Ufupisho wa Suali na Jawabu – 6
Kama ilivyosimulia na Muslim kutoka kwa Abu Hurairah (ra) kwamba Mtume (saw) alisema:
“Hairuhusiwi kwa mwanamke anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiama kusafiri safari ya usiku na mchana bila kuweko na mahram”
Katika Hadithi hii tunapata kuwa:
- Mwanamke ameharamishiwa kusafiri peke yake bila mahram ikiwa safari hiyo itakuwa ya siku nzima (saa 24), usiku na mchana.
- Maandishi yanaashiria muda na sio urefu, mfano mwanamkwe asafiri kwa ndege bila mahram kwa kilomita 1,000 kwenda na kurudi kabla kukamilika kwa siku nzima, hilo linaruhusiwa. Lakini, lau atasafiri kilomita 20 kwa kutembea ambayo itamchukua zaidi ya usiku na mchana basi hilo haliruhisiwi bila mahram.
- Katika safari ya mwanamke kinachozingatiwa ni muda anaochukua katika safari na sio suala la kufupisha swala au kuruhusiwa kufuturu ambapo kinachozingatiwa ni urefu wa safari (kilomita 89).
Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/ideological-questions/10000.html
Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya
20 Shaaban 1439 Hijria
06 Mei 2018 Miladi