Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu”
Lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Mnamo Jumamosi 27 Oktoba 2018, Hizb ut Tahrir Wilayah ya Tunisia itakuwa mwenyeji wa kongamano muhimu la kimataifa la wanawake lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa kichwa, “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu” ili kutatua janga linaloathiri uwiano na umoja wa ndoa na familia katika jamii ulimwenguni, ikijumuisha ardhi za Waislamu. Tukio hili adhimu litawakusanya wanawake waliopendekezwa kutoka Tunisia na nchi nyinginezo, ambao ni viongozi mashuhuri katika jamii zao au walio na ujuzi kuhusiana na mada hii. Wanachama wakike na wazungumzaji wakike wa Hizb ut Tahrir kutoka Mashariki ya Kati, eneo la Ghuba, Afrika, Asia, Kusini-mashariki ya Asia na Ulaya watawasilisha mada za kongamano hilo. Kongamano litapeperushwa moja kwa moja kwa watazamaji wa kimataifa kupitia lugha tofauti na pia litajumuisha maonyesho ya vitabu. Tukio hili ni kilele cha kampeni nzito ya wiki tatu ya kimataifa juu ya janga la kidunia linaloathiri ndoa na familia leo, iliyoangazia chanzo na suluhisho la Kiislamu kwa matatizo mengi yanayozikosesha maelewano na umoja familia. Kampeni hii pia imejumuisha kutangamana na jamii, mashirika, watu mashuhuri, sekta ya habari na kampeni madhubuti katika mitandao ya kijamii ambayo imepata uungwaji mkono kimataifa.
Familia dhabiti na yenye uwiano ni nguzo ya msingi kwa jamii bora, madhubuti na yenye kufaulu. Familia ni kiungo muhimu kinachotoa msaada wa kiwiliwili, kihisia, kimada na kiusalama kwa wanachama wake na kuhakikisha kuwa kunapatikana uangalizi imara na mwema katika malezi ya watoto. Lakini leo tumekumbwa na janga linaloathiri maelewano na umoja wa maisha ya ndoa na familia katika jamii duniani kote ikijumuisha ardhi za Waislamu. Ndoa imedhoofishwa, ukosefu wa furaha ndani ya ndoa na familia kumekithiri na kumesambaa, umama hauthaminiwi na kukithri kwa kuvunjika familia. Haya yanajiri licha ya kwamba umadhubuti wa maisha ya familia na furaha yake ilikuwa ndiyo sifa bora ya Ummah wa Kiislamu. Huzuni, kugawanyika na kusambaratika kwa maisha ya ndoa na familia kunasababisha madhila makubwa ya kihisia kwa wote wanaohusika na kunaweza kuleta athari mbaya kwa watoto na wanachama wa jamii. Ni muhimu kuwekwe mtizamo wa kina katika kutatua janga hili katika kiungo cha familia na kukiokoa kutokana na maagamivu.
Hivyo basi kongamano hili muhimu litazungumzia mada kama: hatari za kubadilika kwa sura ya muundo wa familia katika ulimwengu wa leo; athari ya kuvunjika kwa familia juu ya watoto, watu binafsi na jamii; dori ya propaganda ya walinganiaji ukombozi wa mwanamke “feminist”; vyombo vya habari na sera za serikali katika kukuza janga hili; ajenda za kitaifa na kimataifa za kuifanya familia za Waislamu na Sheria za Kiislamu za kijamii kuzifanya ziwe za kisekula, ikijumuisha Ripoti ya Kamati Juu ya Uhuru wa Kibinafsi na Usawa nchini Tunisia; kubuni mtizamo mpya wa kutatua vurugu za kinyumbani; pamoja na namna nidhamu za kirasilimali zinavyotoa thamani umama. Kongamano litaelezea kwa kirefu namna misingi na sheria za Kiislamu za Nidhamu ya Kijamii zinavyoweza kivitendo kuilinda ndoa, kuleta utulivu katika maisha ya ndoa, kuinyanyua hadhi ya umama, kusimamisha na kuhifadhi viungo vya familia madhubuti vilivyoungana. Pamoja na hayo, kongamano litaelezea jukumu la utawala wa Kiislamu chini ya dola ya Khilafah iliyosimama kwa njia ya Utume katika kuelimisha, kushajiisha na kulinda miundo ya ndoa na familia. Na pia itawapa msukumo Waislamu kuchukua hatua za kidharura na kimsingi ili kuziokoa familia zisiangamie.
Kongamano litaanza 10am Jumamosi 27 Oktoba na litafanyika katika Makao Makuu ya Hizb ya Sakra Interjection-Ariana. Kongamano la wanahabari litafanyika 10am Alhamisi 25 Oktoba Makao Makuu ya Hizb –Ariana. Wanahabari wakiume wataruhusiwa kuhudhuria kongamano la wanahabari kwa sharti wajifunge na muongozo wakiShari’a, lakini kongamano lenyewe ni la wanawake pekee. Kwa taarifa zaidi kuhusiana na kongamano na vibali kwa wanahabari tafadhali wasiliana na: tahrirconference.2018@gmail.com.
Ukurasa wa Kampeni: http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/dawah/cmo/16024.html
Ukurasa wa Facebook: www.facebook.com/WomenandShariah
Link ya Upeperushaji wa Kongamano Moja kwa Moja: http://www.alwaqiyah.tv/index.php/video/1761/liveevent27102018
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir