Damu ya Wanawake na Watoto wa Afghanistan ni Duni kwa Marekani na Utawala Kibaraka wa Afghan

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Usiku wa Jumapili, 22 Septemba, mashambulizi ya angani na ardhini yalitekelezwa na majeshi ya Afghan na Marekani yakilenga kile kilichoelezewa kuwa ni maficho ya Taliban katika wilaya ya Musa Qala katika mkoa wa Helmand, yakaua raia 40 na kuwajeruhi taribani watu 18 wengine ambao walikuwa wanahudhuria sherehe ya harusi katika jengo mkabala. Kwa mujibu wa Abdul Majid Akhundzada, mwanachama wa baraza la mkoa wa Helmand, wengi wa waliouliwa walikuwa wanawake na watoto. Uvamizi huu wa mauaji unakuja siku chache baada ya shambulizi la droni ya Marekani mnamo 19 Septemba na kuwaua na kuwajeruhi takribani wakulima 70 wasiokuwa na hatia katika mkoa wa Nangarhar mashariki ya Afghanistan.

Miezi ya karibuni, kumekuwepo na kuzidi kwa idadi ya raia wahanga katika mikono ya vikosi vya usalama vya Afghan na majeshi ya uvamizi ya Marekani kutokana na kuzidisha juhudi zao za kijeshi dhidi ya Taliban. Ripoti ya UN iliyotolewa mnamo 30 Juni mwaka huu, ilisema kwamba vifo vya raia 717 vilisababishwa na majeshi ya Marekani na Afghan katika kipindi cha miezi sita ya mwaka huu –idadi kubwa kuliko vifo vya raia kutokana na makundi ya kisilaha.

Marekani kutojali utukufu wa damu za watu sio jambo la kushangaza, kwa kuwa Marekani ni muhalifu wa kimsalaba asiyezingatia hasara ya kupoteza uhai, hata iwe kwa kiwango cha juu hata kwa gharama ya juu bora tu iwe ni katika kuhifadhi maslahi yake ya kikoloni kisiasa na kiuchumi, kama tulivyoona ndani ya Afghanistan, Iraq, Somalia na kwingineko. Lakini, kinacho tamausha zaidi ni kwamba utawala wa Afghan unashirikiana mkono kwa mkono na Marekani wakoloni katika kuwaua mama, dada, binti na watoto wake katika njia ya kutekeleza ajenda ya Washington ndani ya eneo hilo. Lengo msingi la uongozi wote wa Afghan ni kufuata mchoro wa uvamizi wa Marekani ndani ya Afghan kuanzia 2001, na hauna ikhlass katika kuwatumikia watu wake bali upo kuhifadhi maslahi ya viti vyao vya uongozi na utajiri and kutumikia maslahi ya mabwana zao Marekani. Rais Ashraf Ghani majibu yake kuhusu umwagikaji damu yamekuwa yakutamausha. Badala ya kutambua majanga yanayokumba raia wasiokuwa na hatia lakini amejitia upofu ili kuitumikia sera ya Marekani na kudai kwamba kuwepo na ‘tahadhari ya ziada’ katika oparesheni za kijeshi. Kwa miaka 18 iliyopita, majeshi ya Marekani yamefanya umwagaji damu katika ardhi hii, yamefanya uharibifu na kukatisha watu tamaa, kutia hofu na kutekeleza uhalifu hata usiosemeka dhidi ya watu wake, ikijumuisha kuwakosea heshima dada zetu katika hali mbaya mno pasina na kujali kuhesabiwa na kusaidiwa na watawala mtawalia wa Afghanistan na tawala zao.

Mpaka lini wanawake, watoto na raia wengine wasiokuwa na hatia wa Afghanistan wataendelea kupitia unyama huu wa uvamizi wa kikoloni ndani ya nchi? Damu na machozi yao yameijaza ardhi hiyo! Umekuwa duni uhai wa dada zetu na watoto wao ambapo vifo vyao vinatizamwa kama takwimu zisizokuwa na maana na majanga yanayostahili katika njia ya kuhifadhi ajenda za kikoloni. Kwa kuongezea, hakika lazima iwe kwamba uchaguzi huu wa urais wa 28 Septemba hautafaulisha chochote kwa watu wa Afghanistan. Watafaulu vipi ilhali wao ni kuweka alama ya kuendeleza utawala ambao upo chini ya mamlaka ya Amerika? Hakika, tumeshuhudia mara kwa mara kwamba uchaguzi ni kuupigia muhuri uongozi wa mtawala kibaraka wa Marekani huku tabu na ukataji tamaa unaendelea kuzidi. Chaguzi hizo zimekuwa kama makaburi ya matumaini ya urongo na ahadi zilizovunjwa, zilizojaa urongo na ukhaini na zisizopanda kitu isipokuwa mgawanyiko na vurugu baina ya watu ilhali hali ya faudhwa, ukosefu wa usalama, vifo na uharibifu, umasikini mkubwa, ukosefu wa ajira, uhalifu, ufisadi, usambaratikaji wa nidhamu ya afya na mtaala wa elimu unaendelea pasina na kusita.

Mito ya damu za Ummah wetu ndani ya Afghanistan itaendelea kutiririka pasina mwisho mpaka pale Marekani wakoloni na tawala zinazo wahudumikia wamagharibi na nidhamu zao zitakapo ondoshwa katika ardhi –mizizi na matawi yao. Hili litafaulu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, kwa kuwa ndio uongozi wa kweli wa Kiislamu na hautokubali kuwa chini ya mamlaka au ushawishi wa dola yoyote ya kigeni. Bali, itakwenda mbio ili iwe inaongoza kisiasa, kiuchumi na nguvu za kijeshi duniani na kuwalinda raia wake kutokana na madhara, na kuwahudumikia kwa ikhlass, na kuweka amani, usalama na ustawi katika ardhi zake na kueneza nuru ya Uislamu duniani kote.

[تَرَى كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُواْ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ اللّهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ]

“Utawaona wengi wao wanafanya urafiki na walio kufuru. Hakika ni maovu yaliyo tangulizwa na nafsi zao hata Mwenyezi Mungu amewakasirikia, nao watadumu katika adhabu.” [Al-Ma’idah:80]

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

H.  2  Safar 1441 Na: 1441 H / 002
M.  Jumanne, 01 Oktoba 2019