Hizb ut-Tahrir Kenya yafanya amali katika kampeni ya kiulimwengu chini ya kauli mbiu:

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Kumbukizi ya miaka mia ya kuvunjwa kwa Khilafah…Isimamisheni  Enyi Waislamu!

Kwa muongozo wa Amiri wa Hizb ut-Tahrir Mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah MwenyeziMungu amlinde, Hizb ut-Tahrir Kenya ilifaulu kukamilisha kampeni ya kimataifa ya kukumbuka miaka 100 kulingana na kalenda ya Kiislamu tokea kuvunjwa kwa  serikali ya Khilafah mnamo tarehe 28  Mwezi mtukufu wa Rajab 1442 AH/2021.

Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya iliweza kuandaa maandamano baridi kila baada ya swala za Ijumaa kwa wiki nne ndani ya mwezi mtukufu wa Rajab. Maandamano haya yalifanywa katika miji ya pwani; Mombasa, Malindi, Shimoni na Lunga Lunga. Katika jiji kuu la Nairobi yakafanywa katika Msikiti mkubwa wa Jamia, Eastleigh, Huruma na Majengo. Kwenye wiki ya kwanza ya maandamano hayo kuligawanywa taarifa kwa vyombo vya Habari chini ya anwani ‘tokea kuvunjwa kwa Khilafah Kubomelewa nyumba za ibada kumekuwa janga kwa umma mzima wa Kiilamu.’ Na katika wiki ya tatu, Hizb ikagawanya toleo jengine la Makala yaliyokuwa na anwani; Umma wa Kiislamu hawawezi kushindwa na maadui zake”

Kampeni hii pia ilihusisha msururu wa darasa kubwa katika misikiti mbali, sambamba na ugawaji wa kadii zilizokuwa na ujumbe mzito wa utukufu wa Khilafah, athari ya kukukosekanwa kwake, na ufaradhi wa kuisimamisha na kurudi kwake. Tarehe 10 Marchi, 2021 Radio Rahma ilifanya kipindi cha mazungumzo ya mubashara kwa muda wa saa moja na Ustadh Shabani Mwalimu – Mwakilishi kwa vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya, mada katika kipindi hicho ilikuwa ni bishara za kurudi kwa Khilafah. Matembezi na ziara za watu mashuhuri na wenye athari kwa lengo la kuwakumbusha jukumu lao kubwa la kazi ya kusimamisha tena Khilafah.

Amali hizi zilikuwa ni sehemu ya Kampeni ya kiulimwengu iliyofanywa na wanaharakati wa kiume na wa kike wa Hizb ut-Tahrir kote duniani ndani ya mwezi mtukufu wa Rajab mwaka huu wa 1442 AH -2021 CE. Hii ilikuwa ni kukumbusha umma miaka mia ya tukio la kuhuzunisha la kuangushwa kwa utaratibu wa kiutawala ambao ndio aliusimamisha bwana wa manabii na Mitume  Mtume Muhammad Rehma na Amani za MwenyeziMungu zimshukie  utawala ambao uliangaza nuru dunia kwa muda wa karne 13.

Twamuomba MwenyeziMungu SWT atusimamishie haraka Khilafah Rashida kwa mfumo wa utume na hilo katu sio zito kwa MwenyeziMungu. Yeye Allah SWT asema:

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

 

 “MwenyeziMungu Amewaahidi wale walioamini miongoni na kufanya vitendo vizuri, kuwa Atawafanya makhalifa karika Ardhi kama Alivyowafanya makhalifa wale wa kabla yao,  Na kwa yakini Atawasimamishia Dini yao  Aliyowapendelea  na Atawabadilishia  amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu hawanishirikishi na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo basi ndio wavunjao amri zetu.

 [TMQ: 24:55]

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

 Hizb ut Tahrir Kenya