Kazi ya Hizb ut Tahrir ni kubeba da’wah ya Uislamu ili kubadilisha hali ya mujtama fisidifu ili kuugeuza kuwa mujtama wa Kiislamu. Inalenga kufanya hivi kupitia kwanza kubadilisha fikra zilizoko leo katika mujtama kuwa fikra za Kiislamu ili fikra hizi ziwe ndio rai jumla miongoni mwa watu, ambao hatimaye zitawasukuma kuzitabikisha na kuzitekeleza. Pili chama hiki kinafanya kazi kubadilisha hamasa ndani ya mujtama kuwa hamasa za Kiislamu ambazo hazikubali chochote isipokuwa kile kinachomridhisha Allah (swt) pekee na kupinga na kuchukia dhidi ya chochote kinachomkasirisha Allah (swt). Hatimaye, chama kinafanya kazi kubadilisha mahusiano katika mujtama yawe mahusiano ya Kiislamu yanayo kwenda kuambatana na sheria na suluhisho za Uislamu. Matendo haya ambayo chama inayafanya ni matendo ya kisiasa, kwa kuwa yanahusiana na mambo ya watu kulingana na hukmu na suluhisho za kisheria, na siasa katika Uislamu ni kuangalia mambo ya watu, ima ki-rai au ki-utabikishaji au yote mawili, kulingana na hukmu na suluhisho za Kiislamu.
Kinachojitokeza katika matendo haya ya kisiasa ni kuulea Umma kwa thaqafa ya Kiislamu ili kuuyeyusha kwa Uislamu na kuutakasa kutokana na itikadi fisidifu, fikra batili na fahamu za kimakosa ikiwemo athari ya fikra na rai za kikafiri.
Kinachojitokeza katika matendo haya ya kisiasa ni mvutano wa kifikra na kisiasa. Kujitokeza kwa mvutano wa kifikra ni kupitia mvutano dhidi ya fikra na nidhamu za kikafiri. Pia hujitokeza kupitia mvutano dhidi ya fikra batili, itikadi fisidifu na fahamu za kimakosa kwa kuonyesha ufisadi na makosa yake, na kuwasilisha wazi wazi hukmu ya Uislamu kuhusiana nazo.
Ama mvutano wa kisiasa, hujitokeza katika mvutano dhidi ya mabepari makafiri, ili kuutoa Umma kutokana na kutawaliwa nao na kuukomboa kutokana na athari yao kupitia kung’oa mizizi yao ya kifikra, kithaqafa, kisiasa, kiuchumi na kijeshi kutoka katika biladi zote za Waislamu.
Mvutano wa kisiasa pia hujitokeza katika kupambana na watawala, kufichua khiyana na njama zao dhidi ya Umma huu, na kuwawajibisha na kuwabadilisha endapo watanyima haki za Umma huu, au kuacha kutekeleza majukumu yao kwake, au kupuuza jambo lolote lake, au kukiuka sheria za Uislamu.
Hivyo basi kazi yote ya chama hiki ni ya kisiasa, ima kiwe madarakani au la. Kazi yake si ya kielimu kwani sio shule, wala kazi yake haihusiani na kutoa hotuba na kuhubiri. Bali kazi yake ni ya kisiasa, ambapo fikra na sheria za Uislamu zinawasilishwa ili kuzitekeleza na kuzibeba kwa lengo la kuziasisi katika mambo ya kimaisha na ndani ya dola.
Chama hiki kinalingania da’wah kwa Uislamu ili utabikishwe, na ili itikadi yake (‘Aqeedah) iwe ndio msingi wa dola yake na msingi wa katiba na kanuni zake. Hii ni kwa sababu ‘Aqeedah ya Kiislamu ni ‘Aqeedah iliyojengeka kupitia kukinaika akili na ni ‘Aqeedah ya kisiasa ambayo kwayo ni chimbuko la nidhamu inayo tatua matatizo yote ya mwanadamu, yawe ya kisiasa, kiuchumi, kithaqafa, kijamii au kadhia yoyote nyengineyo.