Hizb ut Tahrir: Tumaini La Ummah

بسم الله الرحمن الرحيم

“Amma baad”, Siku baada ya siku, ummah watambua uwepo wa Hizb Ut Tahrir kati yao. Na kizazi chake kinazidi kuielekea Hizb katika fikra zake na maoni yake. Kuna wale wanaobisha mlango na kukaa na kujadili, na kuna wale wanaotazama kwa mbali huku wakichunguza. Ingawa hivyo, wote wanashirikiana katika nukta ya: “UFUATILIAJI WA KARIBU WA MAENDELEO YA MPANGO WA KHILAFAH YA UMMAH”. Hii imetokana na imani yao ya kina, na kuamini kwao ahadi ya Allah Mtukufu kwa waja wake kuwa atawapa ushindi na umakinifu japo baadhi yao huificha imani hii au huo ufuatiliaji wa mpango wa kihadhara wa ummah.

Ingawa hadi sasa kuna wanaoipinga Hizb Ut Tahrir pamoja na fikra na maoni yake, lakini leo hii ni wachache mno; hao ambao hawataki ummah ujikomboe (Na hilo ni kuwa) hawa maslahi yao yameambatana na uwepo wa ukoloni, vibaraka na mawakala wao. Hivyo, wakawa wajitafutia riziki kwa kubakia tawala zilizopo, ambazo zimetukalia vifuani. Hivi ndivyo ilivyo! Jambo ambalo humfaidisha kafiri mkoloni, ndipo huvivia maadui wa mpango wa ummah kujikomboa. Lengo lao ni kuuchafua mpango huo kupitia mbinu hatari ya upotoshaji wa kisiasa na vyombo vya habari. Ila Pamoja na hizo juhudi kubwa zote, hakika ufuatiliaji wa ummah kwa upande mmoja, na ukoloni kwa upande mwengine, ufuatiliaji wao kuhusu mpango wa Khilafah haujakatika hata siku moja!

Bila shaka, huu ufuatiliaji wa ummah, na kwenda mbio kwao ili kujikomboa kivitendo kutokana na minyororo ya ukoloni na vibaraka wake, na hisia yao ya ndani inayohusiana na ubaya wa kutokuwepo utawala wa Uislamu, na wakaweza kudhihirisha hilo katika miktadha mbalimbali; yote hayo yamefanya Ummah kuwa na matumaini na wanasiasa wa kiislamu, na yeyote anayejifananisha na Makhalifah Waongofu. Pia, kuzidi kwa maswali yao kuhusiana na dhamana za utekelezaji mwema wa Uislamu. Hakika (Hali hii ya ummah) yastahiki kufuatiliwa, kufahamika vizuri na kujua wanachotaka ummah na wanachokisubiri kutoka kwa wanaotaka kuuongoza.

Naam, katika wakati ambao idadi ya silaha za kimataifa zazidi kuandaliwa ili kuumaliza Ummah  kikamilifu,na katika wakati ambao kizazi cha ummah kinasukumwa ili kusahau sheria na  kufanya suluhu na serikali saba za maangamivu kupitia sera za kuachwa na njaa, na kufungua milango ya mali haramu ili zitumiwe katika haramu (wakati yote hayo yakitendeka) Tunakuta kizazi cha Ummah kikimwelekea Mola wao kwa dua na unyenyekevu, wakiwa mmoja mmoja au kwa makundi. Pia (wakimwelekea) kila wanayemwona aweza kusimamia mpango wa ummah na hisia za jamii. Wakiwa na matumaini ya kumpata miongoni mwao mkombozi atakayewatoa kwenye lindi la maasi ya kijumla; lindi ambalo makafiri wakoloni wataka kuwatumbukiza ndani, ili kuwajeruhi vibaya katika dini yao, imani yao, na Mtume wao mtukufu (s.a.w), Asema Allah Mtukufu:

ودّ كثير من أهل الكتاب لو يردونكم من بعد إيمانكم كفارا حسدا من عند أنفسهم

(Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao)

Zaidi ya hayo, kuna wanaoiweka Hizb Ut Tahrir kama mpango mbadala, endapo wachezaji wa sasa watafeli! Wakidhani kuwa Hizb haifahamu kanuni za kazi ya kisiasa za sasa, na mbinu za matendo ya serikali ya kina na vitimbi vyake. Pia, (kuna wanaodhani kuwa) wale waliojichanganya katika nyanja za siasa kwenye serikali za kibepari eti ndio watakaoweza zaidi kuongoza wakati serikali ya Kiislamu itakaposimama! Na huo ni uelewa unaokadhibishwa na njia ya Mtume wa Allah (s.a.w) katika kubadilisha jamii yake na kusimamisha serikali ya kwanza ya Kiislamu. Na (uelewa huo) utakadhibishwa pia na uhalisia wowote ambao hautatumia njia ileile ya kisheria wakati wa kufanya kazi ya kusimamisha serikali ya Kiislamu.

Haya yote, hufanya majukumu ya Hizb na uongozi wake kuzidi kuwa mkubwa siku baada ya siku. Wakiwa baina ya wajibu wa Mungu ambao watakiwa utimizwe kwa upande mmoja na upande mwengine, kuna matumaini ya ummah walionayo juu ya Hizb iliyokita mizizi ndani ya ummah kwani, serikali ya KHILAFAH ni serikali ya kibinadamu kama inavyojulikana na Waislamu. Nayo wala haitawali kiMungu kama inavyojulikana na Wamagharibi chini ya utawala wa kanisa. Lakini mwanadamu atakayesimamia hiyo serikali (ya Khilafah) atakiwa afanikiwe katika majukumu yake kuanzia pale anapoanza tu majukumu yake. Kwa sababu, hakuna maonyesho ya majaribio katika utawala wala hakuna mitihani na semina za mazoezi kuhusu mahusiano ya kimataifa pamoja na viongozi wa ukafiri! Bali yatakiwa serikali ya Khilafah itekeleze majukumu yake mara moja, na ifanikiwe katika kuchukua maamuzi yake na kuyatekeleza. Miongoni mwayo: maamuzi ya amani na vita, na kuunda nguvu kazi zinazotakiwa katika nyanja zote.

Hili hulazimu uwepo wa uelewa na picha kamili ya hali inavyotakiwa kuwa kisiasa mbeleni na wakati wa kutabikisha hukmu juu ya matukio. Jambo hili kwa serikali ya Khilafah hufanana mno na uzalishaji wa nishati za kinukliya. Kwa sababu, hatua zote za utengenezaji hupitia majaribio ya lazima. Ukiachilia mbali kuzalisha nguvu ya nukliya, kwani yatosha kufanya kazi ya kitarakimu, ambayo hakuna nafasi ya kukosa. Ama majaribio ni jambo lisiloruhusiwa kamwe katika nyanja hizi, bali ni lazima kujifunga na kanuni zote za usalama na kuendelea na kazi ya uzalishaji nishati (energy) baada ya picha kuwa wazi akilini.

Vilevile, naweka wazi kwamba siasa ya kisheria na kuhakikisha maslahi ya ummah ya kidini na kidunia, na kujifunga na mtazamo wa kiusimamizi wa serikali, -yote hayo- hulazimu kuwepo watendaji waliomakini (serious) ili kuhakikisha haya mambo yote yanatimia. Pia, umakini wa kufikiria, huwalazimisha tangu na mwanzo waelewe yote yanayotakiwa kutekelezwa vizuri tena kwa kudumu, na kujiandaa na mbinu na vitendea kazi vyote ili kutekeleza mikakati, na kufuatilia mwendo wa huo utekelezaji, na kufanya pupa maendeleo yawe mazuri, na bora zaidi, haya yapatikane ndani ya Hizb hata kabla ya serikali.

Naam, Hizb Ut Tahrir ndio tumaini la ummah na hakika imefanikiwa kuingia katika jamii, baada ya mafanikio makubwa kujaribu kuongea nayo, na Hizb iliweza kuufanya ummah kiujumla, na tabaka la wanasiasa hasa wote wahisi uwepo wake kama chama cha kisiasa na cha kimfumo. Pia, imeweza kufanya fikra zake ziheshimike na ziwe na uzito wa kuzingatiwa na hakika Hizb ilibisha mlango wa jamii kwa muda mrefu ili kuufungua na sasa twaona wazi peupe ni vipi vilivyo nyuma ya mlango vilivyoanguka, kama vile vizingiti na wakaporomoka wote waliokuwa juu yake, kama vile mabawabu na walinzi. Ndipo iweze kuufungua mlango na kusimama mbele ya jamii iliyo na kiu ya kutabikisha Uislamu na kiu ya kusimamisha serikali ya Kiislamu na haipungukiwi isipokuwa tu waruke wenye nguvu katika kizazi cha ummah na kuingia kwenye jahazi la Khilafah ambao walidhani kwa muda kwamba, Wamagharibi hawashindwi, na eti kwamba viongozi wa ummah hawahitimu ila katika vyuo vikuu vya kimagharibi! Sawa kabisa na walivyokuwa wakidhani watawala wa Kifursi na Roma kwamba, wakaazi wa bara Arabu katu hawawezi kuathiri kwenye siasa za kimataifa!

Vigezo vyote vya serikali yenye nguvu vipo kwa idhini ya Allah na upande wenye vigezo na uwezo wa kipekee, wa kutekeleza kikamilifu maono ya ummah, na kuweza kuitikia wito wa kisheria wa kutupilia mbali mipaka hewa na kukomesha hali ya mfarakano – wenye uwezo huo- ni Hizb Ut Tahrir tu (Hizb) ambayo imesimama juu ya msingi wa Uislamu tangu siku ya kwanza hata kama hilo litachukuwa muda kwa baadhi ya kizazi cha ummah kilichodanganywa kulifahamu.

Kwa hiyo, Hizb Ut Tahrir sio tu kwamba ndio tumaini la ummah, bali pia ndio kazi iliyojisamimia yenyewe, imejiandaa kutekeleza uzoefu muongofu na wa kipekee katika utawala, kwa idhini ya Allah na itatimiza ahadi ya Allah Mtukufu, na bishara ya Mjumbe wake (s.a.w) ya kurudi Khilafah Rashidah (ongofu) kwa njia ya utume.

Haya matumaini, na hii kazi, pamoja na kuenea kwa ummah huu ndani ya jamii ya kimataifa na nchi za kimagharibi, yamewatia kiwewe makafiri wakoloni zaidi na zaidi! Ndio maana wakawa wanapapatika kama jogoo aliyechinjwa! Wakawa wapambe wake wafanya kazi kwa bidii ili kuukinaisha ummah wa ushindi na shahada na ambao wakaribia bilioni mbili, kuwa eti ni ummah ulioshindwa! Hivyo basi, hauwezi tena kutaharaki mbele ya amri za mabwana na viongozi wa kimagharibi! Wakitumia msemo wa Ibnu Khaldun kuwa:” Hakika aliyeshindwa, daima huvutiwa mno na kumfuata mshindi katika mtindo wake, mapambo yake, itikadi na tamaduni zake, bali katika hali zake zote”! Lakini….(ويمكرون ويمكر الله والله خير الماكرين)  “Wanapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu anapanga yake na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango”.

 

Mwandishi:

Mhandisi Wisam Al-atrash. Tunisia.