Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu”
Mnamo Jumamosi 27 Oktoba, kwa Baraka za Allah, Alhamdulillah, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa ushirikiano na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kwa ufanisi kilifanya kongamano kubwa na la kuvutia la kimataifa la wanawake jijini Tunis lenye kauli mbiu, “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu” ili kuelezea sababu na suluhisho la Kiislamu juu ya mgogoro unaoathiri utulivu na umoja wa ndoa na maisha ya familia katika jamii kote ulimwenguni, ikiwemo biladi za Waislamu. Tukio hili muhimu lilihudhuriwa na zaidi ya wanawake 250 kutoka kote nchini Tunisia wakiwemo mawakili, walimu, walezi wa watoto, wahandisi, wanafunzi wa vyuo vikuu, viongozi wa jamii, na watetezi wa vijana. Hotuba zilitolewa na wanachama wa kike wa Hizb ut Tahrir kutoka Tunisia, Uturuki, Ardhi Iliyo Barikiwa – Palestina, Pakistan, Lebanon, Indonesia, Ghuba la Kiarabu. Uholanzi, na Uingereza. Kongamano hilo vile vile lilipeperushwa moja kwa moja mtandaoni kwa washiriki wa kimataifa na kutazamwa na maelfu ya watazamaji kutoka katika pembe tofauti tofauti duniani.
Hotuba za kongamano zilisheheni namna uhuru usiokuwa na mipaka wa kijinsia wa kimagharibi, nidhamu za kirasilimali zinazo pigia debe ubinafsi na mambo ya kimada, mitazamo ya kitamaduni na desturi zisizokuwa za Kiislamu, na maadili ya utetezi wa wanawake kama vile usawa wa kijinsia yanayo sababisha mkanganyo na mzozo katika dori na majukumu ya kindoa, yote yamechangia kuvunjika na kukosa utulivu katika maisha ya ndoa na familia. Hii ikijumuisha kusababisha viwango vikubwa vya talaka, mahusiano nje ya ndoa, na ghasia za kinyumbani, pamoja na kucheleweshwa na kupungua kwa kasi ya ndoa. Hii ni pamoja na kudunishwa kimakusudi kwa umuhimu wa cheo cha mama, ikipelekea kupuuza ulezi na haki za watoto, pamoja na kuwabebesha wanawake mzigo wa majukumu ya kifedha ya wanaume. Wazungumzaji walifafanua jinsi mgogoro huu unavyochochewa katika ulimwengu wa Kiislamu kupitia vyombo vya habari vya kisekula na sekta ya burudani, mashirika ya utetezi wa wanawake, mijumuiko ya kimataifa ya wanawake kama CEDAW na sera na kanuni za serikali za kisekula zinazo pigia debe maadili ya sumu ya kimagharibi ‘dhidi ya familia’ na itikadi nyenginezo za sumu za kikafiri ndani ya mujtamaa za Waislamu. Hii ni pamoja na ufuatiliziaji wa ajenda kali ya kuchafua na kuingiza usekula familia ya Kiislamu na kanuni ya kijamii – kama vile kushambulia usimamizi wa mwanamune katika Uislamu, na sheria za Kiislamu juu ya urithi, talaka na dori za kijinsia na haki katika ndoa – ili kuuvunja muundo wa familia ya Kiislamu. Hotuba hizo pia zilisisitiza haja ya kubuni mtazamo mpya uliojengwa juu ya Uislamu katika kukabiliana na ghasia za kinyumbani ambazo zimefikia viwango vya majanga katika mujtamaa za Waislamu na za wasiokuwa Waislamu, thibitisho tosha la kufeli wazi kwa miradi ya mashirika ya kisekula ya kimataifa na serikali kutatua barabara tatizo hili.
