Habari:
Mawaziri wa elimu na wawakilishi wakuu kutoka dola 54 za Afrika walikutana jijini Nairobi kwa siku tatu kwa ajili ya kongamano la ngazi ya juu la Kiafrika juu ya Llimu (PACE) kuanzia tarehe 25 – 27 Aprili 2018. Lengo la kongamano hilo lilikuwa ni kutathmini maendeleo katika utekelezaji wa shabaha zilizo afikiwa kimataifa na kieneo juu ya elimu. Shabaha za kongamano hilo zilijumuisha Lengo la Maendeleo ya Kudumu juu ya Elimu (SDG4) na Mkakati wa Elimu Barani Afrika (CESA) ya kipindi cha 2016-2025. [Chanzo: gazeti la The Star]
Maoni:
Afrika kama bara lilikoloniwa kinguvu kabla na punde tu baada ya Vita vya Pili vya Dunia na mpaka wa leo limebakia kukoloniwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia watawala vibaraka wanaotekeleza ajenda za kikoloni za mabwana zao wakoloni husika. Ukoloni wa Kimagharibi haukutosheka na kunyonya nguvu kazi na rasilimali katika kumakinisha utawala wake juu ya koloni zake; ulilazimika kuangamiza tamaduni na maadili ya wenyeji (dini, lugha, mavazi, nk) na kuyabadilisha kwa miundo mibovu na isiyo ya sawa ambayo mpaka leo wanaendelea kuiga kutoka hatua moja hadi nyengine katika upande wa merekebisho ya sera. Kutokana na ukoloni, wakoloni walitekeleza muundo wao wa elimu uliojengwa kwa msingi wa usekula ndani ya koloni zao. Serikali za kikoloni zilitambua kuwa ili zipate nguvu juu ya koloni sio tu kupitia udhibiti wa kinguvu lakini pia udhibiti wa kifikra. Udhibiti huu wa kifikra ulitekelezwa kupitia elimu. Lengo la elimu ya wakoloni hawa lilikuwa ni kuwaonyesha Waafrika kuwa thaqafa yao ya Kimagharibi Nndiyo bora. Wakoloni walidhani kuwa elimu itawanyanyua Waafrika kiulimwenguni kutokana na ustaarabu wa kimagharibi. Lakini, haja ya wakoloni ya wafanyi kazi wenyeji na wenye ujuzi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na hamu ya kueneza Ukristo iliwafanya wakoloni kutumia elimu kama chombo cha kufikia udhibiti wa kijamii juu ya Waafrika.
Kwa muda wote wa karne nne na nusu zilizopita, thaqafa kuu ya ubaguzi wa rangi na ubwana kwa ngozi nyeupe umeendelea kuhatarisha uwepo wa Waafrika kabla, wakati, na baada ya utumwa wa kikoloni. Vitisho hivi vimewalazimisha Waafrika kufanya marekebisho ya imani, fikra, na tabia zao ili kubakia hai katika sayari ambayo wanahisabiwa kama “Watu wa Ulimwengu wa Tatu”. Leo watawala vibaraka wa wakoloni na duara la wafuasi wao na wapatilizaji fursa wanaojumuisha wasomi na wajuzi waliosomeshwa kwa elimu ya kikoloni ya kimagharibi mpaka leo wanatabikisha na kuendeleza thaqafa hii kuu yenye sumu juu ya msingi wa mfumo wa kisekula wa kirasilimali. Usekula unalingania kutenganishwa dola na dini; hivyo basi ukaipa dola nguvu za kutunga sheria juu ya mambo ya kimaisha kinyume na matakwa ya Muumba. Kutokana nayo zikachipuza nidhamu na fahamu hatari za uhuru wa kijamii, unyanyasaji wa kiuchumi uliojengwa juu ya mikopo ya riba, sera za ubinafsishaji nk., uhuru aina nne (uhuru wa kuabudu, uhuru wa kumiliki, uhuru wa maoni, na uhuru wa kibinafsi/ubinafsi) na nidhamu ya kiutawala ya kidemokrasia, utaifa, uzalendo nk. kote barani Afrika na kwengineko.
Matunda ya utekelezaji wa ‘thaqafa hii kuu ya kimagharibi’ ni maangamivu sio tu kwa Afrika pekee bali kwa ulimwengu mzima hata zile zinazoitwa nchi za ‘Ulimwengu wa Kwanza’. Kiasi ya kuwa hayahitaji kutajwa kwani yamepita mikapa katika maisha ya kila siku yaliyo fichuliwa kwa muozo wa maadili, ubwana wa wachache, kukithiri kwa ukabila na ubaguzi wa rangi, viwango vya kushtua vya ukosefu wa ajira, wizi na uporaji wa rasilimali za kibinafsi na za Ummah kutoka kwa warasilimali walafi nk.
Mwamko wa Afrika uko katika kubadilisha kwake ukoloni wa kisekula wa kirasilimali na badala yake kukumbatia mradi wa Khilafah. Sera ya elimu ya Dola ya Khilafah imeundwa kwa hukmu za kisheria na kanuni za kiidara zinazo husiana na mtaala wa elimu. Hukmu hizi za kisheria zinazo husiana na elimu zimechipuza kutokana na itikadi ya Kiislamu na zina dalili zake za kisheria kama vile masomo yanayo someshwa na kutenganisha baina ya wanafunzi wa kiume na wa kike. Ama kuhusu kanuni za kiidara zinazo husiana na elimu, ni mbinu na miundo inayo ruhusiwa ambayo mtawala aliye mamlakani huikadiria kuwa na manufaa katika utekelezaji wa sera hiyo ya elimu na kufikia malengo yake. Ni mambo ya kimadania yanayo egemea maendeleo na mabadiliko kwa mujibu wa yale yanayo onekana muwafaka zaidi katika kutekeleza hukmu za kisheria zinazo husiana na elimu na mahitaji msingi ya Ummah. Vile vile zaweza kuchukuliwa kutokana na majaribio, ujuzi na utafiti unao ruhusiwa kutoka mataifa mengine.
Nidhamu hii ya hukmu za kisheria na kanuni za kiidara itahitaji vyombo badili vyenye uwezo wa kufikia malengo msingi ya elimu ndani ya Dola ya Khilafah, nayo ni kujenga shakhsiyya ya Kiislamu. Vyombo hivi vitaangalia usimamizi, uendeshaji na kuzihisabu nyanja zote za elimu katika upande wa mtaala, uteuzi wa walimu waliofuzu, ufuatiliziaji wa maendeleo ya wanafunzi masomoni, na usambazaji wa vifaa muhimu vya maabara na vya kielimu vinavyo hitajika katika mashule, taasisi na vyuo vikuu.
Chini ya Uongozi wa kifikra wa Khilafah inayo tekeleza Uislamu kimfumo na nidhamu zake zitokamanazo nao ikiwemo ile ya elimu, Afrika itainuka kwa vipimo vya kiulimwengu katika upande wa hadhara na kuipiku ile ya mabwana zake wakoloni wa kirasilimali. Wakati ni sasa kwa Afrika kujikomboa kutokana na minyororo ya ukoloni wa kirasilimali ambao ni mzizi wa mateso yake na kutupilia mbali makongamano kama haya ya kila mwaka ambayo hayazai matunda yoyote isipokuwa kumakinisha kinyongo cha ukoloni kwake.
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya
#ReturnTheKhilafah
#SimamisheniKhilafah