Makadirio ya Bajeti Kila Mwaka Hayata Waokoa Ummah Kutokana na Majanga ya Kiuchumi wa Kirasilimali

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mnamo Alhamisi, 13 Juni 2019 Waziri wa Fedha Henry Rotich, aliwasilisha makadirio ya Bajeti ya 2019/2020. Makadirio hayo yalifikia trilioni Sh3.02 huku yakiwa na mapungufu ya bilioni Sh607.8. Ilhali tayari tukiwa tumezama katika deni ambalo tayari limegonga trilioni Sh5.6. Serikali yatarajia kukopa zaidi katika mwaka wa kifedha ujao ili kuziba pengo ambalo litakuwa limezidi kwa bilioni Sh45 kuliko mwaka huu wa sasa la bilioni Sh562. Zaidi ya hayo, hazina ya kitaifa inalenga kukusanya mapato jumla trilioni Sh2.115.

Sisi Hizb ut Tahrir /Kenya tungependa kuweka wazi yafuatayo:

Kama zilivyokuwa bajeti za awali, Bajeti ya 2019/2020 bila shaka ndani yake itajumuisha matumizi ya uinuaji mgongo, viwango vilivyozidishwa na matumizi ya kujirudia ambayo yatarajiwa kuporwa mabilioni ya shilingi. Chini ya uchumi wa kirasilimali, kuna msamiati maarufu unaojulikana kama Bajeti ya ziada ikimaanisha kutoa mapendekezo ya bajeti yaliyozidi kuliko makadirio ya miradi. Kupitia mchakato huu wa uandaaji bajeti ndipo ufisadi unatendeka. Serikali na Bunge katika nyanja ya kitaifa na kaunti hujitengea pesa za ummah kiulafi kwao wao, madalali na wafanyibiashara kupitia uchakachuaji wa bajeti.

Lakusikitisha ni kwamba makadirio ya bajeti kila mwaka huleta mahangaiko kwa raia wa kawaida ambao kila kukicha wanakamuliwa kupita maelezo kupitia utozwaji ushuru ili kuweza kugharamia bajeti pamoja na kulipa madeni yaliyoko na ambayo hayana faida yoyote kutokana na mikopo ya riba. Zote hizo zikiishilia katika matumbo ya kikundi cha wanasiasa na wandani wao katika warasilimali. Kamati ya Bunge ya Bajeti imeashiria upungufu wa fedha bilioni Sh607.8 ambazo bilioni Sh324.3 zitakopwa kutoka nje na ilhali bilioni Sh283.5 zitakopwa ndani. Hii ikimaanisha kuwa viwango vya gharaba ya riba vinatarajiwa kuzidi na kuwa asilimia 10 kutokana na kuzidi kwa asilimia 32 katika deni la nje.

Kusomwa kwa bajeti si chochote zaidi ya usanii wa kisiasa unaolenga kuwapumbaza ummah ambao unaendelea kutaabika kutokana na njaa, maradhi na nidhamu ya elimu ya ummah inayosambaratika. Bajeti za kila mwaka hazitotatua majanga ya kiuchumi yaliyokithiri na yanayoathiri watu wengi kwa kuwa serikali inaendelea kujifunga na nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali ambayo kiasili imeletwa na wakoloni.

Tunawalingania wasomi wa nchi hii kuweza kufikiria na kuona kwamba kufeli kwa urasilimali ambao unapigia debe maslahi ya mabepari wachache kuliko ya raia wa kawaida. Tunaamini kwamba suluhisho la kweli lipo katika kuing’oa nidhamu fisadi na badala yake kuweka nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu itakayotekelezwa na Khilafah punde itakaposimama kwa njia ya Utume ndani ya moja ya nchi kubwa za Waislamu. Khilafah haitopoteza muda kwa kujihusisha na michezo ya kirongo ya kisiasa eti ikisoma bajeti kwa kuwa mapato na matumizi yake yamefungwa na wahyi. Haitotoza watu ushuru katika mishahara yao mfano PAYE, VAT n.k bali itakuwa na vyanzo vya mapato ikijumuisha rasilimali asili mfano rasilimali za madini na ngawira n.k ili kukidhi mahitaji ya raia wake pasina na kumdhuru mtu wa kawaida. Kusimama kwake Khilafah itawakomboa wanadamu duniani kutoka katika udhalimu na umasikini usiokwisha kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

KUMB: 1440 / 11

Ijumaa, 11 Shawwal 1440 H /

14/06/2019 M

Simu: +254 707458907

Pepe: mediarep@hizb.or.ke