Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
Zaidi ya wakimbizi elfu 25 kutoka Syria wanaishi katika takribani vyumba 1400 vilivyojengwa kutokana na simiti katika moja ya kambi zilizoko mpakani eneo la Arsal ambalo lina takribani kambi 126 zinazokaliwa na wakimbizi elfu 60 kutoka Syria.
Mnamo 10/05/2019, maamuzi yalipitishwa na Baraza la Ulinzi wa Juu kuvunjilia mbali majengo hayo ya simiti katika kambi za wakimbizi na kuipa kila familia sehemu iliyojengwa kwa mashiti na mbao ndani ya saa 24 za ubomozi huo wa vyumba vya simiti ambao haukufanyika.
Maelfu ya wakimbizi wanaishi nje peupe ndani ya Lebanon eneo la Arsal lakini mara hii sio kutokana na majanga ya kiasili mfano mafuriko au vimbunga au moto wa kuendelea kutokana na usalama na ulinzi bali ni kutokana na ukosefu wa ubinadamu unaotokana na sheria zinazo lazimishwa kwa nguvu. Kwa upande mwingine hotuba za kiubaguzi na mihemko ya kimadhehebu na chuki dhidi ya wakimbizi, kama ambaye kuta za simiti ambazo zinawalinda kutokana na theluji na mvua katika sehemu wazi zitawaokoa wale ambao nyumba zao, ardhi zao na maisha yao yameibiwa! Kama ambaye hizi kuta za simiti zisizokuwa na hadhi ni nyumba ambazo mtu anahitajia kuishi ndani yake maisha yake yote!
Zaidi ya wakimbizi milioni moja wanaishi katikati ya mizozo ya kila aina ya kisiasa ndani ya Lebanon, wote wakishindana kupata maslahi yao ya kibinafsi, kichama na kimadhehebu. Zaidi ya wakimbizi milioni wanatizamwa kama ambaye ni sehemu ya faili miongoni mwa faili zilizo na patashika katika meza ya makubaliano ili kuweza kuwa ni mchezo kwa kila chama kuweza kushiriki ili kupata maslahi yake na kuboresha hali zao kwa mujibu wa suluhisho lao la kisiasa ili kuwasilishwa na kutekelezwa katika kila mkutano wa wizara na bunge. Zaidi ya wakimbizi milioni moja wanazunguka kati ya wazungumzaji ambao ni wapya katika hali hii na kwa mujibu wa wanasiasa ili kusitisha hali ya kiusalama isiweze kupelekea sintofahamu ya kimadhahebu. Tunasikia michakato ya utu na ubinadamu na ni lazima kuweza kupatilizwa kinyume na upinzani ambao ndio maarufu na ambao ndio unaowatishia wakimbizi na kuwalaumu kuwa ndio sababu ya kudorora kwa uchumi wa Lebanon, kudorora kwa ajira na viwango vya maisha jumla. Hivyo basi, wale waliofurushwa na yule anayekimbia kujiepusha na ukandamizaji wa dhalimu wa Ash-Sham amekuwa analaumiwa kwa ukosefu wa ajira na kutia hasara hazina ya Lebanon na ndio chanzo cha uharibifu wa mazingira na kukatika kwa umeme kama ambaye kabla ya hapo mambo yalikuwa vizuri ndani ya Lebanon!
Enyi watu wa Lebanon, msiwe kama viziwi na vipofu na kupelekea kuwa ni sehemu moja ya michezo inayochezwa na maafisa wafisadi katika utamaduni wao wa kujiweka mbali na majukumu yao ndani ya miaka yao yote katika enzi za utawala wao wa kidhalimu. Wamekimbia majukumu yao ili kuyaepuka hususan yale ya kimsingi kuhusiana na kufanya maamuzi na majukumu. Wao ndio ambao wanastahili kuhesabiwa kwa kufeli na sio wakimbizi madhaifu, waliofurushwa, wanaokimbia wasiuliwe na ambao hivi sasa wanakabiliwa na ubaguzi huu ambao umepenya katika nyoyo za wagonjwa na wanasiasa waliojaa chuki wa Lebanon. Mwenyezi Mungu (swt):
( أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَتَكُونَ لَهُمْ قُلُوبٌ يَعْقِلُونَ بِهَا أَوْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ)
“Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo zao za kuzingatia, au masikio ya kusikilia? Kwani hakika si macho yanayo pofuka, lakini zinazo pofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.” [Al-Hajj: 46]
Enyi Waislamu wa Lebanon: Jueni kwamba rizk imo mkononi mwa Mwenyezi Mungu pekee, na kwamba matatizo ya kiuchumi na maisha yanatokana na kukosekana kwa sheria za Mwenyezi Mungu na usambazaji wa utajiri kwa kikundi cha wafisadi ambacho kinaishi kwa kuwaibia watu kutoka mifukoni mwao. Jueni ya kwamba sheria za Mwenyezi Mungu zimefanya ni faradhi kuungana na kaka na dada zako, wakimbizi kutoka Syria, kwani ni kaka na dada zetu katika Dini. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
(إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ)
“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hiyo niabuduni Mimi.”
[Al-Anbiya: 92].
Musiwaruhusu kuwawekea mipaka hii ambayo inagawanya nchi za Waislamu kuwa vijidola. Musiwape sababu ya kusababisha dhulma kwa ndugu zenu kutoka Syria na musiwasaidie wakandamizaji dhidi ya ndugu zenu. Na fanyeni kazi na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume ili itawale kwa sheria za Mwenyezi Mungu ili uadilifu uweze kuenea na dhulma kuondoshwa kutoka kwa wanaokandamizwa.
(وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ)
“Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu.”
[At-Tawba: 105]
Kitengo cha Wanawake katika Afisi ya Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Shawwal 1440 Na: 1440 H / 034
Jumatatu, 17 Juni 2019