Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kufuatia mafanikio ya kampeni yetu ya kiulimwengu na kongamano la wanawake la kimataifa mnamo Oktoba 2018, “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu”, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kina furaha kutangaza uzinduzi wa kurasa zetu mpya za Facebook zinazojitolea kuangazia kadhia zinazo husiana na mgogoro wa kiulimwengu unao athiri “Kiungo cha Familia”. Kurasa hizi mpya, ambazo zitakuwa kwa Kiarabu, Kiingereza, Kituruki na Kiindonesia, zitawasilisha tena shehena ya fasihi zilizo chapishwa katika kampeni na kongamano pamoja na kutafuta mada za ziada kuhusiana na uhalisia, sababu na masuluhisho ya ukosefu wa utulivu na mfarakano unao athiri muundo wa familia katika jamii kote ulimwenguni.
Miundo imara ya familia, yenye mshikamano na utulivu ndio kitovu cha mujtamaa imara, zenye umakinifu na mafanikio. Lakini, leo kiungo cha familia kina poromoka katika jamii kote ulimwenguni, ikiwemo ardhi za Waislamu. Uhuru haribifu wa ngono ulio pitiliza, miondoko ya kimaisha ya uchoyo na ubinafsi, maadili ya kimada ya kirasilimali, fahamu gawanyifu za ukombozi wa wanawake kama vile usawa wa kijinsia na mitazamo ya kitamaduni na matendo yasokuwa ya Kiislamu yamehujumu ndoa, cheo cha mama na kueneza ukosefu wa utulivu katika maisha ya ndoa na familia ambayo hatimaye yameingiza khiyana, na kusababisha janga la kuvunjika kwa familia.
Serikali leo, ima katika Magharibi au Ulimwengu wa Waislamu, ambazo zinatawala juu ya mgogoro huu unaohusisha kiungo cha familia zimethibitisha kushindwa kutoa masuluhisho ya kihakika ili kuzuia au kutatua tatizo hili kuu. Ukweli ni, sera zao na kanuni zao nyingi za kisiasa, kiuchumi na kijamii zimechochea zaidi kuvunjika huku kwa maisha ya familia, ikiwemo kupigia debe kwao uhuru, ukombozi wa wanawake na fikra chafu na miondoko mengineyo ya kimaisha ndani ya mujtamaa zao. Katika ardhi za Waislamu, umakinishaji usekula ndani ya kanuni za kijamii na kifamilia za Kiislamu kupitia serikali za kisekula na nyenginezo zisokuwa za Kiislamu pia imeongezea juu ya mgogoro huu.
Ukosefu wa furaha, kuvunjika na matatizo kwenye ndoa na maisha ya familia husababisha tatizo kubwa la kihisia kwa wote wanaohusika na huenda ikawa na athari mbaya juu ya watoto na mujtamaa. Hivyo basi umakinifu wa hali ya juu unahitaji kupeanwa ili kukabiliana na mgogoro huu katika kiungo cha familia ili kuiokoa kutokana na kuangamia. Hivyo basi kurasa hizi mpya za Facebook zita:
- Angazia hatari za kubadilika kwa sura ya muundo wa familia leo;
- Tambulisha mambo msingi yanayo dhuru ndoa na maisha ya familia;
- Fichua ajenda za kimataifa na kitaifa za kumakinisha usekula ndani ya familia za Kiislamu na kanuni za kijamii;
- Dhihirisha nidhamu ya kijamii ya Kiislamu na kuonyesha jinsi mtazamo wake wa kipekee katika kudhibiti mahusiano ya kijamii na misingi yake na kanuni zake sahihi unavyoweza kulinda ndoa, kukuuza mapenzi na furaha ndani ya maisha ya ndoa, kuinua hali ya cheo cha mama na kuasisi viungo imara vya familia; na
- Fafanua dori muhimu ambayo utawala wa Kiislamu chini ya Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume katika kukuza, kuimarisha na kulinda ndoa imara na viungo vya familia.
Tunawalingania kufuata, kupenda na kusambaza kurasa zetu mpya na maalumati yake. Tunaomba kuwa kwa usaidizi wa Mwenyezi Mungu (swt), kurasa hizi zitakuwa ni njia ya wazi katika kutibu ukosefu wa utulivu uliozikumba ndoa nyingi leo na kuchangia katika kuunda viungo imara na tulivu vya familia.
Linki za Kurasa:
Kiarabu: https://www.facebook.com/SaveTheFamilyAR/
Kiingereza: https://www.facebook.com/SaveTheFamilyEnglish/
Kituruki: https://www.facebook.com/AileyiKurtarTurkiye/
Kiindonesia: https://web.facebook.com/SaveKeluargaMuslim/
Link ya Tangazo la Uzinduzi wa Kurasa hizi: https://youtu.be/nuQAXhbGYIw
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 24 Jumada II 1440 | Na: 1440 AH / 020 |
M. Ijumaa, 01 Machi 2019 |