Maandamano Baridi Dhidi ya Kitendo cha Kisafihi cha Raisi wa Amerika Juu ya Kadhia ya Al-Quds (Jerusalem)

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mnamo Ijumaa 15 Disemba, 2017 Hizb ut Tahrir Kenya iliongoza Umma katika miji mbali mbali mikubwa katika maandamano baridi dhidi ya tangazo la hivi majuzi la Raisi wa Amerika Donald J Trump mnamo 6 Disemba 2017. Kuwa Al-Quds (Jerusalem) sasa ndio mji mkuu wa dola ya Kiyahudi na kuamuru Wizara ya Kigeni kuandaa uhamishaji wa ubalozi wa Amerika kutoka mji wa Tel Aviv kwenda Jerusalem, na kuanza kwa kandarasi na wajenzi.

Maandamano haya baridi yalifanywa pindi baada ya swala za Ijumaa katika misikiti tofauti tofauti katika jiji la mwambao wa pwani la Mombasa na Kwale kushutumu vikali kitendo hicho cha kisafihi na hatari cha serikali ya Amerika kilicho dhamiria kuongeza msumari wa moto juu ya vidonda vya mateso ambayo tayari yanausibu Umma kwa kupitia mikono ile ile miovu ya dola ya kirasilimali iliyo na kiu ya umwagaji damu. Katika jiji kuu la Nairobi, kuligawanywa toleo kwa waumini wa Kiislamu katika msikiti wa Jamia. Toleo hilo ambalo asili lilitolewa na Amiri wa kiulimwengu wa Hizb ut Tahrir lilikuwa na anwani:

Tangazo la Trump Huku Watawala Wakikosa Kuchukua Hatua Yoyote Mbele Yake ni Kofi Zito Migongoni Mwao

Amewavua Hata Sitara iliyo Wafinika Uchi Wao!

 Hizb ut Tahrir Kenya ingependa kukariri yafuatayo:

Kwanza, Al-Quds ni Qiblah cha kwanza cha Umma wa Kiislamu kwa hivyo ni katika sehemu ya itikadi ya Kiislamu. Hivyo basi, sio tu ni eneo takatifu bali pia ni alama ya umoja wa Umma wa Kiislamu ulimwenguni; na ndio utakao kuwa mji mkuu wa Khilafah Rashidah kama ilivyo ahidiwa na Mtume (saw). Kwa hivyo, itabakia chini ya himaya ya Umma wa Kiislamu licha ya njama na mipango kutoka kwa Wamagharibi wakiongozwa na dola kuu duniani leo (Amerika) na washirika wake.

Pili, hali hii ya Al-Quds imetokana na tukio chungu la kuvunjwa kwa ngao ya Waislamu Khilafah kwa mikono miovu ya iliyokuwa dola kuu duniani wakati huo (Uingereza) ambayo baada ya kufanikiwa katika kitendo chao hicho kiovu ilisonga mbele na kukaribisha tangazo la Balfour na kutoa fursa ya uundaji serikali ovu zaidi duniani ya ‘Israel’. Hili lilifanikishwa kwa usaidizi wa watawala vibaraka wa kiarabu ambao wamo katika ratiba ya mishahara ya Wamagharibi kutoka hapo na mpaka sasa!

Tatu, Al-Quds inalingania ukombozi wake wa haraka; na hili linaweza kufanywa pekee kupitia kuwaunganisha watoto mukhlisina wa Umma huu wa Kiislamu miongoni mwa majeshi makuu ya Waislamu walio na hamu ya kumridhisha Allah (swt) na ambao wako tayari kufa kwa ajili ya kutafuta daraja ya juu ya Pepo! Watoto hawa si wengine isipokuwa wale wanaomwaga machozi kimya kimya kila mara wanapoona ardhi yao tukufu ikiharibiwa na kuchafuliwa na kijiumbile cha Kiyahudi; huku wakinyamaza wakitaraji kuwa viongozi hawa vibaraka huenda wakaamka karibuni na kuwaamuru kunyanyua hatua zao mbele lakini hili kamwe halikutokea. Watoto hawa mukhlisina sasa wameamua kujitweka majukumu wao wenyewe sio tu katika kuikomboa Al-Quds pekee bali pia kuukwamua Umma kutokana na minyororo ya mfumo batili wa kirasilimali na itikadi yake ya kisekula ambayo ndiyo shina la hali mbaya inayoukumba Umma wa Kiislamu leo. Kwa kupitia kuzing’oa serikali za watawala hawa vibaraka na kusimamisha mahali pao serikali iliyo barikiwa ya Khilafah Rashidah kwa Njia ya Utume.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

KUMB: 03 / 1439 AH

Jumamosi, 28 Rabi’ al-awwal 1439 H

16/12/2017 M

 

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke