بسم الله الرحمن الرحيم
Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Amiri wa Hizb ut Tahrir “Juu ya Maswali ya Wanaozuru Ukurasa Wake wa Facebook wa “Kifiqhi”
Jibu la Swali
Kwa: Yahya Abu Zeinah
(Imetafsiriwa)
Swali: Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh.
Mwenyezi Mungu awahifadhi ewe Sheikh wetu na awasaidie kubeba amana, na awatilie nguvu kwa ushindi uliokaribu kwa idhini Yake.
Kwanza, naomba radhi kwa maswali mengi ambayo yawafikia kutoka kwangu. Lakini tumejifunza kwenye hizb kuwa tupekue na tutafiti, ili fikra yetu ibakie kuwa yenye nguvu na safi kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu mtukufu.
Swali langu ni katika usul ul-fiqhi, kuhusu jambo lilo nyamaziwa:
Imekuja katika hadith kama ilivyo kwa Tirmidhi kutoka kwa Salmaan al-Faarisiy, kwamba Mtume (saw) amesema:
(الحَلاَلُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ فِي كِتَابِهِ، وَالحَرَامُ مَا حَرَّمَ اللَّهُ فِي كِتَابِهِ، وَمَا سَكَتَ عَنْهُ فَهُوَ مِمَّا عَفَا عَنْهُ)
“Halali ni yale aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu kwenye Kitabu chake, na haram ni yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu kwenye Kitabu chake, na yale aliyoyanyamazia basi ni miongoni mwa yale aliyosamehe”.
Je, twaweza kufahamu “kunyamaziwa” katika hiyo hadith kwamba ni kunyamazia kuweka sheria katika kipindi cha uteremshaji, yaani kabla ya kukamilika sheria na kuteremka neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu:
(الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِيناً)
“Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.” [Al-Maidah: 3] Kwa sababu kama inavyojulikana, hakuna sheria kabla ya kuja sheria, na kimsingi mtu dhima yake haijafungwa na taklif. Kwani Muislamu alikuwa katika zama za uteremshaji sheria, yuko mbele ya hukmu ambazo zishawekwa, na sheria ishabainisha hukmu yake kwa sifa yake kuwa halali au haramu. Na Muislamu anayatenda kwa msingi wa kuwa ni sheria na kwamba ataenda kuhisabiwa kwayo. Na kuna matendo na vitu ambavyo bado sheria haikuwa imeshuka hadi pale itakapokamilika. Na haya ndio yaliyokusudiwa na Mtume (saw) aliposema,
(وَمَا سَكَتَ عَنْهُ فَهُوَ عَفْوٌ)
“Na aliyonyamazia basi ni msamaha”. Yaani, Muislamu hatohesabiwa kwa hayo mambo, ni sawa iwe kutenda au kuacha. Na Mtume (saw) bila shaka alikataza hayo kuuliziwa na kufanyiwa utafiti, maadamu haijateremka sheria, ili Mwenyezi Mungu asije akawadhikisha Waislamu kwa sababu ya maswali.
Ama baada ya sheria kukamilika na kuteremka neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu:
(الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِيناً)
“Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.” [Al-Maidah: 3] hivyo ikawa hakuna kitu au kitendo kilicho nyamaziwa na kutowekewa sheria yake, kwa sababu, sheria imekusanya hukmu za vitu vyote na matendo yote. Kwa hiyo, hakuna kitu kitendo isipokuwa kina hukmu au ni mahali pa hukmu. Na ni wajibu kwa kila Muislamu kuulizia na kutafuta hukmu ya kila kitendo anachotaka kutenda, tofauti na walivyokuwa Waislamu katika zama za kuteremka sheria.
Sheikh wetu kipenzi, je huu ufahamu waweza kuzingatiwa kuwa sahihi? Pamoja na kujua kwamba mimi natabanni yaliyomo kwenye kitabu chetu cha Ash-Shakhsiya al-Islaamiya juzuu ya tatu, wala katu siendi kinyume nacho in shaa Allah.
Jibu:
Wa Alaikum Salaam Wa Rahmatullahi Wa Barakaatuh.
Yaonekana kuna kifungu kimekutatiza, nacho ni pale unaposema katika swali lako: “na kuna matendo na vitu ambavyo bado sheria haikuwa imeshuka hadi pale itakapokamilika. Na haya ndio yaliyokusudiwa na Mtume (saw) aliposema,
(وَمَا سَكَتَ عَنْهُ فَهُوَ عَفْوٌ)
“Na aliyonyamazia basi ni msamaha”. Yaani, Muislamu hatohesabiwa kwa hayo mambo, ni sawa iwe kutenda au kuacha. Na Mtume (saw) bila shaka alikataza hayo kuuliziwa na kufanyiwa utafiti, maadamu haijateremka sheria, ili Mwenyezi Mungu asije akawadhikisha Waislamu kwa sababu ya maswali”.
Hii sentensi (وما سكت عنه فهو عفو) haimaanishi kwamba hukmu ya hilo jambo haijateremka, bali yamaanisha kuwa hilo jambo ambalo Mtume (saw) amelinyamazia ni halali, yaani mubaah ikiwa “kitu” au (hukmu yake ni) faradhi, au mandub, au mubaah, au makruh ikiwa ni “kitendo”… na tulishawahi kubainisha hilo kwenye jibu letu kuhusiana na swali kama hili tarehe ishirini /Jumada al-Akhirah/1434 H- sawiya na tarehe 5/5/2013 M. na nitakutajia hapa chini kutokana na hilo jibu yale yanayohusiana na hili suala:
1. Hadith zenye kuhusiana na haya:
A. hadith iliyopokewa na Tirmidhi kutoka kwa Salmaan al-Farisy akisema: aliulizwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kuhusu samli, jibini na manyoa akasema:
«الْحَلاَلُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ فِي كِتَابِهِ، وَالْحَرَامُ مَا حَرَّمَ اللَّهُ فِي كِتَابِهِ، وَمَا سَكَتَ عَنْهُ فَهُوَ مِمَّا عَفَا عَنْهُ»
“Halali ni kile alichokihalalisha Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake, na haram ni alichokiharamisha Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake. na alichokinyamazia basi ni katika aliyosamehe”… na katika mapokezi ya Abu Dawud kutoka kwa ibn Abbas:
«فَبَعَثَ اللَّهُ تَعَالَى نَبِيَّهُ، ﷺ وَأَنْزَلَ كِتَابَهُ، وَأَحَلَّ حَلَالَهُ، وَحَرَّمَ حَرَامَهُ، فَمَا أَحَلَّ فَهُوَ حَلَالٌ، وَمَا حَرَّمَ فَهُوَ حَرَامٌ، وَمَا سَكَتَ عَنْهُ فَهُوَ عَفْوٌ»
“…basi Mwenyezi Mungu akamtuma Mtume wake, na akakiteremsha Kitabu chake, na akahalalisha halali yake, na akaharamisha haram yake. Kwa hiyo, alichokihalalisha kitakuwa halali, na alichokiharamisha kitakua haram, na alichonyamazia basi ni msamaha”.
B. Na katika kitabu cha “Al-Sunan ul-Kubraa” cha Bayhaqi, kutoka kwa Abu Tha’alaba (r.a) amesema:
«إِنَّ اللهَ فَرَضَ فَرَائِضَ، فَلَا تُضَيِّعُوهَا، وَحَّدَ حُدُوداً، فَلَا تَعْتَدُوهَا، وَنَهَى عَنْ أَشْيَاءَ، فَلَا تَنْتَهِكُوهَا، وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رُخْصَةً لَكُمْ، لَيْسَ بِنِسْيَانٍ، فَلَا تَبْحَثُوا عَنْهَا».
“Hakika Mwenyezi Mungu amefaradhisha yaliyo lazima, kwa hiyo msiyapoteze. Na ameweka mipaka, kwa hiyo msiivuke. Na amekataza mambo, kwa hiyo msiyafanye. Na mengine ameyanyamazia – kwa ajili ya ruhusa kwenu, wala sio kwa kusahau – basi msiyatafute”.
C. Hadith ya Tirmidhi na Daaraqutni kutoka kwa Ali (ra) asema: wakati ilipoteremka hii aya
(وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً) “Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea.” [Aali-Imran: 97]. Walisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je ni kila mwaka? Akanyamaza. Wakauliza tena: je ni kila mwaka? Akawaajibu:
لَا وَلَوْ قُلْتُ نَعَمْ لَوَجَبَتْ»» “Hapana, na lau ningesema ndio ingekuwa lazima” basi Mwenyezi Mungu akateremsha aya:
(يا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَسْئَلُوا عَنْ أَشْياءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ)
“Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.” [Al-Maida: 101].
Na katika mapokezi mengine ya Daaraqutni kutoka kwa Abu Huraira amesema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْحَجُّ»
“Enyi watu,mumefaradhishiwa kuhiji, kwa hiyo hijini” akasimama mtu akauliza: je ni kila mwaka ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Mtume hakumshughulikia. Kisha akauliza tena: “je ni kila mwaka ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akauliza Mtume: » وَمَنِ الْقَائِلُ»“ na ni nani huyo muulizaji?” Wakajibu: ni fulani… akasema:
«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ قُلْتُ نَعَمْ لَوَجَبَتْ وَلَوْ وَجَبَتْ مَا أَطَقْتُمُوهَا وَلَوْ لَمْ تُطِيقُوهَا لَكَفَرْتُمْ»
“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake! Lau ningelisema ndio basi ingekuwa lazima. Na lau ingekuwa lazima basi mungeshindwa, na lau mtashindwa basi mungekufuru”. Mwenyezi Mungu akateremsha:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَسْئَلُوا عَنْ أَشْياءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُم)
“Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.” [Al-Maida: 101].
2. Na kabla ya kuzama ndani zaidi kuhusu maana yake, ni vizuri kuashiria baadhi ya mambo yanayolazimiana nayo:
A. Kutafautisha kati ya “kitu” na “kitendo” hili ni suala la kifiqhi na usul, wala sio suala la kilugha. Na lau sivyo, basi neno “kitu” kinakusanya na “kitendo” pia. Hivyo hivyo, kugawanywa hukmu za kisheria na kuwa: faradhi/wajib, mandub, mubaah, makruh, haram/mahdhur, rukhsa, azima, sharti, sababu, maani`i, swahih, fasid, na batwil… yote hiyo ni misamiati ya kifiqhi na usul. Na lau utafungua kamusi za lugha ukitafuta maana zake basi hutopata zikiwa kwa maana ya kifiqhi. Na misamiati hii ya kifiqhi na kiusul iliwekwa baada ya zama za Mtume (saw)) na makhalifa waongofu, kama vile tu misamiati ya kinahau: faail na maf-uul… lau utaziangalia kwenye kamusi za kilugha utapata zina maana tofauti kabisa na istilahi ya kinahau.
B. Hivyo kwa msingi huo, popote utakaposoma hadith ya Mtume (saw) au ya maswahaba zake (Mwenyezi Mungu awaridhie) na ukapata neno “shaiun” au “faailun” basi haitomaanisha kuwa yakusudiwa maana ya kiistilahi bali utapaswa kulitafiti ili uone makusudio yake sahihi yataangukia wapi: je ni kwa uhalisia wa kilugha, ama wa ki ada jumla au ada mahsusi, ama ni uhalisia wa kisheria.
C. Ikiwa swali ni kuhusu matamshi maalum na jibu likaja likiwa la kuenea na lenye kujitegemea lenyewe bila ya hilo swali, basi itakuwa ueneaji upo katika maudhui ya swali ambalo limejibiwa, wala haitokuwa makhsusi kwa swali matamshi yaliyo kwenye swali. Kwa mfano: kwenye hadith swahih ambayo imepokewa na Tirmidhi kutoka kwa Abu Said al-Khudri akisema: kuliulizwa: ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Je tutawadhie maji ya kisima cha budhaa? Akajibu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu:
«إِنَّ المَاءَ طَهُورٌ لَا يُنَجِّسُهُ شَيْءٌ»
“Hakika maji ni twahara na hayanajisiwi na kitu”.
Hapa Mtume (saw) ameulizwa kuhusu kisima cha budhaa, lakini jibu limekuja likiwa mbali kuhusu kisima cha budhaa, hakutaja ndani yake kisima cha budhaa, bali alitaja: « «إِنَّ المَاءَ طَهُورٌ لَا يُنَجِّسُهُ شَيْءٌ “hakika maji ni twahara na hayanajisiwi na kitu”. Hivyo, itakuwa ueneaji umehakikishika kwa kujisafisha na maji, ni sawa yawe ni kutokana na kisima cha budhaa au kisima chochote.
Wala haisemwi kuwa maudhui ya ueneaji ni kisima cha budhaa, bali sawa ni kusemwa kwamba jibu ni la kuenea na liko kwenye maudhui yake ambayo imechukuliwa kutokana na jibu wala sio kutokana swali. Yaani, imechukuliwa kutokana na neno lake: ««إِنَّ المَاءَ طَهُورٌ لَا يُنَجِّسُهُ شَيْءٌ “hakika maji ni twahara na hayanajisiwi na kitu” wala sio kutokana na neno: “بئر بضاعة”، [kisima cha budhaa] namaanisha, maudhui yake ni kuhusu kujitwahirisha kwa maji, wala sio kuhusu kisima cha budhaa…
3. Na sasa twakujibu maswali yako:
a) Kuhusu hadith ya Tirmidhi kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu aliulizwa kuhusu samli na jubna na manyoa akajibu:
«الْحَلاَلُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ فِي كِتَابِهِ، وَالْحَرَامُ مَا حَرَّمَ اللَّهُ فِي كِتَابِهِ، وَمَا سَكَتَ عَنْهُ فَهُوَ مِمَّا عَفَا عَنْهُ»… وفي رواية أبي داود «…وَمَا سَكَتَ عَنْهُ فَهُوَ عَفْوٌ»
“Halali ni kile alichokihalalisha Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake, na haram ni alichokiharamisha Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake. Na alichokinyamazia basi katika aliyosamehe”…
Bila shaka kilichofungamanishwa katika neno [“وَمَا سَكَتَ عَنْهُ…”] kinarudi kwa kilicho karibu zaidi nacho neno lake [“وَالْحَرَامُ مَا حَرَّمَ اللَّهُ فِي كِتَابِهِ”،] ikiwa na maana: na alichokinyamazia kimesamehewa, hakikuharamishwa, yaani: basi halali.
Na ueneaji hapa upo kwenye maudhui yake, lakini jibu limekuwa ni la kuenea zaidi kuliko swali na linajitegemea bila hilo swali. Hivyo, maudhui huchukuliwa kutoka kwenye jibu wala sio kutokana na swali. Kwa hiyo (hilo jibu) litaenea kila ambacho hukmu yake ni halali au haramu, sawa iwe ni kuhusu samli, jubna, na manyoa, ama kitu chochote ambacho kitaingia kwenye halali au haramu. Na haya yanaambatana sawa kwa chochote kinachoingia chini tamko “kitu” au “kitendo” kulingana na maana ya kiistilahi. Ikitumika kwa “kitu” basi halali hapa itamaanisha kuwa ni mubaah, na ikitumika kwa “kitendo” basi halali hapa itamaanisha “kisichokuwa haramu” yaani: faradhi, mandub, mubaah, makruh.
b) Kuhusu hadith ya Baihaqiy kutoka kwa Abu Tha’alaba (r.a) kwamba Mtume (saw) amesema:
«وَنَهَى عَنْ أَشْيَاءَ، فَلَا تَنْتَهِكُوهَا، وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رُخْصَةً لَكُمْ، لَيْسَ بِنِسْيَانٍ، فَلَا تَبْحَثُوا عَنْهَا»
“Hakika Mwenyezi Mungu amefaradhisha yaliyo lazima, kwa hiyo msiyapoteze. Na ameweka mipaka, kwa hiyo msiivuke. Na amekataza mambo, kwa hiyo msiyafanye. Na mengine ameyanyamazia – kwa ajili ya ruhusa kwenu, wala sio kwa kusahau – basi msiyatafute”.
Kwenye hadith hii kuna mambo matatu:
Kwanza: kusema kwake: “سَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ”، “amenyamazia vitu vyengine” neno “shai” hapa haikusudiwi maana ya kiistilahi ambayo ni kinyume cha “kitendo” bali linakusanya na kitendo pia. Kwa mfano aya tukufu isemayo:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِنْ تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّهُ عَنْهَا وَاللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ)
“Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur’ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole.” [Al-Maidah: 101]
Na kilichouliziwa ni hajj. Imekuja kwenye tafsir ya Qurtubi (6/330) “hadith ya Tirmidhi na Daaraqutni kutoka kwa Ali (r.a) asema: “ilipoteremka aya hii
(وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً)
“Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea.” [Aali-Imran: 97] watu waliuliza: ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu je, ni kila mwaka? akanyamaza. Wakauliza tena: je ni kila mwaka? Akasema: «لَا وَلَوْ قُلْتُ نَعَمْ لَوَجَبَتْ» “Hapana. na lau ningesema ndio basi ingekua lazima”. Mwenyezi Mungu akateremsha kauli yake:
﴾يا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَسْئَلُوا عَنْ أَشْياءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ﴿
“Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.” [Al-Maida: 101]. Hadi mwisho wa aya.
Na katika mapokezi mengine ya Daaraqutni kutoka kwa Abu Hurairah asema: amesema Mtume wa mwenyezi mungu (saw):
«يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْحَجُّ» “Enyi watu, mumefaradhishiwa kuhiji, kwa hiyo hijini” akasimama mtu akauliza: je ni kila mwaka ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Mtume hakumshughlikia. Kisha akauliza tena: “je ni kila mwaka ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akauliza Mtume: «وَمَنِ الْقَائِلُ» “Ni nani huyo muulizaji?” Wakajibu: ni fulani… akasema:
«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ قُلْتُ نَعَمْ لَوَجَبَتْ وَلَوْ وَجَبَتْ مَا أَطَقْتُمُوهَا وَلَوْ لَمْ تُطِيقُوهَا لَكَفَرْتُمْ»
“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake! Lau ningelisema ndio basi ingekuwa lazima. Na lau ingekuwa lazima basi mungeshindwa, na lau mtashindwa basi mungekufuru”. Mwenyezi Mungu akateremsha:
﴾يا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَسْئَلُوا عَنْ أَشْياءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ﴿
“Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.” [Al-Maida: 101]. Ni wazi kutokana na haya kwamba kilichouliziwa ilikuwa ni hajj, nayo ni “kitendo” na kimeitwa “shai” katika hiyo aya.
Pili: kilichofungamanishwa katika neno [وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رُخْصَةً لَكُمْ] kinarudi kwa kilicho karibu zaidi nacho, nacho ni neno lake [وَنَهَى عَنْ أَشْيَاءَ، فَلَا تَنْتَهِكُوهَا] yaani ina maana kwamba {rukhsa} ni katika katazo la kukata, kwa kidokezi cha ““تَنْتَهِكُوهَا. ikimaanisha alichokinyamazia kimesamehewa, hakikuharamishwa, yaani: basi halali.
Na haya yanaambatana sawa na kilichouliziwa ikiwa ni “shaiun” kwa maana ya kiistilahi. Hivyo basi, halali hapa ni ibaaha na itaingiana na kilichouliziwa ikiwa ni “kitendo” kwa maana ya kiistilahi, basi halali hapa itamaanisha “kisichokuwa haramu” yaani: faradhi, mandub, mubaah, makruh.
Tatu: neno lake (فَلَا تَبْحَثُوا عَنْهَا) ni lenye kushikana na kilichounganisha ((وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ juu ya kiunganganishwa (وَنَهَى عَنْ أَشْيَاءَ، فَلَا تَنْتَهِكُوهَا) ikimaanisha ni halali kwa hiyo msitafute kuhusu uharamu wake, wala haikumaanisha kwamba msitafute hukmu yake kwa upande wa kuwa ni faradhi, mandub…n.k kwa hiyo maana ya hadith ni kuwa kilicho nyamaziwa huwa ni halali, hivyo msitafiti kuhusu uharamu wake, kwa kuhofia isije ikaharamishwa kwa sababu ya kuulizia kwenu. Kama ilivyokuja kwenye hadith ya Bukhari: kutoka kwa Saad bin Abi Waqasw, kwamba Mtume (saw) amesema:
«إِنَّ أَعْظَمَ المُسْلِمِينَ جُرْماً، مَنْ سَأَلَ عَنْ شَيْءٍ لَمْ يُحَرَّمْ، فَحُرِّمَ مِنْ أَجْلِ مَسْأَلَتِهُ»
“Hakika Muislamu mwenye madhambi makubwa zaidi ni yule atakayeulizia jambo ambalo halijaharamishwa halafu likaharamishwa kwa sababu ya kuuliza kwake”
… 25/Jumada Al-Akhira/1434 H- sawiya na 5/5/2013]
Kwa hiyo, iko wazi kutokana na yaliyotangulia kwamba, Mtume (saw) kunyamazia jambo haimaanishi kwamba hakujawekwa sheria, bali yamaanisha ibaaha ikiwa yahusiana na kitu, na itamaanisha kuwa ni faradhi, mandub, mubaah, au makruh ikiwa yahusiana na kitendo. Yaani, kimya cha Mtume (saw) ni uwekaji wa sheria pia kama ilivyo bainishwa huko juu.
Ama suala la kukatazwa kuulizia: hilo ni katika hali ya Mtume kuulizwa kuhusu kitu halafu ajibu au anyamaze. na pindi anapojibu huwa ametoa hukmu kwa uwazi, na ikiwa hakujibu na akanyamaza basi atakuwa ametoa hukmu kwamba hiki kitu au kitendo ni halali. Na kilichokatazawa ni kurudia rudia swali na kukariri, wakati Mtume (saw) ameshalijibu au kalinyamazia.
Na hii haimaanishi kwamba, Muislamu haifai kuulizia kitu au kitendo asichojua (hukmu yake)… imekuja kwenye kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu, juzuu ya tatu, kwenye mlango wa ( (لا حكم قبل ورود الشرع”hakuna hukmu kabla ya kuja sheria” haya yafuatayo:
[Na kwa kuwa imethubutu kwenye Qur`an na Hadith kwamba mtu kama hajui basi aulizie hukmu, na sio kusita na kukosekana hukmu. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:
﴾فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِنْ كُنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿
“Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.” [An-Nahl: 43] na amesema Mtume (saw) katika hadith ya Tayammum kama alivyo pokea Abu Dawud kutoka kwa Jaabir:
«أَلاَ سَأَلُوا إِذْ لَمْ يَعْلَمُوا فَإِنَّمَا شِفَاءُ الْعِيِّ السُّؤَالُ»
“Kwanini wasiulize ikiwa hawajui?! Kwani hakika dawa pekee ya ujinga ni kuuliza”. Hivyo, ikajulisha kuwa asili sio kusita na kutokuwepo hukmu. Kwa hiyo, baada ya Mtume (saw) kutumwa hukmu itakuwa ni ya sheria, na ndio ikawa hakuna hukmu kabla ya kuja sheria. Yaani, juu ya kuwepo dalili ya kisheria kwa suala moja, kwa hiyo, haitolewi hukmu bila dalili, kama ambavyo haitolewi hukmu isipokuwa baada ya kuja sheria, na asili ni kutafutwe hukmu kwenye sheria, yaani kutafutwe dalili ya kisheria juu ya hukmu kutokana na sheria]
Kwa hiyo, kilicho katazwa ni kuulizia jambo ambalo Mtume (saw) ashabainisha hukmu yake, ikawa (mtu) hatosheki na hilo na badala yake akaendelea kuulizia. Akisema: hija ni faradhi basi haulizwi: ni mara ngapi?. Na akiulizwa kuhusu kitu, Mtume akakikutanisha na kitu chengine ambacho hukmu yake yajulikana kuwa ni mubaah, basi ni wajib mtu ajifunge na hilo na wala asirudie kuulizia kwa kusema (kwani haiwezi kuwa wajib?) au mfano wake miongoni mwa vitu vya undani na haswa haswa katika zama za Qur`an kuteremka, ili isije mtu akajiwekea vikwazo mwenyewe naye Mwenyezi Mungu akaamua kumuwekea vikwazo kama ilivyokuja katika aya:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِنْ تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّهُ عَنْهَا وَاللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ)
“Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur’ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole.” [Al-Maidah: 101]
Kama ilivyokuja katika sababu za kuteremshwa aya hii tukufu:
– Imekuja kwenye sunan Tirmidhi: pindi ilipoteremka hii aya:
(وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً)
“Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea.” [Aali-Imran: 97] watu waliuliza: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu je, ni kila mwaka? Akanyamaza. Wakauliza tena: je ni kila mwaka? Akasema: «لَا وَلَوْ قُلْتُ نَعَمْ لَوَجَبَتْ» “Hapana. Na lau ningesema ndio basi ingekuwa lazima”. Mwenyezi Mungu akateremsha kauli yake:
﴾يا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَسْئَلُوا عَنْ أَشْياءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ﴿
“Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.” [Al-Maida: 101]. Hadi mwisho wa aya. Amesema Tirmidhi: na kwenye mlango huu pia imepokewa kutoka kwa ibn Abbas na Abu Hurairah. Asema Abu Isa: hadith ya Ali ni Hasan – gharib kwa njia hii.
– na imekuja katika Sahih ibn Hibban kwamba Abu Hurairah alitaja kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alikhutubu akasema:
«يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ اللَّهَ قَدِ افْتَرَضَ عَلَيْكُمُ الْحَجَّ» “Enyi watu, hakika Mwenyezi Mungu amewafaradhishia kuhiji”, kwa hiyo akasimama mtu akauliza: je ni kila mwaka ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Mtume akamnyamazia mpaka aliporudia mara tatu. Akasema mtume:
»لَوْ قُلْتُ: نَعَمْ، لَوَجَبَتْ، وَلَوْ وَجَبَتْ مَا قُمْتُمْ بِهَا، ذَرُونِي مَا تَرَكْتُكُمْ، فَإِنَّمَا هَلَكَ الَّذِينَ قَبْلَكُمْ بِكَثْرَةِ سُؤَالِهِمْ، وَاخْتِلَافِهِمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ، فَإِذَا نَهَيْتُكُمْ عَنْ شَيْءِ فَاجْتَنِبُوهُ، وَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِشَيْءٍ، فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ«
“Lau ningesema ndio basi ingekuwa lazima. Na lau ingekuwa lazima basi msingeweza kutekeleza. Niacheni madamu nimewaacha, kwani hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu maswali yao mengi, na kutofautiana kwao na mitume wao. Nitakapowakataza chochote basi jiepusheni nacho, na nitakapowaamrisha lolote basi litekelezeni kwa kadri muwezavyo”.
Na pia wamepokea mfano wake: Ahmad katika Musnad yake, Hakim katika Mustadrak, Daaraqutni, na wengineo…
Kwa hiyo, Waislamu hawapaswi kuwa kama mayahudi ambao walipoambiwa: mchinjeni ng`ombe, wakawa wanadadisi sifa na hali za huyo ng`ombe, basi wakawekewa uzito wa sifa zake, na lau wangemchinja tu ng`ombe yoyote ingelitosha.
Imekuja kwenye tafsir ya Tabari: [usemi kuhusu tafsiri ya neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu:
(وَإِذْ قَالَ مُوسَى لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَنْ تَذْبَحُوا بَقَرَةً قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُواً قَالَ أَعُوذُ بِاللَّهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ)
“Na Musa alipo waambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje ng’ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema: Audhubil lahi! Najikinga kwa Mwenyezi Mungu nisiwe miongoni mwa wajinga.“ [Baqara: 67]
Na ilikuwa sababu ya Musa kuwaambia: ﴿إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَنْ تَذْبَحُوا بَقَرَةً﴾ “Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje ng’ombe ” ni yale aliyotuhadithia Muhammad bin Abdi Aqir, asema: alituhadithia AMutamar bin Sulaiman, asema: nilimsikia Ayub kutoka kwa Muhammad bin Sirin, kutoka kwa Ubaida, asema: katika wana wa Israil kulikuwepo mwanaume tasa, akauliwa na walii wake, kisha akambeba na kumtupa nyumba isiyokuwa yake. (alisema) basi kukatokea shari kati yao hadi wakachukua silaha! Wakasema walio na akili miongoni mwao: hivi mwapigana na hali ya kuwa kuna Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko kati yenu?! Basi wakamuendea Mtume wa Mwenyezi Mungu, akawaambia: mchinjeni ng`ombe. wakasema: watufanyia mzaha? Akasema:
(أَعُوذُ بِاللَّهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ * قَالُواْ ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لّنَا مَا هِيَ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ)
“Audhubil lahi! Najikinga kwa Mwenyezi Mungu nisiwe miongoni mwa wajinga * Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni ng’ombe gani? Akasema: Hakika Yeye anasema kwamba ng’ombe huyo…” [Baqara: 67-68] hadi aliposema:
(فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُواْ يَفْعَلُونَ) “Basi wakamchinja, na walikaribia kuwa wasifanye hayo.” [Baqara: 7]. Akasema akapigwa (yule maiti) akawaelezea aliyemuua ni nani. Akasema: na hakuchukuliwa huyo ng`ombe ila kwa dhahabu yenye uzito sawa naye. Na lau wangemchukua ng`ombe yoyote angeliwatosheleza, basi tangu baada ya hapo ikawa muuaji harithishwi…
Akasema na lau hao watu wakati walipoamrishwa kumchinja ng`ombe wangemtafuta ng`ombe yoyote wakamchinja basi angekuwa ni huyo tu. Lakini walijiwekea ugumu wenyewe, na Mwenyezi Mungu naye akawaekea ugumu. Na lau wasingelisema:
﴾وَإِنَّآ إِن شَاء اللَّهُ لَمُهْتَدُونَ﴿
“Na kwa yakini, Inshaallah, Mwenyezi Mungu akipenda, tutaongoka” [Baqara: 70] basi wasingeongozwa kumfikia huyo ng`ombe milele…]
Hivyo basi, bila shaka kuuliza maswali mengi mahali pasipo kuwa pake, hilo ni jambo lilokatazwa.
Natumai hayo yanatosheleza. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi na mwenye hekima zaidi.
Ndugu Yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
11 Rabi ul-Awwal 1443 H
18/10/2021 M
Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri wa Facebook