بسم الله الرحمن الرحيم
Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa
Amiri wa Hizb ut Tahrir
Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Katika Ukurasa Wake wa Facebook
Jibu la Swali:
Kwa: Mustafa Ali Ibrahim
(Imetafsiriwa)
Swali:
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh
Nina swali:
Surah Yunus ayah 90: [فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ] “na Firauni na askari wake wakawafuatia” na Surat Taha ayah 78: [فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ بِجُنُودِهِ] “Firauni akawafuata pamoja na majeshi yake”
Je, hii ina maana kwamba amri ya mtawala na kitendo cha mtawala ni kitu kimoja, ili tunaseme kuwa kusimama kinyume na amri zake ni sawa na kusimama kinyume na matendo yake, tukimaanisha kwamba tunaseme neno la haki mbele ya polisi wake au wasaidizi wake, kama kuzungumza mbele yake? «أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ» “Jihad bora ni kusema neno la haki mbele ya mtawala jeuri”. Shukran.
Una haki ya kubadilisha mpangilio wa maneno wa swali hili, na Mwenyezi Mungu akulipe kheri.
Jibu:
Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh
Kwanza: kuhusiana na ayah mbili ulizozitaja katika swali hili, ambazo ni katika yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Surah Yunus, ayah 90:
[وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْياً وَعَدْواً]
“Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui”, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika Surat Taha, ayah 78:
[فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ بِجُنُودِهِ فَغَشِيَهُمْ مِنَ الْيَمِّ مَا غَشِيَهُمْ] “Firauni akawafuata pamoja na majeshi yake. Basi kiliwafudikiza humo baharini kilicho wafudikiza!” Ni kana kwamba unabainisha tofauti katika maana inayotokana na matumizi ya herufi الواو na herufi الباء katika maneno (askari wake), kama anavyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya ya kwanza: [فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ] “na Firauni na askari wake wakawafuatia”, huku Mwenyezi Mungu Mtukufu akisema katika ayah ya pili:
[فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ بِجُنُودِهِ] “Firauni akawafuata pamoja na majeshi yake”. Maana ya “akawafuata” ni kwamba aliwafuata na akawafikia, kwa mujibu wa yale yaliyotajwa katika vitabu vya Tafsiri.
Lakini ayah ya kwanza [فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ] “Firauni na askari wake”, Kwa mujibu wa lugha, inafahamika kuwa Firauni alikuwa miongoni mwa waliowafuata, ikimaanisha kuwa kumfuata Musa, amani iwe juu yake, na Wana wa Israili (Bani Israil) wanajumuisha Firauni, Mwenyezi Mungu amlaani, na alikuwa miongoni mwa watu wale waliowafuata na kuwafikia. Hii ni kwa sababu الواو katika neno (na askari wake) hapa inaashiria kushiriki, yaani kushiriki kwa Firauni na askari wake katika kuwatafuta Wana wa Israili (Bani Israil).
Ama ayah ya pili: [فِرْعَوْنُ بِجُنُودِهِ] “Firauni pamoja na majeshi yake”. Inaweza kueleweka kutokana nayo kwa mujibu wa lugha kwamba Firauni alishiriki pamoja na askari wake na mwenzao katika kuwasaka, lakini pia inaweza kueleweka kutokana nayo kwa mujibu wa lugha kwamba Firauni hakushiriki pamoja na askari wake na hakutoka pamoja nao, bali alitafuta tu msaada kutoka kwao katika kuwasaka, na hiyo ni kwa sababu neno “ba” katika lugha linaonyesha uandamani na usaidizi. Kwa hiyo neno (pamoja na askari wake) katika ayah hiyo linaweza kutumika kama lugha ya kuambatana, ikimaanisha kwamba Firauni aliandamana na askari wake katika kuwafuata Bani Israil, na pia inaweza kuchukuliwa kuwa ni kutafuta msaada, ikimaanisha inaweza kuwa alikuwa pamoja nao, na inaweza kuwa alitafuta msaada kutoka kwa askari wake ili kuwafuatilia bila ya kushiriki nao, maana yake ni kwamba waliowafuata ni askari wa Firauni bila ya Firauni mwenyewe.
Utambulisho wa mojawapo ya maana hizi mbili (usindikizaji au usaidizi) unadhihirika kutokana na mchanganyiko wa aya hizo mbili:
Ayah ya kwanza ina maana moja katika lugha. Na ni kwamba Firauni, Mwenyezi Mungu amlaani, aliungana nao, yaani, masahaba zake, katika kumkamata Musa (as). Maana ya Aya ya pili yaelekea ni katika lugha ya kuambatanisha, maana yake alifuatana nao katika kumkamata Musa, amani iwe juu yake, na pia yawezekana aliomba msaada, maana yake aliomba msaada kwa askari wake ili kumkamata Musa (as) bila ya Firauni kuwafuata, Mwenyezi Mungu amlaani katika hilo. Kwa sababu maana ya Aya hizo mbili hazipingani, maana ya kuziunganisha Aya hizo mbili ni kwamba Firauni alikuwa na jeshi lake katika kumfuata Musa (as). Yaani الباء katika “pamoja na askari wake” hapa inaashiria maana ya kuandamana, kumaanisha kwamba alikuwa na jeshi lake katika kumfuata Musa, amani iwe juu yake. Hii ni kuhusiana na maana ya Aya hizo mbili.
Pili: Ama Hadithi tukufu iliyotajwa katika swali hili, imepokewa na Al-Tirmidhi katika Sunan yake kutoka kwa Abu Said Al-Khudri kwamba Mtume (saw) amesema:
«إِنَّ مِنْ أَعْظَمِ الْجِهَادِ كَلِمَةَ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ» “Hakika, miongoni mwa Jihad kubwa ni kusema neno la haki mbele mtawala jeuri”. Abu Issa amesema, na katika sura hii kutoka kwa Abu Umamah, na hii hadith hasan ghareeb kwa mtazamo wake. Imetajwa katika Al-Mu’jam Al-Kabir ya Al-Tabarani kutoka kwa Abu Umamah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«أَحَبُّ الْجِهَادِ إِلَى اللهِ كَلِمَةُ حَقٍّ تُقَالُ لإِمَامٍ جَائِرٍ» “Jihad inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni kusema neno la kweli kwa Imam jeuri”. Katika riwaya nyengine ya Al-Tabarani kutoka kwa Abu Umamah, kwamba mtu mmoja alisema katika Jamarat: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni jihad gani iliyo bora? Akasema:
«أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ» “Jihad iliyo bora kabisa ni kusema neno la kweli mbele ya mtawala jeuri.” Yafuatayo yametajwa katika kitabu cha Aoun Al-Ma’boud katika kuielezea Hadithi hii: [… Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri, ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: Jihad bora kabisa. ni neno la uadilifu kwa mtawala dhalimu. Swahaba wa Awn al-Ma’boud alisema:
(Jihad iliyo bora kabisa): Yaani, mojawapo ya bora zaidi, kama inavyo thibitishwa katika riwaya ya Al-Tirmidhi: Hakika, miongoni mwa jihadi kubwa kabisa (Neno la uadilifu) Na katika riwaya ya Ibn Majah kuna neno haki, na linalokusudiwa na neno hilo ni lile linaloamrisha mema au kukataza maovu, sawa iwe ni neno au maana yake, maandishi na mfano wa hayo.
(Kwa mtawala jeuri): Yaani dhalimu. Hakika hii imekuwa ni jihad bora kabisa, kwa sababu anayepigana dhidi ya adui anasitasita baina ya matumaini na khofu, bila kujua atashinda au atashindwa.
Mwenye mamlaka amedhulumiwa mkononi mwake, hivyo iwapo atasema ukweli na kumuamrisha M’aruf (mema), amefichua uharibifu na analenga kuangamia yeye mwenyewe. Hii inakuwa aina bora ya jihad kwa ajili ya kuishinda hofu, kama Al-Khattabī na wengineo walivyosema. (Au mtawala dhalimu (Amiri)): Inaonekana kwamba ni shaka kutoka kwa msimulizi.].
Kutokana na Hadith hii tukufu inaweza kufahamika kwamba jihad iliyo bora zaidi ni kusema neno la ukweli mbele ya sultan dhalimu, sio mbele ya wafuasi wake. Kinachomaanishwa na sultan dhalimu ni mwana mtawala dhalimu, awe rais, mfalme, waziri mkuu, au gavana. Ni lazima awe na mamlaka na utawala ili upendeleo huu utolewe katika kusema ukweli mbele yake.
Lakini hii haimaanishi kwamba hakuna wema katika kusema neno la ukweli mbele ya wafuasi wa mtawala dhalimu. Kusema neno la kweli siku zote ni jambo la kheri na la jema. Hata hivyo, faida maalum ambayo Mtume (saw) aliitaja katika Hadith tunayozingatia ni upendeleo unaohusiana na mwenye mamlaka, yaani, mtawala mwenyewe. Kwa sababu ya umuhimu wa kusema neno la ukweli mbele yake na hatari, ujasiri, na nguvu inayohusika, kama baadhi ya wafasiri wa Hadith walivyotaja:
[… Al-Khattabi amesema: Hakika hiyo ikawa ndio jihad bora kabisa; Kwa sababu anayepigana na adui husitasita baina ya matumaini na hofu, bila kujua atashinda au atashindwa. Mwenye mamlaka amedhulumiwa mkononi mwake, basi iwapo atasema kweli na akamuamrisha M’aruf (mema), amefichuliwa uharibifu, na amejiweka kwenye maangamivu, na hii imekuwa ni aina bora za jihad kwa ajili ya kuishinda hofu. Al-Muzher amesema: Lakini ilikuwa bora zaidi kwa sababu dhulma ya Sultan inamhusu kila mtu chini ya utawala wake, na ni umati mkubwa. Kwa hivyo, ikiwa atakataza dhulma, basi ataleta manufaa kwa watu wengi zaidi ya kumuua kafiri…].
Mazungumzo yote ni juu ya mtawala dhalimu mwenyewe, sio juu ya wafuasi wake, wasaidizi, na askari.
Ndugu Yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
17 Rajab Al-Khair 1445 H
Sawia na 29/01/2024 M
Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook