Ufupisho wa Suali na Jawabu – 13
Suali
Nini tofauti kati ya ardhi ambayo hatimiliki na manufaa ni ya mtu binafsi, na ardhi ambayo manufaa ni ya mtu binafsi lakini hatimiliki ni ya dola?
Jibu
Hakuna tofauti kati ya ardhi ya “Ushri na Kharaji” ziko sawa isipokuwa katika hali mbili:
- Mwenye ardhi ya Ushri anamiliki ardhi na manufaa yake, na mwenye ardhi ya Kharaji anamiliki manufaa pekee. Hivyo basi, mwenye ardhi ya Ushri anapotaka kuipeana ardhi anayomiliki anaweza kuipeana wakati wowote maanake ni mali yake. Lau mwenye ardhi ya Kharaji atataka kuipeana ardhi hiyo hawezi maanake sio mali yake. Lakini mwenye ardhi ya Kharaji hamiliki hatimiliki bali anamiliki manufaa yake kwa kuwa hatimiliki ni ya Bait ul-Mal (Hazina ya Serikali ya Khilafah).
- Ardhi ya Ushri, inalipiwa Zakat nusu ya kumi. Ardhi ya Kharaji inalipiwa Kharaji.
Kando na nukta hizo mbili ziko sawa. Wenye ardhi hizo wanaweza kufanya watakavyo bora tu iwe ndani ya mipaka ya kiShari’ah: kuuza na kununua, kurithi…n.k.
Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.
Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/ideological-questions/7843.html
Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya
27 Shaaban 1439 Hijria
12 Mei 2018 Miladi