Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mnamo Jumapili 17 Septemba, shirika la msaada la ‘Save the Children’ lilionya kuwa wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh huenda wakafariki kutokana na uhaba wa chakula, makao, na bidhaa msingi za usafi. Zaidi ya Waislamu wa Rohingya 410,000 wamekimbia Myanmar na kwenda Bangladesh tangu Agosti 25 kutokana na kampeni ya mauaji ya halaiki inayotekelezwa na jeshi la Burma. Kwa mujibu wa shirika la UNICEF, asilimia 80% ya wakimbizi hawa ni wanawake na watoto, 92,000 kati yao wako chini ya umri wa miaka 5, na takriban wanawake 52,000 ni waja wazito au wananyonyesha.
Baada ya kutoroka mauaji, ubakaji, na kiwango cha mateso yasiyoelezeka katika jimbo la Rakhine, maelfu ya wanawake wa Kiislamu na watoto wa Rohingya kwa sasa wanakabiliwa na mandhari ya kufariki kutokana na baa la njaa, maradhi, na ukosefu wa makao msingi na matibabu katika kambi za kuogofya za wakimbizi katika eneo la Bazar la Cox nchini Bangladesh. Baada ya kuokoka katika safari ya kutisha, ya khiana ya kutoka Myanmar katika kutafuta hifadhi, wakimbizi hawa wahitaji na wenye fazaiko sasa wanapambana na kujimudu ndani ya mahema yaliyotengezwa kwa mifuko ya plastiki, yaliyojaa matope, yenye msongamano, ambayo hayatoi hifadhi ya aina yoyote kutokana na mvua kubwa ya monsoon, huku maelfu ya wengine, walioshindwa kupata makao wakilala wazi nje. Maelfu ya wanawake wa Kiislamu wa Rohingya wanaohangaika wanalilia watoto wao wachanga mikononi mwao wakipiga foleni kwa masaa mengi huku wakinyeshewa na mvua hii kubwa katika vituo vya ugawanyaji chakula mara nyingi wakiambulia mikono mitupu, wakishindwa kujilisha wao na watoto wao kutokana na uzembe wa kihalifu wa idara za Bangladesh katika kuwakimu vya kutosha Waislamu hawa wanyonge, na wahitaji. Zaidi ya hayo, mnamo Septemba 17, gazeti la ‘The Guardian’ liliripoti kuwa watoto 400 wamezaliwa katika ardhi iso mwenyewe baina ya mipaka ya nchi ya Bangladesh na Myanmar ndani ya siku 15 zilizopita. Baadhi ya wanawake wa Rohingya wamefariki kwa mazazi kutokana na ukosefu wa huduma za afya, baadhi ya watoto hao wakiangamia kutokana na hali mbaya za kambi hiyo au kutokana na mama zao kushindwa kuwanyonyesha kutokana na uhaba wa chakula na maji.
Licha ya kushuhudia maelfu ya wanawake wa Kiislamu, vijana, na watoto wakivumilia maisha haya mabaya, serikali ya kikatili ya Hasina, iliyoleweshwa na uovu wake, itikadi za kinyama za kizalendo, imeweka vikwazo vikali juu ya mizururo ya watu wa Rohingya, ikiwakataza kutoka katika kambi hizo chafu zisizokalika, na hata kuondoka na familia au marafiki, ikitoa wito kwa wenye nyumba kutopangisha nyumba zao kwao, huku ikiwabandika jina la “wageni haramu” na kuamiliana nao kama wanyama walio gerezani, ilhali ni ndugu na dada za Ummah huu! Hakika, anachojali pekee Hasina huyu mkosefu wa utu ni vipi atakavyo wafurusha kwa haraka Waislamu hawa wanaohangaika fukweni mwake, kurudi mikononi mwa serikali ya kinyama ya Myanmar! Ni mwanya mkubwa wa tofauti uliyoje kati ya uongozi huu wa kikatili wa kisekula na Waislamu waheshimika wakarimu wa Bangladesh ambao licha ya kukabiliwa na ufukara, wamefungua milango ya nyumba zao na kutoa kwa ukarimu chakula na makao kwa ndugu na dada zao wanaohitaji, na ambao wameandamana kwa idadi yao kubwa kuitisha hifadhi na usaidizi kwa watu wa Rohingya. Inaonesha tofauti wazi baina ya itikadi safi na fungamano la kidugu la Kiislamu lililomo ndani ya Dini hii ya Haki na Huruma, na maadili na sheria za kikatili za mfumo huu wa kisekula na sera zake za kinyama za kizalendo zilizokumbatiwa na serikali katika kila pembe ya ulimwengu wa Kiislamu ambazo zimejivua jukumu la Uislamu la kuwahami, kuwaokoa na kuwachunga Waislamu hawa wanaohangaika.
Enyi Waislamu! Je, biladi za Kiislamu hazikukithiri; utajiri, rasilimali, na majeshi yake sio makubwa? Basi ni dharura gani iliyopo kiasi ya kuwa ndugu zenu na dada zenu wa Rohingya wanatelekezwa kuteseka katika hali ya unyama kiasi hiki? Ni kwa kugawanywa kikoloni kwa biladi zetu kuwa dola za kizalendo na kulazimisha juu yake serikali vibaraka na nidhamu za kisekula katika maeneo haya ndiko kuliko wapelekea Waislamu kuangamizwa na kutelekezwa huku kukiwa hakuna dola inayojitokeza kuwasaidia. Tunawalingania kung’oa serikali hizi ovu, nidhamu na mipaka bandia yanayougawanya Ummah huu na kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume itakayo watetea watu wa Rohingya na Waislamu wote wanaonyanyaswa. Khilafah itaiunganisha Arakan na kuwakumbatia watu wa Rohingya kama raia kamili wa dola hii, kuwapatia hifadhi ya kweli na kuhakikisha kuwa mahitaji yao yote yameshibishwa kama alivyo amrisha Allah (swt).
[وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
“…Na wakikutakeni msaada katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72]
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 18 Muharram 1439 | Na: 1439 AH / 001 |
M. Jumapili, 08 Oktoba 2017 |