni katika mafungamano baina ya waja. Ama kuhusu sifa ya MwenyeziMungu kupenda waja wake hii humaanisha kumtunukia mja neema ya msamaha. Na ni ukubwa gani huu ulioje wa neema hii ya kupendwa na Mwenyezi Mungu Muumba Mbingu na Ardhi na vilivyomo? Quran imethibitisha kuwa MwenyeziMungu huwapenda waja wake wema kama alivyosema katika suratul Maidah aya 54:

فَسَوْفَ يَأْتِي ٱللَّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ

Basi MwenyeziMungu atawaleta watu ambao atawapenda nao watampenda.

Kabla ya kuweka hapa alama zinazoashiria kuwa mja anapendwa na MwenyeziMungu, ni muhimu sana kuzindusha kuwa mapenzi ya MwenyeziMungu kwa waja wake yamefungamanika na kujifunga na taklifu za kisheria yaani wakati wowote mja anapojifunga na maamrisho ya MwenyeziMung na kujiepusha na makatazo yake. Hii ndio kujiwekea dhamana nzuri ya kuyapapata mapenzi ya Allah. Hii ndio sababu ya Mtume (SAAW) katika kuomba kwake mahaba ya Mola wake, alikuwa akiomba amali itakayomfikisha kwenye mahaba hayo. Amepokea Tirmidhy kutoka Abi Dardai kwamba Mtume Rehma na Amani za MwenyeziMungu zimshukie Yeye alisema

كَانَ مِنْ دُعاءِ دَاوُدَ: اللَّهُمَّ إنِّي أَسْألُكَ حُبَّكَ، وَحُبَّ مَنْ يُحِبُّكَ، وَالعَمَلَ الَّذِي يُبَلِّغُنِي حُبَّكَ..، ».

Katika dua za Daud AS : Ewe Mola nakuomba mahaba yako na Mahama ya yule unayempenda na amali itakayonikisha kwenye mahaba yako..

Kwanza:Kupendwa na watu hapa duniani.

Ukijiona kuwa waja wema wanakutaja kwa uzuri na hufurahi kila unapokutana nao basi ni ishara kuwa MwenyeziMung anakupenda.  Abu Hureira anasimulia Hadithi kutoka kwa Mtume

إنَّ اللهَ تعالى إذا أحب عبدًا دعا جبريل، فقال: إني أحب فلانا فَأَحْبِبْهُ، فيحبه جبريل، ثم ينادي في السماء، فيقول: إن الله

يحب فلاناً فأحبوه، فيحبه أهل السماء، ثم يوضع له القَبُولُ في الأرضِ،

MwenyeziMungu pindi anapompenda mja, humuitwa Jibril na kumwambia: Hakika yangu mimi ninampenda fulani nawe mpende na hapo jibril humpenda mtu huyu. Kisha Jibril hutangaza kwa Malaika wenzake mbinguni akisema: MwenyeziMungu anampenda fulani basi nanyi mpendeni. Hapo viumbe hao watukufu humpenda kisha huwekewa Qabul  kwa hapa duniani.(Watu wakawa wanampenda.)

Pili: Kuipa nyongo/Mgongo Dunia

Hii ni moja wapo ya alama za kujulisha mtu kuwa ametunikiwa mapenzi ya Allah. Mmoja katika wanavyuoni mkubwa  Sufyan Thauri alisema kwamba Zuhd hapa duniani ni kumaanisha kuwa uko tayari moyoni mwako kwa kufikiria Akhera kuwa kivyovyote vile utakufa.’ Hivyo Kuipa nyongo dunia ni hali ya moyo wa mtu zaidi kuwa kwamba hotoishi milele hapa duniani bali ataihama. Tukiwa na ufahamu huu tutakua na hisia ya kwamba tutaondoka hapa dunia hii itatupelekea kutofitinika na starehe za dunia na tutajikurubisha zaidi kwa MwenyeziMungu kwa kujifunga na maamrisho yake na kuepuka makatazo yake. Hii humaanisha kutofitinika kabisa na mali, watoto na wanawake. Leo ulimwengu yanarembeshwa na mfumo wa kirasilimali ambao kila uchao utaona unavumbua fitina mpya za kumfanya mtu aone kuwa dunia ndio kila kitu.  Runinga  majumbani mwetu zimesheheni ya ulevi ’kata kiu na Tusker’ yanayohadaa watu wengi kuamini kuwa maisha ya duniani ndio kila kitu hivyo watu ni kufukuza tamaa za mali!  kujenga ufahamu kwamba ufanisi hapa duniani upo katika kufikia upeo mkubwa wa kukimu mahitaji yako ya kimwili hivyo fanya utakalo pasina na kujali halali au Haramu!   Hali hii ndio hufanya watu wamecharukwa katika kutafuta ‘maisha bora’ huku wakiona kuwa hawana wakati kabisa kuutumikia Uislamu. Alikuja mtu mmoja kwa Mtume Rehema na Amani za MwenyeziMungu zimshukie akimuuliza

Nijulishe ewe Mjumbe wa MwenyeziMungu amali nitakayoifanya itanipelekea kupendwa na MwenyeziMungu  na kupendwa na watu. Mtume SAAW akwambia ni Ipe nyongo dunia Allah atakupenda  na achana kutamani vitu vya watu watakupenda watu.

Tatu: Upole na waja wenzako

Hakuna tabia inayovutia watu wengi kama kuwa na upole katika kila jambo tena mahala panapostahiki. Upole hapa ni kuwa na busara iliojaa hekima katika kila jambo. Kwa mfano kumwambia Muislamu anayafahamu kwamba njia ya kusimamishwa kwa dola ya Kiislamu ni kupitia kujenga imani …Mwambie ndugu yangu kuna tofauti baina ya kulingania mtu imani na kulingania kurudisha maisha ya Kiislamu. Hii tofauti lau utambwambia wewe ni zuzu ! Kinyume chake ni busara kumwambia ewe ndugu yangu umejua jambo moja lakini umepitwa na mambo mengi kisha uanze kumwelezea njia halisi ya kisheria ya kusimamisha Darul Islam. Hivyo hivyo tunapotangamana na wake zetu majumbani tunatakikana kujipamba na sifa ya upole. Si hekima kabisa kumtukana  mkeo kwa sababu tu amevunja kikombe!

Nne: Subra

MwenyeziMungu SWT amakariri katika Quran sifa ya subra kwamba yeye siku zote yuko pamoja na wenye kusubiri. Sifa hii ni muhimu sana katika maisha ya Mwislamu. Ni katika suna ya MwenyeziMungu kuwatahini waja wake kwa maradhi, njaa, ukame vifo na kadhalika. Isitoshe subra inahitajika zaidi leo hususan tukizingatia kuwa kazi kubwa ilioko mbele yetu ni kuregesha tena Khilafah, bila shaka njia yake ni yenye kusuhubiwa na mazito. Uvumi dhidi ya Ujumbe unaobebwa, mateso ya walinganiaji na mengineo ni katika masaibu yanayokumba njiya ya mabadiliko.  Asema Allah katika aya 146 ya suratul Imran:

وَكَأَيِّن مِّن نَّبِيٍّ قَاتَلَ مَعَهُ رِبِّيُّونَ كَثِيرٌ فَمَا وَهَنُواْ لِمَا أَصَابَهُمْ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَمَا ضَعُفُواْ وَمَا اسْتَكَانُواْ وَاللّهُ يُحِبُّ الصَّابِرِين

Na manabii wangapi walipigana na maadui na pamoja nao kulikuwa na watakatifu wengi na hawakulegea kwa yale yaliyowasibu katika njia ya Mwenyezi Mungu, hawakudhoofika wala kudhalilika. Na MwenyeziMungu anawapenda wenye kusubiri.

Mwenyezimungu kutangaza kuwa anapenda wenye kusubiri ni amri kwa Waislamu kujipamba na subra kama vilevile subra ni alama ya kunali mahaba ya Allah.

Tano: Kumfuata Mtume katika yote aliyotuamrisha na Kutukataza:

MwenyeziMungu anasema:

قُلْ إِنْ كُنْتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ

Kitendo hiki moja kwa moja hutupelekea kupata mahaba ya MwenyeziMungu SWT. Katika safu ya Waislamu kuna ulinganizi unaokaririwa sana wa kufuata sunna za Mtume SAAW. Na hili ni jambo zuri ispokuwa kufuatwa Mtume SAWW kumedogoshwa mno leo kiasi cha kuwaona Waislamu wanamfuata katika kuta nne na misikiti huku maisha jumla wakimuasi Mtume SAAW wakifuatwa siasa za  Biden na Boriss Johnson. Waislamu hawafuati uchumi wa Mtume Muhammad SAAW badali yake ni wafuasi wa mfumo wa Kirasilimali uliotungwa Adam Smith. Hawafuati tabia za Mtume SAAW bali wanafuata mienendo ya kileberali za kina John Lokce! Kama kweli unaona kuwa unamfuata Mtume SAAW katika kila jambo lako basi ni alama nzuri kuwa Allah anakupenda.

Hizi ni alama tano lau Muislamu ataonekana kuwa nazo basi ni dalili nzuri ya kuwa amenali mahaba ya ALLAH. Kwa hakika Mahaba ya Allah ni kitu cha thamani kwa mja kukikimbilia. Bahati nzuri ilioje Mtume SAAW akabainisha njia ya kuyafikia mahaba haya kama ilivyokuja katika hadith Qudusi

 

وما تقرب إليّ عبدي بشيء أحب إليّ مما افترضته عليه ، ولا يزال عبدي يتقرب إليّ بالنوافل

حتى أحبه ، فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به ، وبصره الذي يبصر فيه ، ويده التي يبطش بها

ورجله التي يمشي بها ، ولئن سألني لأعـطينه ، ولئن استعاذني لأعيذنه }

Na hajikurubishi kwangu mja wangu kwa jambo ninalolipenda zaidi ila kwa mambo ya faradhi niliyomfaradhishia. Na wala hatoacha mja kujikurubisha kwangu na suna bali akiendelea na ibada za sunna hufikia mimi Kumpenda. Na nitakapompenda, basi ninakua masikio yake anayosikia kwayo. Na Macho yake ambayo kwayo huonea na mkono wake ambao kwake hushikia na mguu wake anaoutembelea na endapo akiniomba humpa na akiniomba ulinzi mimi humlinda.

Na twamuomba MwenyeziMungu atupe mapenzi yake.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

 Hizb ut Tahrir Kenya