Gaza inakufa njaa ilhali Viongozi Wa Kiislamu bado wamebakia Viziwi,mabubu na Vipofu

Habari

Baa la njaa huko Gaza linalosababishwa na mashambulizi ya ‘Israel’ limefikia “hatua ya mwisho,” Wataalamu na mawakili walieleza Shirika la habari NBC, huku vifo vinavyotarajiwa kuongezeka ikiwa Wapalestina hawatapata afueni ya haraka. Na watoto wengi wanaugua utapiamlo watakabiliwa na athari ya kuendelea kwa maisha yote. Wataalamu hao wanaonya. “Dirisha la kuzuia vifo vya watu wengi linafungwa kwa kasi, na kwa wengi tayari limechelewa,” alisema Kirin Lanning, mkurugenzi mkuu wa dharura wa Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji (IRC), shirika la kibinadamu la Marekani. Shirika la Afya Ulimwenguni lilionya kwamba “afya na ustawi wa kizazi kizima cha baadaye” uko hatarini.

Maoni:

Umbo la Kiyahudi linaloungwa mkono na Marekani linabeba jukumu kubwa la baa njaa linaloikumba Gaza. Tangu 2007, Utawala wa Mauaji ya halaiki umedumisha kizuizi cha ardhini, anga na baharini katika mji wa Gaza na hivyo kuzuia kuingia kwa chakula, mafuta na vifaa vya Matibabu kwa watu wa Gaza. Katika ukatili wake, kikosi cha kijeshi cha kiyahudi kinachoongoza operesheni ya kijeshi kililipua mashamba, uvuvi na vifaa vya maji. Imethibitika kuwa Umbo la Kiyahudi linatumia njaa kama njia ya ‘kuwaadhibu’ wakazi wa Gaza na kutoa shinikizo kwa Hamas kwa kufanya maisha kuwa magumu.

Jeshi jeuri la Kiyahudi limeendeleza uovu wake wa kushambulia kwa mabomu msafara wa misaada ya chakula jambo ambalo ni kinyume na kile kinachoitwa sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Kutumia njaa kama njia ya vita ni uhalifu chini ya Kifungu cha 8 cha Mkataba wa Kirumi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Cha kushangaza kufikia sasa, ICC bado haijafungua rasmi mashtaka au kutoa hati za kukamatwa kwa IDF.

Idadi ya watu wenye njaa huko Gaza wanaachiwa wahalifu wa Marekani na mayahudi, kana kwamba wao si wa Ummah mtukufu ambao wana Dini yenye  uungwana usioruhusu hata mtu mmoja kufa njaa. Kimsingi, kuwalisha wenye njaa sio tu tendo la hisani katika Uislamu; ni miononi mwa sifa msingi za Imani inayoakisi dhamira ya Mwislamu katika uwajibikaji wa kijamii, huruma, na kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu.

Mtume (saw) amesema,

«لَيْسَ الْمُؤْمِنُ الَّذِي يَبِيتُ شَبْعَانَ وَجَارُهُ جَائِعٌ»

“Sio Muumini ambaye tumbo lake limejaa na ilhali jirani yake ana njaa.”

Ni ajabu kwamba watu wa Gaza wanakufa njaa, wakati viongozi wa Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu wamebaki viziwi, mabubu na vipofu! Wamechukua kitendo hiki cha aibu cha ukimya kwa sababu wako chini ya matakwa ya Marekani, ambayo yanakidhi matakwa ya Wayahudi. Ni katika muktadha huu utawala wa Misri, Uturuki, Iran na Saudi Arabia kwa pamoja zimekuwa zikitekeleza njama mbovu za Kiyahudi kama vile kuzingirwa kwa Gaza kwa lengo la kuvunja matakwa ya watu wa Gaza ya kujisalimisha kwa adui, na kuutia Umma wote katika hali ya kukata tamaa kabisa.

Watu wa Gaza, pamoja na ukatili huu wote, wamesimama imara juu ya Imani thabiti. Tabia hii kwa hakika imetisha mioyo ya maadui zao. Hakika Mwenyezi Mungu hatapoteza jihadi yao na wala damu haitamwagika bure. Majeshi ya Kiislamu yanapaswa kujua kwamba Mwenyezi Mungu atawawajibisha kwa yale yanayotokea Gaza katika Siku ya Qiyama. Kunyamaza hakuwezi kuwaokoa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Msimamo pekee wa Kiislamu unaopaswa kuchukuliwa ni kuvunja mzingiro, jeshi  kwenda kuikomboa Gaza na Palestina nzima.

Imeandikwa kwa Niaba ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya