Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Kufuatia mauaji ya halaiki yanayoendelea kufanywa na serikali ya kinyama ya kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza,Hizb ut Tahrir Kenya iliweza kufanya maandamano baridi mnamo siku ya Ijumaa Oktoba 20,2023 katika miji ya Nairobi na Mombasa sambamba na miji mengine ya pwani.
Awali, Hizb ilikua imepanga kuongoza swala ya Ijumaa kwenye uwanja maarufu wa Makadara Jijini Mombasa kusimama pamoja na ndugu zao wa Filastin, hata hivyo kufuatia hali mbaya ya hewa amali hiyo ikahamishiwa msikiti wa Taqwa. Na baada ya swala ya Ijumaa, maandamano hayo yakafanywa nje ya msikiti ambapo mwito ulielekezwa kwa majeshi ya nchi za Kiislamu hususan Misri, Lebanon na Jordan yaweze kuvunja vizuizi walivyowekewa na watawala wao katika kambi zao ili weweze kunusuru oparesheni ya Tufani ya Al-aqsa kukomboa msikiti mtukufu wa Al-aqsa kutoka kwa makucha ya walowezi wa kiyahudi. Maandamano hayo yalitamatika kwa kufanya mkao mfupi na wanahabari kuangazia mashambulizi ya umbo la Kiyahudi dhidi ya watu wa Filastini.
[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini basi ni juu yenu kuwasaidia.
[Al-Anfal 8:72].
Hizb ilikariri kwamba majeshi ya Kiislamu na watu wenye nguvu wana jukumu kubwa la kuunga mkono vijana wa ardhi iliobarikiwa. Umma wa Kiislamu aidha, ukakumbushwa jukumu lao tukufu la kubeba ulinganizi wa kuregesha maisha ya Kiislamu kwa kupitia kusimamisha Serikali ya Khilafah ambayo ndio itakayosukuma kikweli jeshi kupambana na dola ya kizayuni na zile zinazoiunga mkono ambazo ni Amerika na Uingereza.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut Tahrir in Kenya