MAGEUZI HUANZA KWA KUKATAA HALI HALISI.MPOROMOKO HUZIDI KWA KUKUBALI YALOWEKWA NA WENGINE

Ulimwenguni kote,kila sehemu ilotokea mageuzi,sawa yawe ni mazuri,kama vile kudhihiri kwa Uislam kama mfumo,ulokuja na mafunzo yenye kukataa kuikubali hali mbaya na duni Duniani,au kuja kwa mifumo baatil kama ukomunisti ulokufa;au ubepari demokrasia,hali zote hizi,mageuzi yalipatikanwa kwa *KUKATAA HALI HALISI ILOKUWEPO*

Kukataa huko,kulianza kifikra.Kwa kuangalia, kuchunguza na hatimae,kupima hali halisi, kwa mtazamo tofauti na ilivyokuwa imezoweleka mbeleni.

Kisha fikra hio,ikajenga hisia ambazo,zilisukuma joto la kukataa hali hio,na badala yake,kutoa maamuzi ya kuleta hali halisi tofauti.Hivyo kukawa ni kwenye kutokea mageuzi.

Uislamu,kama mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu,unasisitiza umuhimu wa kukataa ufuataji hali halisi kipofu (taqlid).

Na kuikubali bila kupinga dhulma na kuamka dhidi ya mfumo fisadi.

Ilikufikia kilele cha mageuzi,kuna hali mbili ambazo lazima kuvaliwa njuga:

1)HALI YA KWANZA

Kujitolea kihali na mali,kupambana na hali halisi.Hata iwe ngumu vipi.Au itatwaa muda mrefu kubadilisha

Kwa sababu tulichofaradhiwa na ALlah ﷻ,ni kujitolea kufanya wala sio kuona matunda.Na tutahesabiwa kwa matendo yetu

Hivyo,tukiangalia Qur’an Tukufu,twaona mifano kadhaa yenye kutubainishia namna ambavyo,hatufai kukubali kunyenyekea hali halisi mbaya yenye maovu:Bali tumetwikwa jukumu la kuibadilisha.Na kuzilinda hali halisi njema:

A.Qur’an yatukemea kufuata mababu kiholela.ALlah ﷻ Atwambia:

*إِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ

“Na wanapoambiwa: ‘Fuata Alichoteremsha ALlah,husema: ‘Bali twafuata tulowakuta nayo baba zetu.’Jee! Hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala hawakuongoka?” Surat Al-Baqarah (2:170)

Hii yamaanisha,kukubali mila,desturi na ada potofu, badala ya haki kutoka kwa ALlah ﷻ

ni kukubali hali halisi (status quo) jambo linalozuia  mageuzi ya haki.

B.Jukumu la kuamrisha mema na kukataza maovu:

*وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ*

“Na kuwe miongoni mwenu na kundi linalolingania khair(Uislam),na kuamrisha mema na kukataza maovu.Hao ndio waliofaulu.” Surat Al-Imran (3:104)

C.Kukataa mifumo yote ya kitwaghuti:

*أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا*

“Jee! Huwaoni wale wanaodai kuwa wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako? Wanataka kuhukumiwa kwa Taaghut (mfumo wa batili),ilhali wameamrishwa kumkufuru!Na Shaitwan anataka kuwapoteza upotevu wa mbali kabisa.” Surat An-Nisā’ (4:60)

Ayah hii Tukufu,yabatubainishia wazi uharamu wa kufuata hukmu,au uongozi kutoka kwa mfumo wa batili (taaghut) badala ya Sharia za ALlahﷻ.

Kando na kuwa,ayah hii ni onyo kali dhidi ya kukubali mamlaka na hukumu zisizo za Kiislamu,bali ni jukumu la Waislam kujitwika dhimma ya kubadilisha hali halisi mbaya, ambayo ni sehemu ya mfumo ulowekwa na vijiungu vyengine,kando na ALlah ﷻ.

2) SEHEMU YA PILI

Ama upande wa pili,wenye kuchangia kutotokea mageuzi na kuibakisha dhulma,unyonge na Ummah kupoteza haiba,ni kuridhika na hali halisi na yale *YALOWEKWA na WENGINE

Msimamo huu, hutokamana na hali mbili mbaya zinapomvamia Muislam:

1)Muislam kuwa na hofu juu ya matwaghuti.

2)Muislam kujishuhulisha mno na Dunia,na kupuuza majukumu ya Dini.

A)Ar Rasulﷺ,alitutahadharisha juu ha hali hizi mbili,pale alipomwambia:

عن ثوبان قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:

*“توشك الأمم أن تداعى عليكم كما تداعى الأكلة إلى قصعتها“.*

فقال قائل: ومن قلّة نحن يومئذ؟

*قال: “بل أنتم يومئذ كثير، ولكنكم غثاء كغثاء السيل، ولينزعنّ الله من صدور عدوكم المهابة منكم، وليقذفنّ الله في قلوبكم الوهْن”.*

فقال قائل: يا رسول الله، وما الوهْن؟

*قال: “حبّ الدنيا وكراهية الموت”.*

Imepokewa na Thawban (رضي الله عنه) alisema:

Ar Rasul ﷺ alisema:

“Yahofiwa kuitana watu dhidi yenu kama walaji wanavyoitana kwenye sahani yao ya chakula.”

Akaulizwa ﷺ:

“Jee!Ni kwa sababu sisi tutakuwa wachache siku hiyo?”

Akasema ﷺ:

“Hapana,bali siku hiyo mutakuwa wengi.Lakini mutakuwa kama povu linalobebwa na mafuriko.

Na hakika ALlah Ataondoa hofu yenu kutoka kwenye vifua vya maadui wenu.

na hakika ALlah Atatupa ndani ya mioyo yenu wahn!

Akaulizwa ﷺ:

 “Ewe Mtume wa ALlah!Nnini wahn?”

Akasema ﷺ:

“Kupenda dunia na kuchukia kifo.”

Muongozo huu kutoka kwa mwana mageuzi mahiri:Ar Rasulﷺ ukowazi kama jua. Kutubainishia kuwa,kuridhika na hali halisi,ndio jambo lenye kututokomeza kwenye lindi la unyonge na udhalilifu!

B)Lazima tujue,kuporomoka kwa Ummah kwatokana si kwa idadi yao kuwa ndogo,au wao kushikamana na Uislam,bali kwa kupoteza dira na kuikubali hali halisi ya mfumo wa kitwaghuti!

Jambo lenye kupelekea Ummah kupoteza utambulisho, msimamo na kushindwa kujitolea bila uwoga kwa haki ya Kiislamu.

Matokeoa yake?Ummah umekuwa kama povu la zimba:idadi yetu kubwa isiyo na nguvu wala mwelekeo.Jamii iliyojaa lakini isiyo na athari.

Haya yote yakiwa ni matunda ya kupenda dunia na kuchukia kifo.Ambayo yachochewa na kuikubali na  kujisalimisha kwa hali halisi ya mfumo wa kitwaghuti.

Kupoteza ari ya kusimama na haki,kukubali hali halisi chafu ilowekwa na wengine,hata kama,hali hio yapelekea kutomuamini kamwe ALlah ﷻ ,ndio mambo yenye kuzuia mageuzi na kuchochea unyonge.

C)Shaitwan atajwa kama chanzo cha upotevu mkubwa kwa wale wanaoridhia hali halisi,ktk mfumo wa baatil licha ya kubainika wazi haki na baatil.

Kwa kuwapambia Dunia mpaka waone kuwa kujitolea kwa Ajili Ya ALlah ﷻ,ni kujiharibia Dunia yao.Na pia ule uchafu na munkar kuwa ndio starehe na ufanisi:

*الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ…

“Shaitwan awa ahidi umaskini,na anakuamrisheni uchafu!” Al-Baqara:268

Enyi Waislam watukufu!

Mulobahatika kutemremshiwa mfumo wenye kulenga kuleta mageuzi kamili ulimwenguni.Mageuzi ktk nyanja zote za maisha,iwe ni kiroho, kijamii,kiuchumi,kielimu,kiutawala na kisiasa,jueni kuwa mageuzi hupatikana kwa kuchukua msimamo dhidi ya  *HALI HALISI* mbaya,hata iwe imezoweleka vipi.

Enyi Waislam watukufu!

Kama kweli tuna azma ya kurudisha izza,haiba na utukufu wetu na WA Dini yetu,basi mageuzi ya kweli ya kimfumo, hukataa mfumo wa batili.Kwa sababu, hakuna mageuzi yoyote ya kimsingi wala mitagaa,yatakayo patikana ndani ya mfumo wa upotevu.

Kando na mabadiliko ya vyama,mirengo na miungano mipya.Yote chini ya hali mbaya ya kwanza!

Ni jukumu la Waislam,kuwaelimisha vijana wa Gen z na wengine,wenye ari ya kutaka kuleta mageuzi,kuwa kumuondoa kiongozi yoyote mamlakani na  kumpachika mwengine,hakuleti mageuzi ya kweli.

Bali shina la matatizo Yako ndani ya mfumo wa kikoloni ubepari demokrasia, wenye kukandamiza watu.

Hivyo,mageuzi ya kweli, huja kwa kutoridhika na kuondoa mfumo huo muovu.

Mahali pake,kueka mfumo mwengine.

Na wala hakuna mfumo wa haki wenye kuleta uadikifu na haki,kando na Uislamu.

Lakini kukumbatia mfumo wa kikoloni ubepari demokrasia,kisha kutarajia mageuzi,ni kujenga ghorofa kwa matofali ya theluji!

Iwapo Ummah, utaendelea kurudia makosa na ya kutobadilisha hali halisi iliopo bila kuirekebisha,basi bila wasi wasi, watakuwa kwenye mwelekeo wa kuporomoka.

Kwa kukubali miundo ya uonevu kama mikataba na maazimio yenye kukandamiza Ummah au kutugawanya,na misimamo ya kigeni,yote yaleta kuanguka kwa Ummah.

HATMA YA WENYE KUPIGANIA MAGEUZI!

Kwa hakika,mvutano baina ya wenye kufaidika na hali halisi mbaya,huwa hawapendi mageuzi,I wala walinganizi wa mageuzi.

Ndio ALlah ﷻ,Atupa mfano ndani ya Qur’an Tukufu,ya namna Farauni na wafuasi wake,walivyokuwa kizuizi cha mageuzi.Lkn hatimae,wanamageuzi huwa niwenye kushinda:

*إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ*

“Hakika Firauni alijitukuza katika nchi, akawagawa watu wake makundi, akiwadhalilisha kundi moja.Na kuwachinja watoto wao wa kiume na kuwawaacha was hana

Hichi ni kiwango cha juu ya kuzuia mageuzi.Lkn ALlah ﷻ Ahitimisha kwa kutwambia:

*وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ*

Na tukataka kuwafadhilisha wale waliodhalilishwa katika ardhi,na kuwafanya viongozi,na kuwafanya warithi.” Surat: (Al-Qasas:4-5)

Na ktk ayah nyingine, ALlah ﷻ Atuhakikishia kupata ushindi na utawala kwa kuikataa hali halisi mbaya na kukubali hali nzuri ya khair!

*ولقد كتبنا في الزبور من بعد الذكر أن الأرض يرثها عبادي الصالحون*

Na kwa hakika tumeandika ktk zaburi baada ya kumbukumbu,kuwa ardhi itarithiwa na waja wangu wema! Al Anbiya aya-105

Na kwengine ALlah ﷻ Atwambia namna Alivyowakabidhi Answar utawala baada ya Maqureish KUKATAA KUBADILI HALI YAO HALISI:

*أُولَٰئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَٰؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا بِهَا بِكَافِرِينَ*

Hao ndio ambao tulowapa kitabu,hukmu na utume.Wakikufuru hao(Maqureish)basi tumewawakilishia watu wasioikufuru

Suratul Al-An’aam:138

Hivyo,kukubali hali halisi,yenye uonevu,dhulma na ukandamizi, kunaangamiza jamii;kuikataa hali hio ni mwanzo wa mageuzi na hatimae ushindi.

Enyi Waislam watukufu!

Ni hatari kuinyamazia dhulma.Tabia hii ndio ilopelekea walotangulia kulaaniwa na kukasirikiwa na ALlah ﷻ:

*لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَى لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ذَلِكَ بِمَا عَصَوْا وَكَانُوا يَعْتَدُونَ ۝ كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَنْ مُنْكَرٍ فَعَلُوهُ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ۝ تَرَى كَثِيرًا مِنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنْفُسُهُمْ أَنْ سَخِطَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ ۝ وَلَوْ كَانُوا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالنَّبِيِّ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مَا اتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَاءَ وَلَكِنَّ كَثِيرًا مِنْهُمْ فَاسِقُونَ*

“Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa Bani Isra’il kwa ulimi wa Dawud na wa ‘Isa mwana wa Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi na walikuwa wakivuka mipaka.”

