Lengo lake ni kurudisha tena mfumo kamili wa Kiislamu na kulingania da’wah ya Kiislamu Ulimwenguni. Lengo hili lamaanisha kuwaregesha Waislamu kuishi maisha kamili ya Kiislamu ndani ya Dar al-Islam na ndani ya mujtama wa Kiislamu ambao kwamba mambo yote ya kimaisha yatasimamiwa kwa mujibu wa hukmu za kisheria, na kipimo ndani yake ni halali na haramu chini ya kivuli cha dola ya Kiislamu, ambayo ni dola ya Khilafah. Dola ambayo Waislamu watateua Khalifah na kumpa ahadi ya utiifu (Bay’ah) kumsikiza na kumtii kwa sharti kuwa ahukumu kuambatana na Kitabu cha Allah (swt) na Sunnah za Mtume wa Allah (saw) na kwa sharti kuwa alinganie Uislamu kama risala ya kiulimwengu kupitia da’wah na Jihad.
Chama hiki, pamoja na hayo, kinalenga kufikia muamko sahihi wa Umma kupitia fikra angavu. Pia kinafanya bidii kuurudisha tena katika nguvu na izza yake ya mwanzoni kiasi ya kuuwezesha kunyakua uwezo wa kiathari kutoka kwa dola nyenginezo na kurudi mahali pake panapo stahili kama dola inayoongoza duniani, kama ulivyokuwa mwanzoni, ulipo utawala ulimwengu kuambatana na hukmu za Kiislamu.
Pia kinalenga kuurudisha uongofu wa Uislamu kwa wanadamu na kuuongoza Umma huu katika mvutano na ukafiri, nidhamu zake na fikra ili Uislamu utawale ulimwengu mzima.