Hukumu Juu ya Hijabu ni Dhidi ya Uislamu kama Mfumo Badala ya Mfumo Uliofeli wa Kisekula wa Kirasilimali

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Siku ya Alhamisi, 24 Januari 2019; Mahakama ya Upeo ya Kenya, ilibatilisha uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya kuwaruhusu wanafunzi watatu Waislamu kuvaa hijabu ndani ya shule.

Sisi Hizb ut Tahrir / Kenya, tunasema yafuatayo:

Kwanza, wakati huu ambapo nchi inakumbwa na uzorotefu wa maadili miongoni mwa wanafunzi kwa kiwango kikubwa cha wasichana wanaokwenda shule wakiripotiwa kutiwa mimba. Ni hukumu mbovu ya mahakama na ambayo inalenga kuwasukuma wasichana waweze kumakinishwa ndani ya mfumo uliooza wa uhuru wa kisekula ambao unaendelea kuangamiza maadili ya jamii nzima. Uamuzi huo ambao umekuja wakati ambapo Waislamu tayari wamo ndani ya makucha ya vitengo vya usalama vya serikali chini ya kisingizio cha kupambana na misimo mikali mfano Ijumaa, 18 Januari 2019 Saa Tano (11am), machifu wawili kutoka Kaunti ya Kisumu waliuvamia msikiti kwa kile walichokiita jaribio la kusimamisha mafunzo ya misimamo mikali! Walisema kwamba walikuwa wanaitikia agizo la serikali la kuwataka Machifu na wasaidizi wao kuwa katika tahadhari na majaribio ya kufanya watoto wa Kenya kuwa na misimamo mikali ili waweze kupambana na hatari za Ugaidi. Hii ni ishara wazi kuwa Kenya inaongozwa na sera za kisekula za kikoloni za kimagharibi ambazo zinataka kuhakikisha kuwa Waislamu wamegawanyika kuwa Waislamu wa misimamo poa (Liberal) na Waislamu wenye misimamo mikali (Radical).

Pili, Uislamu ni mfumo kamili wa maisha unaotoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ambao una nidhamu za kipekee zinazojumuisha nidhamu ya kijamii na nidhamu ya kielimu miongoni mwa nyinginezo. Hijabu inaingia katika nidhamu ya kijamii ya Kiislamu nalo ni vazi ambalo hufunika uchi (awrah) wa mwanamke. Vazi hilo linajumuisha vipande viwili cha chini na cha juu. Kipande cha chini ni vazi pana (lisilokuwa jembamba) ambalo latiririka mpaka chini na kufunika nyayo zake, ambalo mwanamke lazima alivae juu ya nguo zake za kawaida kabla kutoka nje. Ama kipande cha juu (kitambara cha kichwa) au mfano wake au nguo yoyote itakayofanya kazi ya kufinika kichwa kizima, na shingo yote, na ufunuo wa kipande cha chini juu ya kifua. Hili ni amrisho na haliwezi kupingwa na mtu yeyote. Mwenyezi Mungu (swt) Asema:﴿يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ“Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao.” [Al-Ahzab: 59]. ﴿وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيُوبِهِنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاء بُعُولَتِهِنَّ… “Na waangushe shungi (vitambaa) zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao…”[An-Nur: 31]

Tatu, tunawakumbusha Ummah wa Waislamu kuwa lazima wajifunge kikamilifu na Uislamu wao iwe itakavyokuwa. Huku wakimuiga Mtume (saw) na Maswahaba (ra) katika kuwa na subra kama walivyokuwa ndani ya Makkah: «يِأْتِي عَلَى النَّاسِ زَمَانٌ الْقَابِضُ عَلَى دينه كالقابض على الجمر» “Zitakuja zama ambapo kujifunga na dini yako itakuwa kama kushika kaa la moto.”[Sahihi Muslim]. Tunawalingania Waislamu jumla na hususan Wasomi kuwa wasipoteze juhudi zao kwa kutafuta suluhu ndani ya katiba ya kisekula ya kikoloni. Badala yake wajiunge na ulinganizi wa kurudisha tena Maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume ndani ya nchi yenye Waislamu wengi. Ni Khilafah pekee ambayo itauondosha mfumo wa kisekula wa kirasilimali uliokufa na kuoza kwa kuuzika pamoja na majanga yake ndani ya kaburi la sahau. Khilafah itahakikisha kuwa Waislamu watapata Utambulisho wa Kiislamu kwa kutekeleza Shari’ah (Qur’an na Sunnah) kiukamilifu na hivyo kudhamini mazingira mazuri ya kuutekeleza Uislamu kiujumla.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

KUMB: 1440 / 05

Jumamosi, 20 Jumada I 1440H /

26/01/2019 M

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke