Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
Watoto kumi na tano wasio na makao, wengi wao wakiwa wachanga, wamekufa nchini Syria kutokana na baridi kali na ukosefu wa matibabu, kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF mnamo Jumanne 15/1/2019. Watoto, 13 kati yao walio chini ya umri wa mwaka mmoja, walifariki katika kambi ya Al-Rukban kusini mashariki mwa Syria, karibu na mpaka wa Jordan. Al-Rukban na kambi nyenginezo zinakumbwa na uhaba mkubwa sana wa misaada ya kibinadamu, pindi wakimbizi wanapowasili baada ya safari nzito baada ya kukimbia ngome ya mwisho ya ISIS mashariki mwa nchi hiyo. Geert Cappelaere, mkurugenzi wa UNICEF wa eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, alisema “Baridi kali zaidi na hali mbaya za maisha katika Al-Rukban zimesababisha maisha ya watoto kuongezeka kuwa hatarini,” aliongeza, “Kwa mwezi mmoja tu, kwa uchache watoto wanane wamekufa – wengi wao wakiwa chini ya umri wa miezi minne, na mdogo wao zaidi akiwa umri wa saa moja.”
Katika hali hizi ngumu za kimaisha na kibinadamu katika kambi ya Al-Rukban katika mpaka wa Syria na Jordan, ambao karibu wakimbizi 50,000 wa Syria wanaishi, wakimbizi hao wanaishi katika vibanda vya matope na mahema ya plastiki, na wanakumbwa na uhaba mkubwa wa chakula na madawa. Siku chache zilizopita, vyombo vya habari viliripotia habari za mwanamke mkimbizi wa Syria katika kambi ya Al-Rukban aliyejitia moto kutokana na kushindwa kuwapa chakula wanawe watatu. Msemaji wa Idara ya Kibinadamu katika kambi hiyo, Khalid Al-Ali, aliliambia Shirika la Habari la Kijerumani (DPA) mnamo Jumapili, 13/1/2019, kambi ya Al-Rukban ina ukosefu wa miundomsingi ya umeme, maji, usafi, vituo vya matibabu na shule, na kuwasili kwa msimu wa baridi kumechochea zaidi mateso kwa wakimbizi. Kuna ukosefu wa miti katika eneo hili la jangwa kwa ajili ya kuzalisha joto, na kutokuwa na uwezo wa kununua bidhaa za mafuta. Wakaazi wa kambi hizi pia wanateseka kutokana na ongezeko la bei ya chakula na mboga, ambazo ziko juu zaidi kuliko katika maeneo yanayo dhibitiwa na serikali hiyo.
Hali katika kambi nyenginezo za wakimbizi ndani au nje ya Syria sio nzuri zaidi kuliko ile ya kambi ya Al-Rukban, na hali ya watu wa kambi hizi na watoto wao sio nzuri zaidi kuliko ile ya watoto wa kambi ya Al-Rukban. Wote wako sawa katika kukabiliwa na dhuluma, mateso na kutelekezwa. La Hawla Wa La Quwata Ila Billah, Al-Ali Al-Athim.
Usaidizi kwa Waislamu wanyonge nchini Syria na katika biladi nyenginezo za Waislamu sio zawadi au sadaka, bali ni jukumu linalohitajika na udugu wa itikadi ya Kiislamu, na aya na Hadith tukufu zinalingania hili. Allah (swt) asema:
﴾وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ﴿
“Na wakikutakeni msaada katika Dini basi ni juu yenu kuwasaidia,” [Al-Anfal: 72]
Mtume (saw) amesama: «مَا مِنِ امْرِئٍ يَخْذُلُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ، وَيُنْتَقَصُ فِيهِ عِرْضُهُ إِلا خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنِ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَتُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ إِلا نَصَرَهُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ».“Hakuna mtu (Muislamu) yeyote atakayemkhini Muislamu (mwenzake) katika eneo ambalo utukufu wake unakiukwa, na heshima yake kuvunjwa ndani yake isipokuwa Allah naye atamkhini katika eneo lake ambalo anataka nusra Yake, na hakuna mtu (Muislamu) yeyote atakayemnusuru Muislamu (mwenzake) katika eneo ambalo utukufu wake unakiukwa, na heshima yake kuvunjwa ndani yake isipokuwa Allah Azza wa Jalla atamnusuru katika eneo lake ambalo anataka nusra Yake.”
Lakini afueni kwa wenye kudhulumiwa na usaidizi kwa wanyonge ni misamiati isiyokuwemo ndani ya kamusi ya serikali ya Jordan, ambayo yaliyomo ndani ya kamusi yake pekee ni khiyana na njama dhidi ya Waislamu na kadhia zao, na kukamatwa kwa Wabebaji Ulinganizi wanaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah. Serikali hii imefunga mipaka yake usoni mwa wakimbizi wa Syria wanaokimbia dhuulma na maonevu, na kutangaza kuwa ni maeneo ya kijeshi yaliyofungwa na kulazimisha kuzingirwa kwa kambi hizo, kwa kisingizio cha kudumisha usalama wake na kuzuia kupenya kwa “magaidi”.
Ingawa hatuoni misimamo inayo onyesha nguvu na usaidizi kwa wenye kudhulumiwa kwa serikali ya Jordan na mifano yake ya serikali zinazo tawala katika ulimwengu wa Waislamu, licha ya hayo tumeshuhudia msimamo mtukufu kutoka kwa Waislamu wa Jordan wakitaka kufunguliwa kwa mpaka wa Jordan na Syria kwa wakimbizi kutoka kusini mwa Syria na kuwa tayari kwao kuwapokea ndugu zao baada ya serikali hiyo kutangaza kuwa Jordan haiwezi kupokea wakimbizi zaidi kutoka Syria.
Tabia hii haikosekani ndani ya Uislamu, ambao Mtume (saw) ameusifu kama mwili mmoja, na tunaulingania Ummah kuondoa mipaka hii bandia yenye kuleta mgawanyiko unaowazuia Waislamu kutokana na kusaidiana wenyewe kwa wenyewe na kuziunganisha biladi za Waislamu chini ya dola moja, na chini ya bendera moja inayo tawaliwa na Imam mmoja.
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir
H. 13 Jumada I 1440 | Na: 1440 AH / 011 |
M. Jumamosi, 19 Januari 2019 |