بسم الله الرحمن الرحيم
(Imetafsiriwa)
Habari:
Barabara za Kenya zilisalia kuwa uwanja wa vita huku maandamano, yaliyochochewa na ongezeko la ushuru lenye utata, yakibadilika na kuwa kilio kikubwa dhidi ya tofauti za kiuchumi zilizokita mizizi na kukosekana kwa uwajibikaji wa serikali. Mstari wa mbele wa vuguvugu hili ni kizazi cha vijana wa Kenya, wanaokataa kunyamazishwa licha ya kukabiliwa na msako mkali wa polisi. Maandamano hayo yalizuka kujibu mswada wa fedha uliopendekezwa na serikali ambao ulijumuisha ongezeko la kodi huku kukiwa na changamoto ya mazingira ya kiuchumi. Mswada huo ulizua hasira za wananchi, hasa miongoni mwa vijana, ambao waliona kuwa ni hatua ambayo ingeongeza gharama ya maisha inayoendelea katika taifa hili la Afrika Mashariki.
Maoni:
Maandamano ya hivi majuzi nchini Kenya ya Gen-Z na Milenia ni ya aina ambayo tabaka la kisiasa lilikuwa halijayashuhudia hapo awali. Maandamano kwa hakika yalikuwa na masuala ya kweli yaliyodai kwamba yaliweka wazi ushawishi mkubwa wa kikoloni katika nyanja ya uchumi wa kisiasa wa Kenya. Hali hii si ya kipekee kwa Kenya bali katika nchi zote za ulimwengu wa tatu, ambapo sera nyingi za kisiasa, kijamii na kiuchumi zinapitishwa moja kwa moja ili kufaidi ukoloni wa Magharibi.
Mswada mkali wa kifedha ambao ulizua hasira kwa wananchi kwa jumla, idadi ya watu ambao ni karibu 40% chini ya kiwango cha umaskini na zaidi ya 80% ya ajira katika sekta isiyo rasmi na ujira mdogo, wanapaswa kutozwa ushuru mkubwa kutoka kwa gari hadi mkate. Mkono mzito wa mkoloni kutoka taasisi kama IMF, Benki ya Dunia na sera za kigeni zimeweka mtego moja kwa moja na kukandamiza maisha ya jamii katika nchi za ulimwengu wa tatu.
Wito wa mabadiliko hasa miongoni mwa vijana wanaodai uwajibikaji juu ya jinsi nchi ilivyoangukia kwenye dimbwi la mtego wa madeni na kuitaka serikali ya iliyoko kujitenga na utawala wa Magharibi ni sura ya kweli ya dhamira ya mabadiliko. Cha kusikitisha zaidi kwa mapambano haya ya Gen-Z ni yamefungwa ndani ya kitanzi cha fikra, mfumo na miundo ya Magharibi, ambapo kwa hakika mabadiliko ni jitihada kubwa. Kufikiri juu ya mabadiliko ni muhimu kwa maisha kwa sababu kudumaa kwa maisha na kujisalimisha kwa majaaliwa kunatokana na majanga hatari zaidi yanayosababisha watu na mataifa kuangamia, kufa na kusahaulika katika mwendo wa matukio na wakati. Kwa sababu hii, kufikiri juu ya mabadiliko ni miongoni mwa aina muhimu zaidi za fikra na aina hii ya kufikiri haipendelewi na walegevu na haikubaliwi na wavivu kwa sababu gharama ya mabadiliko ni nzito na kwa sababu wale wanaotawaliwa na desturi wanaona kufikiria mabadiliko ni kama kuwakilisha madhara juu yao na kuhama kutoka hali moja hadi nyingine. Kwa ajili hiyo, wale walioporomoka na wavivu wanapigana na fikra za aina hii huku wale wanaoitwa tabaka la kisiasa, wasomi na wale wanaotawala shingo za waja na vyanzo vyao vya riziki wakiipinga na kusimama dhidi yake. Na kwa sababu hii, kufikiri kwa ajili ya mabadiliko kunawakilisha hatari kwa yule aliye nayo na ikawa ndiyo fikra iliyopigwa vita zaidi dhidi yake katika vita visivyokwisha.
Ni jambo la umuhimu mkubwa kwa Gen-Z na vizazi vyote katika wigo wa jamii kuinua hisia hadi kiwango cha fikra ili kuelewa kweli msingi ambao Magharibi inatawala ulimwengu leo. Kwani hii ndiyo njia pekee ya kuhakikisha mwenendo wa hatua kuelekea mabadiliko makubwa. Uislamu kama mfumo pekee unaofaa leo, kwa kuwa unamhutubia Mwanadamu kama mwanadamu pamoja na mahitaji na matakwa yake ya asili. Unashughulikia matatizo ya Mwanadamu kwani yanahusiana naye kama kiumbe chenye maumbile maalum.
Uislamu ulimtazama Mwanadamu kwa mtazamo wa jumla na ulishughulikia mahitaji ya Mwanadamu kama msingi wa suluhisho lake. Wakati ubepari haukumtazama Mwanadamu kwa mtazamo kamili. Ulizingatia vipengele fulani vya mahitaji ya Mwanadamu huku ukipuuza mahitaji yake mengine. Kwa mfano, katika ubepari bidhaa au huduma yoyote inachukuliwa kuwa ya manufaa na inapaswa kuzalishwa mradi tu inakidhi hitaji la mtu binafsi katika jamii, k.m., pombe, dawa za kulevya, ukahaba. Ubepari humwona mtayarishaji au mtoaji wa huduma hizo kuwa ndiye anayechangia katika kutatua tatizo la kiuchumi. Tatizo linatatuliwa kwa kuongeza uzalishaji na hatimaye kuziba pengo kati ya ugavi na mahitaji. Kuongezeka kwa uzalishaji ili kukidhi mahitaji kunapuuza athari za kuzalisha nyenzo na huduma kwa jamii, huku katika Uislamu baadhi ya bidhaa na huduma hazina thamani kwa sababu ya athari zake mbaya kwa jamii. Zaidi ya hayo, chombo ambacho Ubepari unahakikisha upataji wa bidhaa au huduma ni kupitia pesa. Kwa hivyo, asiye na miliki bei ya kitu atanyimwa. Katika Uislamu, ustawi wa mtu binafsi na jamii kwa jumla huzingatiwa na hivyo mtu kupata vitu vinavyohitajika ama kupitia utaratibu wa bei au kwa njia nyinginezo, kama vile Zaka au kupitia hazina ya Serikali.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Omar Albaity
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya