Kipimo cha Sarafu ya Dola ndio Chanzo cha Mfumuko wa Bei

Habari:

Imekuwa ni wiki ya majanga ndani ya Afrika Mashariki, kutokana na uhaba wa mafuta na kuzidi kwa bei za bidhaa za watumiaji, ilhali eneo likiendelea kujinasua kutoka katika janga la Covid-19 ili kuhuisha uchumi wa dola.

Maeneo mengi hivi karibuni yameshudia uhaba mkubwa wa mafuta, na pale ambapo bidhaa hiyo inapatikana, basi bei yake imepanda viwango vya juu mno.

Gharama ya maisha inazidi kupanda. Nchini Kenya mfumuko wa bei ni asilimia 6.29, Uganda ni asilimia 3.2, Rwanda ni asilimia 4.2, Tanzania ni asilimia 3.8, Burundi ni asilimia 13.3, Sudan Kusini ni asilimia 25 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni asilimia 5. (The EastAfrican, Saturday, 09/04/2022)

Maoni:

Hali ya dhiki inayoendelezwa kutokana na kutiwa minyororo sarafu za mataifa mengine kwa ile inayodaiwa kuwa ni sarafu yenye nguvu ya Dola ya Amerika haingii akilini! Kwa hiyo, jambo hilo linathibitisha uhuru wa kiuhadaifu uliopo katika dunia hii inayotawaliwa na Amerika na taasisi zake za kifedha hususan Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia.

Janga la Covid-19 na mzozo baina ya Urusi na Ukraine umezidisha kasi ya kuzama kwa nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali katika kina ambacho haitarajiwi kunusurika kwani kuanguka kwake kutakuwa na hatari zaidi ikilinganishwa na ile ya 2008. Utabiri mpya wa ukuaji wa uchumi umekitwa juu ya sarabi ili kuwalaza watu walioghadhabika lakini ni vipofu wa kimfumo.

Kuzidi kwa mfumuko wa bei SIO tu ndani ya nchi za Afrika Mashariki, bali duniani kote. Vyombo vya habari vya Magharibi ambavyo daima vinaegemea upande mmoja vimelazimika kupeperusha kuzidi kwa gharama ya maisha inayowakumba raia katika yale yanayoitwa mataifa ya ulimwengu wa kwanza na pili. Yote ikiwa ni natija ya utumwa wa sarafu zao kwa dola. Ama kuhusiana na mataifa ya ulimwengu wa tatu hususan Afrika, yanataabika zaidi kutokamana na utumwa wao wa kikoloni hadi leo!

Kwa mfano nchini Kenya, hivi sasa Dola inabadilishwa dhidi ya shilingi ya Kenya kwa $1 = Ksh117! Tunapouweka muktadha huo katika mahusiano ya Kenya katika usafirishaji bidhaa kutoka ng’ambo na madeni yake ya nje ni janga kubwa. Katika nchi nyingine, hali ni mbaya zaidi. Yote haya ni natija ya kipimo cha sarafu ya dola ambayo haidhaminiwi kwa chochote kile isipokuwa kuwa na matumaini katika Amerika iliyoimarika! ‘Matumaini’ ni kipimo katika nidhamu ya fedha za makaratasi!

Kama Waislamu lazima tusikate tamaa kwa sababu tunayo nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu ambayo imechipuza kutoka kwa Mummba wa ulimwengu, uhai na mwanadamu –Allah(swt). Badala yake tunatakiwa kuelekeza nishati yetu na kuhimili kipindi hichi cha ugumu wa kiuchumi uliozidishwa na kufeli kwa mamlaka ya Amerika na mfumo wake batili wa kirasilimali wa kisekula na nidhamu zake zinazojumuisha sio tu nidhamu kandamizi ya kiuchumi iliyojikita juu ya utozaji ushuru na mikopo ya riba.

Sasa ni wakati wa Waislamu kuwasilisha Uislamu kuwa ni mfumo mbadala ambao una uwezo wa kutatua matatizo yaliyopenya katika nyanja za maisha. Hilo litawezekana kupitia uongozi wenye uwezo wa Dola ya Kiislamu, Khilafah iliyosimamishwa tena kwa njia ya Utume. Khilafah itautekeleza Uislamu kiukamilifu na hususan nidhamu yake ya kiuchumi ambapo sarafu ya dhahabu na fedha itatumika kama kipimo cha kifedha na sio chengine kile! Kwa kuongezea, itafutilia mbali utozaji ushuru watu kwa kuwa Uislamu unalizingatia hilo kuwa ni ukandamizaji kwa njia ya kuwapora mali zao walizo zichuma kwa dhiki. Ama kuhusu riba na aina zake zote haitoruhusiwa. ﴿وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلۡبَيۡعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰاْ “Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba.” [Al-Baqarah 2: 275]. Kwa kuongezea, itajifunga na sera za kujitosheleza kindani ili kuepuka utegemezi wa ng’ambo.

Kujiunga na ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha tena mradi wa Khilafah ndio suluhisho pekee kwa matatizo tofauti yanayo wakabili wanadamu duniani kote. Kuwabadilisha wanasiasa wa kidemokrasia, vyama vyao au kubadilisha katiba au kujiunga na Muungano wa Afrika (AU) au Umoja wa Mataifa (UN) au mifano yake hakutoleta afueni katika hali zetu, kwa sababu chanzo ni wao kuwa watumwa kwa mfumo wa kirasilimali wa kisekula na nidhamu zake zenye sumu. Majanga yataendelea pasina kusita isipokuwa tubadilishe demokrasia, nidhamu ya utawala wa kubahatisha na sehemu yake ichukuliwe na ile ya Khilafah.

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir