Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa Mary May, alifanya ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu kuchukua mamlaka mnamo 13 Julai 2016. Alichukua mamlaka baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu David Cameron kutokana na kura ya maoni ya kuiondosha UK katika Muungano wa Ulaya (EU) maarufu Brexit iliyofanyika mnamo 23 Juni 2016 na asilimia 51.9 ya waliopiga kura wakapigia mrengo wa kujiondosha. Hivyo basi Uingereza kupitia Waziri Mkuu Theresa ikaanza mchakato wa kujitoa mnamo 29 Machi 2017 ili kuanza mazungumzo ya kimikataba na EU kabla kujitoa rasmi katika muungano huo mnamo 30 Machi 2019. Wakati muda unayoyoma na huku mazungumzo yakiendelea na EU; upande mwengine Marekani nayo imezusha vita vya kibiashara vya karne ya 21 dhidi ya China na Umoja wa Ulaya ambayo Uingereza bado ni mwanachama kufikia sasa!
Kwa hiyo Uingereza iko mbioni kuhakikisha inajizatiti kiuchumi baada ya kujitoa katika muungano wa EU na pia kuhakikisha kuwa inapambana vilivyo na haiathiriwi na vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Marekani. UK ilianza na kuandaa mkutano wa 11 wa Jukwaa la Kibiashara la Mataifa iliyokoloni (CBF) kwa mara ya kwanza kuwahi kufanyika mjini London ndani ya miaka 20 kati ya tarehe 16 – 18 Aprili 2018. Miongoni mwa kauli mbiu ilikuwa ni ‘kufanya wepesi katika njia za ukuwaji biashara na kubuni mitazamo mipya ya namna ya kuendesha biashara’. (Commonwealth Business Form, 2018). Kisha ikafuata ziara hii katika koloni zake Afrika. Kabla kusafiri Waziri Mkuu huyo alisema kuwa “Afrika imesimama ukingoni ili kucheza dori ya kiuchumi ulimwenguni” na kwamba “Afrika iliyo tajirika na yenye kufanya biashara iko katika maslahi yetu yote.” Akiongezea, “Tunapojiandaa kutoka katika Umoja wa Ulaya, huu ni wakati wa Uingereza kumakinisha na kukazanisha ushirika wake wa kiulimwengu.”(The Guardian, 26/08/2019).Dori ya kila nchi aliyoizuru Waziri Mkuu wa Uingereza ilikuwa kama ifuatavyo:
Kwanza, Jumanne 28 August 2018: Afrika Kusini (SA) ndiyo nchi nambari 2 yenye uchumi mkubwa barani Afrika kwa kiwango cha uzalishaji wa dola bilioni 349.3 (2017, IMF). Na ndiyo nchi kibaraka mpendwa kwa Uingereza Afrika jumla na hivyo basi ndiyo mshirika wa kibiashara mkubwa nambari 1 wa Uingereza. Na ndiyo maana ikawa nchi ya kwanza kufanyiwa ziara na Waziri wa Fedha, Philip Hammond mnamo Jumatano, 14 Disemba 2016 ili kuihakikishia SA kwamba haitoathiriwa na hatua ya Uingereza kujiondoa katika EU (Reuters, 07/12/2016) Kibiashara SA ni “Ni mshirika muhimu wa kibiashara kwa Uingereza, na rafiki wa miaka mingi wa Uingereza ndani ya Afrika na kimataifa. Ndiyo soko letu kubwa la usafirishaji bidhaa Afrika…” matamshi ya Dr Liam Fox, Waziri wa Biashara ya Kimataifa wa Uingereza (GOV.UK 24/01/2017). Kwa sababu hizo SA ilichaguliwa kuwa ya kwanza ili “Kufikia 2022, nataka UK iwe ndiyo nambari moja miongoni mwa nchi 7 ulimwenguni zilizoendelea katika uwekezaji ndani ya Afrika, huku sekta ya kampuni za kibinafsi za Uingereza zikiongoza,” May aliwaambia wafanyi biashara mjini Cape Town, SA. (TheEastAfrican, 28/08/2018). Hivyo basi, SA inatarajiwa kucheza dori ya kuhamasisha mataifa ya kusini na ambayo ina usemi juu yake ili kuyaunganisha na kufanya kazi na bwanake Muingereza kama ilivyoshuhudiwa kwa kutiwa saini mikataba kati ya UK na SA, Botswana, Lesotho, Mozambique, Namibia na eSwatini (Swaziland) ili kuhakikisha kwamba wanaendelea kufanya biashara na UK baada ya UK kujitoa rasmi katika EU ikiwa pamoja na mikataba ya awali inayohusu EU. (GOV.UK 28/08/2018)
Pili, Jumatano 29 Agosti 2018: Nigeria ndiyo nchi nambari 1 yenye uchumi mkubwa barani Afrika kwa kiwango cha dola bilioni 376.3 (2017, IMF). Ni nchi kibaraka mpendwa kwa Uingereza baada ya SA ambayo hivi majuzi ilikuwa chini ya mkono wa Marekani kupitia kibaraka wao Goodluck Jonathan lakini hivi sasa imerudi tena katika mikono ya Muingereza kupitia Muhammadu Buhari. Kwa kuwa Nigeria ndiyo yenye uchumi unaokuwa haraka na pia mkubwa Afrika, na inatarajiwa kuwa nchi ya 3 duniani yenye watu wengi kufikia mwaka 2050 na pia Nigeria ina usemi katika Nchi za Mashariki na Kati ya Afrika. Licha ya kuwa nchi yenye uchumi mkubwa pia ndiyo nchi yenye umasikini zaidi duniani. Kwa sababu hizo UK inatazamia kuboresha biashara na Nigeria ili kupitia kuzishawishi nchi za Kaskazini na Magharibi ya Afrika na pia kupatiliza soko kubwa kutokana na idadi kubwa ya watu wake. “Ikiwa UK inataka kubuni kitu, ziko njia moja au mbili zenye kutia moyo na matumaini ili kuanza sekta ya kibiashara ya mataifa yaliyokoloniwa. Tunazo idadi kubwa za watu mfano Nigeria ambayo itakuwa na watu milioni 320 –kubwa kuliko Marekani chini ya miaka 10 ijayo. Wanapenda bidhaa za Uingereza…Ni soko kubwa la wanunuzi. Kimsingi kunao utajiri mkubwa.” matamshi ya Lord Marland kutoka Odstock -Mwenyekiti wa Baraza la Kibiashara na Uekezaji wa Mataifa yaliyokoloniwa na Uingereza (Premium Times, 29/08/2018). Wakati huo huo kuisadia Nigeria kupambana na kundi Boko Haram ili lisije kuwa kikwazo katika azma ya UK kiuchumi nchini humo wakati huu mgumu ambapo inatarajia kujitoa katika EU.
Tatu, Alhamisi 30 Agosti 2018: Kenya ndiyo nchi nambari 8 yenye uchumi mkubwa barani Afrika kwa kiwango cha dola bilioni 79.5 (2017, IMF). Kenya ni miongoni mwa nchi kibaraka wa Uingereza na hivi sasa ndiyo yenye uchumi mkubwa na ushawishi katika kanda ya Afrika mashariki na ambayo inacheza dori kubwa katika kupambana na Alshabab nchini Somalia. Kwa sababu hizo inatarajia kupatiliza fursa ya ushawishi wa Kenya ili kujipatia soko la kibiashara nchini humo na jirani zake. Na pia kuangalia namna ya kuboresha KDF katika ushirikiano na wanajeshi wa Uingereza walioko nchini katika vita dhidi ya Alshabab ili isiwe kikwazo katika mipango ya kibiashara inayotazamia siku za usoni baada ya kujitoa rasmi katika EU.
Ni wazi kuwa Uingereza inazuru koloni zake kwa maslahi yake na wala sio kwa kuipenda au kuijali Afrika! Bali inaitizama Afrika kama soko huru la bidhaa na huduma zake ili ijipatie faida mara dufu kupitia watu wake wengi! Muhimu tukumbuke kuwa Afrika imezama ndani ya umasikini wa kupindukia na maisha duni yaliyo sababishwa na wamagharibi wakoloni kupitia itikadi yao batili na mfumo wa muovu wa urasilimali ambapo nidhamu jumla ikiwemo hii ya kiuchumi inayolazimisha Afrika kubakia mtumwa na wakoloni kubakia mabwana kupitia watawala wao vibaraka watiifu. Afrika na hususan SA, Nigeria na Kenya kamwe hazitoona matunda ya utulivu kwa kuwa mali zao zitaendelea kuporwa na mataifa ya kikoloni na kubuniwa mizozo kati yao wenyewe kwa wenyewe ili washughulishwe.
Suluhisho msingi ni kwa viongozi wa Afrika kutupilia mbali mafungamano na wakoloni wamagharibi ambao ndio chanzo cha kubakia nyuma kiuchumi na kimaendeleo jumla.Na badala yake kukumbatia mwito wa kiulimwengu wa kusimamisha Serikali ya Kiislamu ya Khilafah. Khilafah itakayosimama kwa njia ya Utume na itakayoendeshwa kwa uchajiMungu kwa misingi ya Qur’an na Sunnah; na sio kwa matamanio na akili finyu kama inavyoshuhudiwa hivi sasa kutoka kwa masekula wa koloni. Khilafah itaipa nguvu Afrika na kuilinda dhidi ya ushawishi muovu wa kimagharibi pamoja na sera zao potofu kwa kuwapa muongozo safi wale watakaokuwa na mahusiano mema na Khilafah. Hivyo basi wakati ni sasa kwa Afrika kupatiliza fursa na kujiunda na mwito huu ambao muda si mrefu nuru yake itachomoza kwani ishara za alfajiri kuingia zishaonekana.
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afsisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya