Kifo cha Moi: Wakati wa kubaini kwa kina muozo wa mfumo wa uongozi wa Kisekula.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Aliekua rais wa Kenya, Daniel Arap Moi alifariki dunia tarehe 4 February, 2020 akiwa na miaka 95. Moi ni rais wa pili aliyewahi kuhudumu uongozini kwa kipindi kirefu zaidi cha miaka 24 hadi pale alipostaafu mwaka 2002. Viongozi kadhaa duniani wakiwemo marais wakiafrika wameunganana raia wa Kenya katika kuomboleza kifo chake.

Kufuatia kifo chake, sisi Hizbut-Tahrir Kenya tungependa kusema yafuatayo:-

Kifo ni jambo lisiloepukika, na kila mmoja pasi na kujali cheo au mamlaka yake atakionja isipokuwa Mwenyezi Mungu(Swt) pekee. Hivyo kwa uhalisia huu, kifo lazima kiwe ni ukumbusho mkubwa kwa wanadamu wote kwamba maisha ya dunia ni ya muda tu, hivyo kuna haja kubwa ya kubadili tabia zetu za kisiasa, uchumi na jamii ili ziimbatane na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Uislamu umeweka bayana jinsi ya mahusiano ya kuumbwa kwa kufafanua lengo kuu la maisha hapa duniani ni kumuabudu Mwenyezi Mungu na kwamba mahusiano ya kufufuliwa ni kumaanisha kuwa matendo ya wanadamu hapa duniani yatahisabiwa siku ya Hukumu.

Kugawanyika kimaoni juu ya wasifu wa utawala wa Moi, wengi wa wanasiasa wakionekana kufanya juhudi kubwa ya kujaribu kuziba historia yake kuchafuliwa kwa kumpa sifa kedekede, huku wachache sana ndio wakionekana wakieleza ukweli juu ya utawala wake. Haishangazi kuwaona wanasiasa wengi wakiwemo hata wale waliokuwa wakimpinga, kuonekana wakiusifu utawala wake kwani asili wengi wao walilelewa na kukuzwa kisiasa na Moi. Ama wale wanasiasa wanaodai kutaja ubaya wa Moi, kwa hakika hawafanyi hivyo kwa kuwa wana mfumo mwengine wa kiutawala tofauti na ule wa Moi wa kiusekula, aliourithi kwa mtangulizi wake ambaye naye alipewa na mabeberu. Hatua yao hiyo ni jaribio la kuhadaa tu raia wa kawaida kwani wao pia kimsingi huamini Usekula unaotenganisha Dini na siasa. Kwahivyo, kama utawala wowote ule wa Kisekula, uongozi wa Moi ulisheheni matatizo mengi ikiwemo lile la ufisadi. Mfano wa wazi ni Kashfa kubwa kubwa za ufisadi kama ile ya Goldenberg iliokadiriwa kupoteza asilimia 10 ya pato kiujumla la nchi. Moi ambaye anajulikana sana katika kipindi cha ujana wake alikuwa mwalimu ambaye baada ya kuingia tu uongozini alibadilika na kuwakatiya familia yake utajiri nchini Kenya. Jamii ya Kiislamu huko kaskazini mwa Kenya bado inakumbuka mauaji ya kutisha ya halaiki ya Wagalla yaliyofanywa mwezi February, mwaka 1984. Kulingana na Tume ya mapatano Ukweli na Haki ya Kenya, mauaji hayo ambayo hadi sasa idadi ya waliouwawa haijulikani ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika historia ya Kenya. Katika ukanda wa Afrika mashariki, Moi pamoja na viongozi wengine wa eneo hili alikuwa kiungo muhimu sana katika kufanikisha miradi miovu ya kikoloni kama lile suala la kuigawanya Sudan.

Tofauti na usekula, uongozi katika Uislamu ni amana na wala sio kupambika na sera za kuwadhuru raia. Uongozi ni cheo kipasacho kutumiwa katika kutatua matatizo ya wanadamu na kuwaongoza kwenye ufanisi wa hali ya juu maishani. Katika kipindi kifupi cha uongozi wake bwana Mtume(SAAW) kupitia utawala uliokuwa ukitegemea sheria za Mwenyezi Mungu (swt) aliweza kuunda viongozi wengi miongoni mwa raia wake na kuweka mfano mwema wa kuigwa baadaye.Tuna Imani kubwa kuwa kwa kuisimamisha tena utawalawa Khilafah kwa njia ya bwana Mtume(SAAW) katika mojawapo ya mataifa  makubwa ya Kiislamu, hapo ndio ulimwengu utatawaliwa na viongozi wa kweli wasiojiangalia kibinafsi kwani watakuwa zaidi wa kifanya kazi kubwa ya kuboresha raia wao hivyo kuacha athari nzuri kwa watu watakao waacha.

 

Shabani Mwalimu,

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari,

Hizbut-Tahrir, Kenya.

REF: 06/1441 AH

Jumatano 17, Jumada II 1441/

12/02/2020 CE.