Nusu ya pili ya kongamano hili iliwasilisha suluhisho la Kiislamu juu ya mgogoro katika maisha ya familia, kimsingi kupitia kuonyesha nidhamu ya kijamii ya Kiislamu ya kipekee kama ilivyo fafanuliwa kikamilifu na kwa upana katika fasihi ya Hizb ut Tahrir. Wazungumzaji walifafanua namna ya mtazamo, maadili na kanuni hizi za kipekee za nidhamu ya kijamii ya Kiislamu za kudhibiti mahusiano baina ya wanaume na wanawake na kupangilia dori, haki na majukumu ya kijinsia katika ndoa na maisha ya familia, yaliyojengwa juu ya msingi wa sheria tukufu za Allah (swt) kuliko maadili potofu ya uhuru wa kibinafsi au ya usawa wa kijinsia, yanavyolea na kulinda ndoa na familia imara zenye furaha. Hii ikiwemo kupunguza ghasia za kinyumbani na mahusiano nje ya ndoa pamoja na kudhamini kile kilicho bora kwa wanafamilia na wanajamii wote kwa jumla. Hotuba pia zilisisitiza jinsi kama Ummah wa Kiislamu tunavyo hitaji kuregesha umuhimu wa cheo cha mama katika jamii zetu kupitia kukumbatia maelekezo ya Uislamu ya dori msingi ya mwanamke kama mke na mama na ambaye anabeba jukumu muhimu mno la kukuza vizazi imara vya mustakbali. Tukio hili pia liliweka sawa ufafanuzi wa Uislamu kuhusu usimamizi wa mwanamume katika maisha ya familia kuwa ni fadhila kwa mwanamke na jukumu kubwa kwa mwanamume kwani amelazimishwa kulinda, kusaidia, kuchunga na kutoa kwa wale alio na mamlaka juu yao kwa huruma, upole na kwa uangalifu. Pamoja na hili, wazungumzaji walifafanua viungo muhimu mno vilivyo fafanuliwa na Uislamu ili kuunda ndoa zenye furaha na kutosheleza kwa msingi wa usuhuba, kama vile kuwa na uchaMungu kuhusiana na ndoa, kupinga ubinafsi na kutafuta kwa bidii thamani ya utulivu katika maisha ya ndoa kama ilivyo amrishwa na Uislamu ili kutafuta Radhi za Allah (swt). Hii ni pamoja na kutabanni kikamilifu dori za ndoa za Kiislamu, majukumu na matarajio katika ndoa yanayoleta utulivu katika maisha ya familia. Mwisho, kongamano hili liliangazia jinsi mageuzi ya ndoa ya kivipande au kanuni za familia au kuanzisha miswada mipya ya wanawake itafeli kutatua mgogoro huu katika maisha ya familia. Bali kinacho hitajika ni mabadiliko ya kikamilifu ya msingi usiokuwa wa Kiislamu, maadili, kanuni na nidhamu za kisiasa ndani ya ardhi zetu, na kuasisi Khilafah kwa msingi wa manhaj ya Utume iliyo jengwa kwa usafi wake juu ya Uislamu na yenye kutekeleza sheria zake zote. Khilafah hii ndio ngome halisi ya familia kwani taasisi na nidhamu zake hulea, hutabikisha, hupigia debe, hutekeleza na hulinda maadili na kanuni za familia ya Kiislamu ndani ya mujtamaa. Dola hii pekee hupangilia mujtamaa kwa msingi wa mtazamo sahihi wa uhusiano kati ya wanamume na wanawake unao hifadhi familia, pamoja na kuisaidia kivitendo kwa nidhamu zake za kisiasa, kiuchumi, kimahakama, kielimu, kijamii na nidhamu nyenginezo pamoja na vyombo vyake vya habari, kutimiza dori za kindoa na kifamilia za Kiislamu, haki na majukumu ili kupata utulivu katika ndoa na maisha ya familia. Hii ikiwemo kurudisha hadhi ya cheo cha mama katika hadhi yake ya kifahari inayostahili katika mujtamaa. Kongamano hilo lilimalizika kwa kuwalingania walio hudhuria na wale walio tazama katika mtandao kujiunga na da’wah tukufu ya Hizb ut Tahrir ili kusimamisha dola tukufu ya Khilafah kwa haraka ili kuiokoa familia kutokana na maangamivu. Hii ilifuatiwa na kudhihirishwa kwa uungaji mkono mkubwa na wa dhati kutoka kwa washiriki wa kusimamisha tena Khilafah kwa haraka ili kumaliza mgogoro katika maisha ya familia.
Kongamano hili lilijumuisha maonyesho yaliyovutia sana waliohudhuria, pamoja na mashairi ya maonyesho ya kuchangamsha yaliyo fanywa na watoto, ikitoa wito wa kuokolewa kwa familia kutokana na maangamivu na dori ya mama ilindwe. Mkutano wa waandishi habari ulifanywa siku mbili kabla ya tukio hili. Kongamano hili na kampeni ya kiulimwengu iliyo tangulia wiki tatu kabla juu ya sababu na suluhisho la Kiislamu juu ya mgogoro katika maisha ya familia iliyo andaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, ilileta mchango mkubwa Alhamdulillah katika kufungua wazi njia ya kutibu migawanyiko katika ndoa na familia na kuunda miundo imara na ya utulivu ya familia.
Hotuba za kongamano, video, na picha pamoja na maalumati ya kampeni zaweza kupatikana katika:
http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/dawah/cmo/16024.html
www.facebook.com/WomenandShariah.
﴾هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا﴿
“Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja (Adam); na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu.” [Al-Araf: 189]
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir