Enyi Waislamu…Waokoeni Watoto wa Yemen!

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

(Imetafsiriwa)

Mnamo 21/11/2018, ripoti ya Shirika la Uingereza la Okoa Watoto ilisema kuwa takribani watoto 85,000 chini ya umri wa miaka mitano wamekufa kutokana na ukosefu wa lishe bora ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya vita ndani ya Yemen.  Idadi hii pekee ni sawa na jumla ya idadi ya watoto walioko chini ya miaka mitano ndani ya Birmingham, jiji la pili kubwa ndani ya Uingereza.

Ripoti hii haikujumuisha wale waliokufa zaidi ya miaka mitano na wale waliouliwa na miili yao midogo kupasuliwa kuwa vipande kwa mabomu au waliokuwa kama “mazimwi” kutokana na ukame na majanga! Je ingelikuwa ni Uingereza, Marekani na Magharibi kwa jumla ndiyo waliopoteza kiasi hicho cha idadi ya watoto wao, ungelikuwaje msimamo wa kimataifa kuhusiana na kupotezwa kwa maisha ya watoto wasiokuwa na makosa?

Lakini watoto wa Yemen ni kama mayatima juu ya meza za wasiokuwa na thamani, wasiokuwa na wakuwalilia na wakuwaunga mkono, kama bakuli ambalo mataifa yanaitana kuja kuliteka, ikiwa ni katika moja ya sura za kutisha za mzozo wa Uingereza-Marekani ndani ya eneo hili. Baya zaidi ni kuwa wale wanaopigana na kumwaga damu, wanaoleta njaa na kuhamisha watu wa Yemen ni wale ambao ni wa moja katika damu, itikadi, lugha na Dini! Ni nchi za muungano wa Oparesheni ya Msingi wa Kimbunga ya kuunga mkono uhalalishaji wa Rais Hadi na kwa upande mwingine Iran inawaunga mkono wanamgambo wa Houth, yote ni katika mvutano kwa ajili ya mamlaka na utajiri. Vita vya Yemen vinakaribia mwisho wa mwaka wa nne wa vita vya maangamivu ambavyo watu wake wanavilipia gharama kubwa.

Mwezi jana, Umoja wa Mataifa ilitoa onyo kuwa wa Yemen milioni 14 wanakaribia tishio la ukame, ilhali Yemen ina bahari ya utajiri ikiifanya kuwa Hazina ya Mashariki. Yemen ina beseni kubwa la madini ya graniti na kokoto ndani ya Mashariki ya Kati na ina hifadhi kubwa ya pili ya gesi ya kawaida ndani ya ulimwengu wa Kiarabu ya kuweza kusuluhisha janga la ukame, maradhi, umasikini na uhamisho. Madini, dhahabu, shaba, mafuta, kilimo na uvuvi yatosha kujitosheleza kwa karne bila maadui. Kiuhakika, iko katika eneo zuri kijiografia kutokana na kuiangalia Chanel ya Bab al-Mandab ambayo inadhibiti biashara ya kiulimwengu kati ya Mashariki na Magharibi. Lakini utajiri huu uliopotea ndiyo uliyoifanya Magharibi “kuimezea mate” na kuipelekea Yemen katika maangamivu na ukosefu wa amani; watu wake wanauliwa na kila dakika kumi mtoto wa Yemen anakufa kwa njaa na maradhi.

Sisi katika Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunawalani watawala  wote, Waarabu, Waislamu na wasiokuwa Waarabu kila mmoja wao kutokana na yanayoendela Yemen na kwa watu wake hususan watawala wa dola za Guba ambazo zimeizunguka Yemen kutoka kila upande ambao wameshirikiana katika uvunjaji na mauaji kama watawala wa Saudi Arabia na UAE. Napia tunailani Iran na wanaoshiriki katika mzozo huu na kuuchochea moto wake kitaifa, kieneo na kimataifa. Na tunawalani wale wote ambao wanajitia hamnazo juu ya janga la Yemen na kuifunga mipaka jirani na kuwadhibiti hata watoto Mukhlisina wa nchi zao wasitoe usaidizi, mfano kama mtawala wa Oman ambaye ameifanya ardhi yake kuwa ni kaburi la umbile la Kiyahudi na sehemu ya kijeshi na makubaliano ya kisiasa! Majirani wanatakiwa kunusuriana kati yao hususan kama ni wamoja katika Dini, itikadi na historia. Lakini dola za Guba zimebadilisha mambo na kumfanya jirani kuwa adui wa jirani, msaliti au mpiga njama dhidi yake, ilhali Iran inawasha moto wa vita kwa silaha zake na kuwaunga mkono Houthi kwa sura sawa ya kimadhehebu

Mtume (saw) alisema;

«إِذَا مَرَّ بِكُمْ أَهْلُ الْيَمَنِ يَسُوقُونَ نِسَاءَهُمْ، وَيَحْمِلُونَ أَبْنَاءَهُمْ عَلَى عَوَاتِقِهِمْ، فَإِنَّهُمْ مِنِّي، وَأَنَا مِنْهُمْ»“ Lau watu wa Yemen watawajieni wakiwa katika mjumuiko wa wanawake wao huku wakiwa wamebeba watoto wao mabegani mwao, wao ni katika mimi  na mimi ni katika wao.”

[At-Tabarani]

Hali ya Yemen na watu wake na uharibufu unaotokea ni masikitiko makubwa. Wanauliwa mbele zetu, tunahuzunika kama Waislamu tumeachana na maamrisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambayo aliyataja katika Hadith nyingi na kuwasifu na kuwaombea dua mara tatu:

«اللَّهُمَّ بَارِكْ لَنَا فِيْ شَامِنَا وَيَمَنِنَا»“Ewe Mwenyezi Mungu ibariki Sham yetu na Yemen yetu.” Tumekwenda kinyume na hali zetu, ambazo zinatuunganisha safu zetu na mioyo yetu.

Ni Khilafah pekee kwa njia ya Utume inayoweza kupambana na Kafiri Mmagharibi ambaye ndiye mlanjama dhidi ya Yemen na kusitisha uadui wao, na kumuhesabu kila msaliti na kuisitisha mikono yake iliyojaa damu za ndugu zake na kusitisha vita baina yao na kuondosha vyanzo na sababu zake na kurudisha khair na baraka kwa Yemen. Mtume (saw) alisema:

«جَاءَ الْفَتْحُ، وَجَاءَ نَصْرُ اللَّهِ، وَجَاءَ أَهْلُ الْيَمَنِ»، فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا أَهْلُ الْيَمَنِ؟ قَالَ: «قَوْمٌ رَقِيقَةٌ قُلُوبُهُمْ، لَيِّنَةٌ قُلُوبُهُمُ، الْإِيمَانُ يَمَانٌ، وَالْحِكْمَةُ يَمَانِيَةٌ، وَالْفِقْهُ يَمَانٌ».“Fath (ufunguzi) umekuja, ushindi wa Mwenyezi Mungu umekuja, na watu wa Yemen wamekuja.” Mtu akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni nani hao watu wa Yemen? Mtume (saw) akajibu: “ni watu wenye mioyo laini na wapole. Iman ni ya Yemen, Hekima ni ya Yemen na fiqh ni ya Yemen.” [Nasa’i]

Kitengo cha Wanawake

Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

H.  22 Rabi’ I 1440 Na: 1440 AH / 008
M.  Ijumaa, 30 Novemba 2018