Kongamano la BRICS la 2018 Jijini Johannesburg: Jumuiko la Upangaji Njama ya Kuendelea Kuinyonya Afrika Hususan CHINA

Kongamano la BRICS la 2018 Jijini Johannesburg: Jumuiko la Upangaji Njama ya Kuendelea Kuinyonya Afrika Hususan CHINA

Johannesburg, Afrika Kusini ilikuwa mwenyeji wa kongamano la kumi la BRICS lililofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 27 Julai 2018. Mada ya mwaka huu ya kongamano hili ilikuwa, “BRICS Barani Afrika: Ushirikiano kwa Ajili ya Ukuaji wa Pamoja na Ufanisi Shirika katika Mapinduzi ya Nne ya Kiviwanda.” Mada kama hii ni muhimu mno kwa Bara la Afrika ambalo hukadiriwa na wakoloni wa kimagharibi kuwa “bara lisiloustaarabu la ulimwengu wa tatu”.

Brazil, Urusi, India na China ziliunda BRIC mnamo 16 Juni 2009 katika kongamano lao la kwanza lililofanywa mjini Yekaterinburg, Urusi. Kisha baadaye ikawa BRICS baada ya Afrika Kusini kujiunga nayo mnamo 24 Disemba 2010. Mnamo Aprili 2011, Raisi wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alihudhuria kongamano la BRICS la 2011 mjini Sanya, China, kama mwanachama kamili. Kuundwa kwa BRICS kulijiri katika wakati ambapo ulimwengu ulikuwa umezongwa na mgogoro mbaya wa kiuchumi wa mwaka 2008 uliochipuza kutoka Amerika. Hivyo basi, lengo la BRICS lilikuwa ni kuweka mikakati ya mageuzi ya kisiasa na ya kiuchumi ulimwenguni ili kukinzana na yale ya Amerika japo kisiri kama ilivyo thibitishwa na taarifa ya baada ya kongamano hilo la Yekaterinburg, ambapo mataifa ya BRIC yalitangaza haja ya kuwepo “hazina mpya ya fedha ya kiulimwengu”, ambayo itapaswa kuwa “pana, makinifu na inayotabirika”.

Kuanzia mwanzoni mwa kuundwa BRIC na baadaye BRICS ilikuwa ni kukinzana na Amerika. Hivyo basi, Afrika Kusini dola koloni ya Uingereza ya muda mrefu na mshirika wake ilijiunga ili kuyapigia debe maslahi ya bwana wake mkoloni. Ikizingatiwa kuwa Uingereza ilipoteza haiba yake ya kiulimwengu baada ya Vita vya Pili vya Dunia ambapo uongozi wake wa kiulimwengu ulichukuliwa na Amerika. Tangu wakati huo Uingereza imetumia sera mbili kwa Amerika: ya kwanza – inajiunga na Amerika ili kujishindia makombo na pili – inajiunga na washindani wa Amerika ili kuidhuru Amerika. Ama kuhusu kujiunga kwa Afrika Kusini ni katika sera ya pili ya Uingereza kwani China kwa zaidi ya muongo mmoja imeinyakua Afrika kupitia kuupiku kasi uwekezaji wa Amerika. Mnamo 2014, takwimu rasmi zilionesha kuwa China inarekodi ya juu ya dolari bilioni 220 katika biashara kati yake na Afrika.

Kati ya wanachama watano wa BRICS kwa sasa, yule anayeng’ara ndani ya BRICS na kiulimwengu, ni China iliyo na uchumi, ulioupita ule wa Amerika mnamo 2016. China ni mshirika wa kibiashara nambari moja duniani kwa mataifa 138 kati ya mataifa 200 duniani. BRICS pia imeanzisha benki mpya ya Maendeleo (NDP) iliyo na makao makuu yake jijini Shanghai, China na hivi majuzi mnamo 17 Agosti 2017, Benki ya NDP ilifungua rasmi Kituo cha Eneo la Afrika (ARC) jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Benki hii inalenga kuimakinisha ARC kuwa mchangiaji muhimu wa maendeleo ya kudumu ya miundo msingi nchini Afrika Kusini na kama mshiriki muhimu katika ajenda ya maendeleo ya bara hili.

Afrika kiulimwengu inajulikana kama “jaa la bidhaa ambazo mali ghafi yake inatoka ndani yake!” Afrika imebarikiwa na rasilimali nyingi mno lakini kutokana na ukoloni wa kimagharibi uliididimiza katika viwango vikubwa vya umasikini na hali za kimaisha zisizovumilika yakichochewa na watawala vibaraka wanaohudumia maslahi ya mabwana wa kikoloni kuanzia Kusini hadi Kaskazini na Magharibi hadi Mashariki mwa Afrika!  Na sasa mfano wa China na washirika wake walioungana kuendeleza unyonyaji wa Afrika wakiendeleza kile walichokiacha wakoloni wenzao walipokuwa na udhibiti wa moja kwa moja na sasa udhibiti kupitia watawala vibaraka wao. Wakitekeleza sera zile zile lakini wakijifinika guo la “marafiki wa Afrika” mithili ya BRICS iliyoipa kipaumbele Afrika na kufungua ARC kuwalaza Waafrika kutotilia maanani matokeo ya BRICS na hususan mipango ya China ndani ya Afrika. Afrika Kusini kuwepo katika muungano huo ni kuipa uhalali BRICS ndani ya Afrika, kwani mizani ya biashara yake haiko wima ikilinganishwa na wengineo hususan China kama ilivyo thibitishwa na Tebogo Khaas aliyesema, “Dori ya Afrika Kusini katika BRICS yaweza kusifiwa vizuri kama tendo la ukarimu wa kiuchumi na wa kisiasa usiolipika kwa Urusi na China. Kushiriki kwetu katika BRICS kimsingi inadhihirisha uaminifu kwa jumuiya hii na kutoa mwanya wa bidhaa za China na Urusi Afrika – ikiwemo kura katika Umoja wa Mataifa. Lakini, kwa upande mwengine inaikamua Afrika na kubakia kama soko lemavu la wanunuzi wa bidhaa na huduma za Urusi na China

Taarifa hii imethibitishwa na Raisi wa China Xi Jinping katika ziara ya muhula wake wa pili wa mwaka 2018 barani Afrika. Kwa mujibu wa takwimu rasmi za 2016, zinaeleza kuwa “Waagizaji bidhaa wa kubwa kutoka China walikuwa ni 1.Afrika Kusini -dolari bilioni 13.9, 2.Senegal -dolari bilioni 0.87, 3.Mauritius -dolari bilioni 0.85 na 4.Rwanda -dolari bilioni 0.35”. Zaidi ya hayo, hali ya mikopo ya China kwa Afrika kufikia 2015 ilikuwa “1.Angola -deni la dolari bilioni 19.22, 2. Ethiopia –deni dolari bilioni 13.07, 3.Kenya –deni dolari bilioni 6.85 na 4.Sudan –deni dolari bilioni 6.48! Misaada na mikopo yote Afrika iliyopewa na China au NDP ina “masharti yaliyo ambatanishwa nayo ikiwemo kiwango cha riba na kuratibu sera za kitaifa ili kujumuisha maslahi ya China nk.” hili natija yake imeyaacha mataifa ya Afrika yakiteseka kama yalivyoteseka wakati na baada ya enzi ya ukoloni kupitia sera dhalimu za kikoloni na sasa kupitia mashirika ya kifedha yanayoegemea Amerika k.m. Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) ambayo BRICS inajaribu kuupiku uongozi wao wa kiulimwengu.

Utambuzi wa ukombozi wa Afrika uko katika kuukumbatia Uislamu kama mfumo unaotekelezwa kupitia Khilafah. Dola safi na yenye fikra nzito itakayoiwezesha Afrika kuwa bara huru kutokana na njama za warasilimali wasekula zilizo sababishwa na mfumo wao batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake chafu ikiwemo ile nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali inayozunguka baina ya wizi wa rasilimali za bara hili na utoaji mikopo kama uwekezaji ili kuunyonga uchumi zaidi na hivyo basi kuyasambaratisha mataifa haya na kuyashinikiza kwa huruma yao. Khilafah itazitumia rasilimali za Afrika kwa ajili ya Afrika kupitia utekelezaji wa mfumo safi wa Kiislamu utokao kwa Muumba wa viumbe chini ya usimamizi imara wa Khalifah muadilifu na mchaMungu (mtawala wa Khilafah) ambaye utiifu wake uko kwa Allah (swt) pekee na wala sio kwa warasilimali wasekula pamoja na taasisi zao za kirasilimali kama UN, WTO, IMF, WB na NDP nk. Chini ya Khilafah Afrika itakuwa uwanja wa chimbuko la utulivu na ufanisi kinyume na hali yake ya sasa ya vurugu!

Imeandikwa kwa Ajili ya Radio Rahma

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Makala Na.4   Tarehe: Ijumaa, 14 Dhul-Qaada 1439 | 2018/07/27

  1. http://www.brics2018.org.za/
  2. http://www.sais-cari.org/data-chinese-foreign-aid-to-africa/
  3. https://edition.cnn.com/2018/07/18/asia/xi-jinping-africa-visit-intl/index.html
  4. https://www.news24.com/Columnists/GuestColumn/ramaphosas-rubicon-moment-20180211-3