“Hawakuwakatazana na maovu waliyokuwa wakiyafanya. Bila shaka baya mno yalikuwa hayo waliyokuwa wakiyatenda.”

“Utawaona wengi wao wawawafanya wale waliokufuru kuwa marafiki. Baya mno yaliyoandaliwa na nafsi zao kwa ajili yao kwamba Allah amewakasirikia, na wataadhibiwa milele!”

“Na lau kuwa wao wangemuamini ALlah na Mtume,na yaliyoteremshwa kwake, wasingewafanya (makafiri) kuwa marafiki zao. Lakini wengi wao ni wapotovu.” Al-Maidah:78-81

Na Ar Rasulﷺ,akatusisitiza kwa kutwambia:

عن ابي سعيد الخذري رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:

*ألَا لا يَمنَعَنَّ أحَدَكم رَهْبةُ النَّاسِ أنْ يقولَ بحَقٍّ إذا رَآهُ أو شَهِدَه؛ فإنَّه لا يُقرِّبُ من أجَلٍ، ولا يُباعِدُ من رِزْقٍ؛ أنْ يقولَ بحَقٍّ أو يُذكِّرَ بعَظيمٍ*

رواه الترمذي ،وابن ماجه وأحمد

Imepokewa na Abu Said Al Khudhriy ra.Kuwa Ar Rasulﷺ asema:

Jueni isimzuie mmoja wenu hofu ya watu kuacha kusema haki(kweli)pale anapoiona au kuishuhudia.Kwani kusema haki hakukurubishi KIFO wala kupunguza RIZKI.Basi (Muislam afaa) kusema haki au kukumbusha jambo kuu

Kwa sababu,ukimya na uzembe katika uso wa dhulma na upotofu huleta maangamizi na uharibifu mkubwa.Kama tunavyoshuhudia leo hali ilivyo kwa ndugu zetu Ghaza.Na kuna ktk biladi za Kiislam jeshi lenye nguvu,ambalo laweza kubadilisha hali ile kwa masaa ya kuhesabu.

Ar Rasulﷺ,atwambia:

عن أبي عبد الله طارق بن شهاب البجلي الأحمسي رضي الله عنه أن رجلاً سأل النبي صلى الله عليه وسلم، وقد وضع رجله في الغرز‏:‏ أي الجهاد أفضل‏؟‏ قال‏:‏ “كلمة حق عند سلطان جائر‏”‏

(‏رواه النسائي بإسناد صحيح‏)‏‏

Imepokewa na Abuu AbdiLlahi Twaariq bin Shihaab Al-Bajaliy Al-Ahmasiy ra kwamba mtu mmoja alimuuliza Ar Rasul wakati ambapo alikuwa ameweka mguu wake kwenye korodani (ya mnyama wa kupanda):

“Ni ipi jihadi bora?”

Akajibu :

“Ni kusema neno la haki mbele ya mtawala dhalimu.” Imepokelewa na An-Nasaaiy kwa isnadi sahihi

Ujasiri na ushujaa,ni sifa muhimu kwa Ummah,na thamani yake yawezesha kusema ukweli mbele ya mamlaka dhalimu bila hofu ya kuuliwa au kuteswa!

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي ﷺ أنه قال:

*بدأ الإسلام غريباً وسيعود غريباً كما بدأ فطوبى للغرباء*

رواه مسلم في صحيحه،

“Uislamu ulianza kwa hali ya kigeni, na utarejea ku

wa hali ya kigeni. Basi heri kwa wageni.” (Sahih Muslim)

Enyi Waislam  watukufu!

Mageuzi ya kweli, mara nyingi yahitaji mtu kusimama peke yake dhidi yab wengi.Wala sio kuwaridhisha wengi kwa kumuudhi ALlah ﷻ

Hussein Muhammad

Mwanachama wa Hizb-ut-Tahrir Kenya

Muharram 28 1447 (July 24 2025)