Majanga Halisi Maovu Hata Bila ya Kuwepo Dhoruba za Barafu

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)

Video kutoka ndani ya kambi iliyo sambazwa na wanaharakati katika tovuti za mitandao ya kijamii, zimeonyesha mkimbizi kutoka Syria ndani ya hema lake akitetema kutokana na hali baridi ya anga. Aliziomba mamlaka husika kuwapa mafuta.

Wakimbizi katika kambi za kinyama kadha wa kadha wameyaomba usaidizi mashirika ya misaada na wametoa wito kwa msaada wa dharura kutoka kwa mamlaka husika. Wamesema kuwa ni kiwango kidogo pekee cha msaada ndio kimewafikia wakaazi katika kambi, ambacho hakitoshi kwa asilimia 10 ya idadi jumla ya wakimbizi katika kambi, katika wakati ambapo kuna uhaba mkubwa wa mafuta na njia za kujikanza moto katika hali mbaya za anga kama hizo ambazo zimelikumba eneo zima la Ash-Sham.

Kwa mfano, zaidi ya wakimbizi 80,000 kutoka Syria, katika mji wa Lebanon wa Arsal ambao ni takriban mita 1300 juu ya bahari, wanalalamikia ukosefu wa mambo msingi ya maisha mazuri, kama vile kuhakikisha mitandao sahihi ya majitaka na ujenzi wa njia za wapita njia. Kila mwaka hali mbaya ya anga inakuja na athari ya majanga kwa watoto na wanawake, hata watu wazima na vijana katika kambi hizi zisizo na miundo na hata zile zenye miuondo.

Ni kawaida katika miezi hii ya kila mwaka kuona barafu juu ya milima na mvua kubwa na dhoruba kwa majina yake tofauti tofauti, lakini si kawaida kwa maafa haya na majanga ya kibinadamu kujirudia miaka nenda miaka rudi kutokana na ukosefu wa mahitaji ya kiwango cha chini ya kujiziba baridi kama vile blanketi na mafuta, ikiongezewa na ukosefu wa baadhi ya vyakula msingi kama mkate na maziwa ya unga kwa watoto.

Vile vile ni kawaida kwa maeneo haya kusibiwa na kushuka kwa viwango vya joto wakati wa miezi hii ya mwaka, lakini si kawaida kuona kuwa watoto, hususan wachanga, wakiendelea kusibiwa na hali mbaya sana za baridi.

Yale ambayo si kawaida na yasiyo wezekana hutokea. Tumeyaona, kuyasikia na kuyashuhudia pamoja na watu wetu katika kambi hizi za wakimbizi katika miaka hii yote ya taabu, ambapo majanga halisi yanatokea, hata bila ya kuwepo dhoruba za barafu, ambazo zimeinua pazia ya mwisho ya makhaini hawa, watawala wasiojali, kwa upande mmoja na mashirika yanayodai kufanya kazi kwa ajili ya binadamu kwa upande mwengine.     

Kubuniwa kwa kambi hizo za wakimbizi na hali hizi mbaya za maisha zisizostahiki hata wanyama, Allah awahifadhi kutokana nazo, ndio natija ya kuwapiga mafungu wanadamu kwa msingi wa kanuni ya kuchukiza ya uraia (utaifa) iliyo pelekea ubaguzi huu mkali. Yule aliye na haki ya kuishi maisha mazuri ni yule anayebeba uzalendo, ikiwa unapatikana nchini mwake, huku ikimfunga yule anayedaiwa kuwa mgeni kwa nidhamu na kanuni zinazo weka kikomo uwezekano wa kuishi maisha mazuri na ya ustawi. Na vipi endapo wageni hawa wana sifa ya ziada ya ukimbizi … hususan katika nidhamu kama hizo za kimaslahi za kirasilimali ambazo hazithamini binadamu!!! Wanalazimika kuishi katika sehemu za taabu na zenye hali mbaya zaidi kama vile milima yenye baridi kali na majangwa yenye joto kali na katika mabonde yenye mafuriko. Kana kwamba unyama wa ukosefu wa makao na utafutaji hifadhi hauwatoshi, wanawaongezea unyama wa maisha pasi na utu.     

Waislamu jueni, kwamba hii ndio hali ya wakimbizi: njaa na fedheha katika biladi za Waislamu na wameachwa mkono na wale wanaojisifu kusimamia mambo yao, wanaolala mikononi mwa Wamagharibi na kujadiliana (nao) baada ya kuuza damu ya mashahidi kwa bei rahisi zaidi na mikataba. Tatizo la wakimbizi pamoja na hali zao mbaya na unyama wanaopitia haiko tena kileleni mwa Makala ya vyombo vya habari yaliyo ingizwa siasa kama ilivyo kuwa miaka ya mwanzoni ya mgogoro wa Syria. Faili yao, kama zilivyo faili nyenginezo za kibinadamu zinazo husiana na vita, imetoweka na kubadilishwa kwa upuuzi wa kisiasa na mizozo juu ya maslahi, kana kwamba ziko mnadani, ili kuingiza suluhisho la kisiasa la Kiamerika katika eneo hilo ambalo linaregesha sura ya Mhalifu Bashar kama isiyokuwa na hatia “ndama wa kondoo”!

Na jueni kuwa katika umoja wetu ndio izza na tamkini, na katika mgawanyiko wetu ndio fedheha na unyonge. Basi tufanyieni kazi umoja wetu, na tutafute kuishi kupitia maamrisho ya Uislamu na Dini na turudisheni tena Khilafah Rashida ili tutimize ahadi ya Mola wa Walimwengu.

 (وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً)

“Allah amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na kutenda mema atawafanya Makhalifah katika ardhi kama alivyo wafanya Makhalifah wale waliokuwa kabla yao na atawamakinishia Dini yao ambayo amewaridhia na atawabadilishia baada ya hofu yao usalama.” [An-Nur: 55]

Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

H.  9  Jumada I 1440 Na: 1440 AH / 010
M.  Jumanne, 15 Januari 2019