Habari na Maoni
Habari: Siku ya Jumanne tarehe 18,Agosti,2020 maofisaa wa ngazi za juu wa jeshi la Mali walianza mchakato wa kuipundua serikali ilioko mamlakani kwa kuivamia kambi ya kijeshi ya Soundiata iliopo kwenye mji wa Kati, kulikuweko na makabaliano ya risasi ambapo kabla ya kuchukuliwa kwa silaha kwenye ngome hiyo ya kijeshi na kugawanywa huku maafisa kadhaa wa kijeshi wakikamatwa. Vikosi vya kijeshi viliwatia mbaroni viongozi kadhaa wa serikali akiwemo rais Ibrahim Boubacar Keita (mwenye umri 75) ambaye baadaye alijiuzulu na kuivunja serikali yake. Mapinduzi haya yanakuja wiki chache za maandamano dhidi ya uchaguzi tata uliofanyika, hali ya ufisadi serekalini na utovu wa usalama uliodumu kwa miaka minane sasa.
Maoni:
Mapinduzi haya ya kijeshi ni ya pili katika kipindi kisichopungua mwongo mmoja, kufuatia yale ya mwaka 2012 ambapo serikali ya Amodou Toumani Tour’e kubanduliwa madarakani na wanajeshi waliounda kamati ijulikanayo;National Committee for the Restoration of Democracy and State. Tarehe 21 Agosti,Marekani ikakata msaada wa Kijeshi kwa nchi ya Mali kama hatua yake ya kujibu mapinduzi haya. Licha ya kupingwa vikali na jamii ya Kimataifa, mapinduzi haya yamepokelewa kwa shangwe na raia wa Mali katika mji mkuu wa Bamako.Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imekashifu vikali mapinduzi haya na ikachukua uamuzi wa kusitisha uanachamana wa Mali kwenye jumuiya hiyo.Jumuiya hiyo ya kanda ya Afrika Magharibi ikasema kwamba mataifa ya Afrika Magharibi yanayopakana na Mali yanafunga mipaka yake na endapo mzozo huu ni wenye kuendelea basi wataiwekea vikwazo. Katika ngazi ya kimataifa, raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron amekashifu mapinduzi haya na kutoa mwito wa utawala kuregeshewa raia na viongozi waliokamatwa wachiliwe huru. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari tarehe 19,Agosti 2020 ya kupinga vikali mapinduzi hayo ya Mali. Marekani inatoa mwito wanasiasa wote pamoja na wakuu wa kijeshi kufanya kazi ya kuregeshwa tena kwa serikali ya kikatiba. Tunawaomba washikadau wote nchini Mali kufanya mazungumzo ya Amani yatakayoheshimu haki za raia wa Mali ikiwemo uhuru wa kuzungumza,kukongamana kwa Amani na kukataa fujo’. Ikasema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa kuwa mapinduzi yaliyotokea miaka minane iliyopita yaliungwa mkono na Marekani, kuna uwezakano kusema kwamba mapinduzi ya mara hii pia yamepata Baraka za Marekani. Hivyo kule kayakashifu kwake ni urongo. Hii ni ikizingatiwa kwamba kiongozi wa mapinduzi haya, Kanali Assimi Goita ameripotiwa kuwa alipewa mafunzo ya Kijeshi na Marekani na kufanya kazi na kwenye kikosi cha maalumu cha oparesheni ya kupambana na wapiganaji wa Kiislamu huko Afrika magharibi kwa miaka kadhaa. Mapinduzi ya 2012 yalifanywa na maofisaa wa ngazi za chini hivyo kukaibua mgongano kati yao na wale viongozi wa kuu wa kijeshi hali hii ikasababisha kuzorota kwa usalama nchini Mali na kupelekea jimbo la Kaskazini mwa Mali kuchukuliwa na Jamii ya Tuaregs na baadhi ya makundi ya Kiislamu ya eneo hilo, hii ni kumaanisha Ufaransa ilifaulu katika kuidhibiti siasa ya Mali pale ilipoweza kumleta madarakani kibaraka huyu alieong’olewa mamlakani Ibrahim Aboubacar Keita. Hii ndio maana i Ufaransa na wenzake wa Ulaya wakishirikisha jumuiya za kikanda kama hii jumuiya ya ECOWAS wakaonekanwa wakikashifu mapinduzi hayo. Ni wazi kwamba Amerika inavutana na Ufaransa katika kujaribu angaa naye apate mtu wake atakayeweza kubadilisha hali ya sasa ya mambo ya Mali ambayo inayomilikiwa na Ufaransa.
Hivi ndivyo jinsi gani nchi ya Kiislamu ya Mali inavyojipata ikiwa katikati ya mvutano kati ya mkoloni wa zamani wa Kiulaya Ufaransa,na mkoloni mpya Marekani. Isitoshe kuanzia mwaka 2013, muungano wa Ulaya (EU) umekua ukilipa jeshi la Mali mafunzo ya kijeshi, aidha katika eneo Sahel kunahudumu kikosi cha ha kupambana na ugaidi cha Ufaransa katika ‘Operation Barkhane, kikosi hiki kinasaidiwa helikopta za Uingereza, na mataifa mengine ya Ulaya pia na ndege zisizo na rubani za Marekani. Muungano wa kijeshi wa umoja wa mataifa unaohudumu nchini Mali unaojulikana MINUSMA (United Nations Multidimensional Intergrated Stabilization Mission ) ulioanzishwa na baraza la usalama azimio nambari 2100 la mwezi Aprili 2013, ni muungano uliobuniwa kama njia ya kuingilia masuala ya ndani ya kisiasa ya Mali huku kwa kisingizio cha ‘kulinda usalama’ ukisukuma ajenda za kisiasa za Kikoloni kwa taifa la Mali. Ni muhimu kubaini kwamba mataifa ya Ufaransa na Marekani kwa kusaka maslahi yao kikoloni yamekuwa yakiingilia masuala ya ndani ya mataifa mengi ya bara la Afrika.
Licha ya nchi ya Mali kuwa na utajiri ukiwemo dhahabu, Phosphates, bauxite, chuma, madini yay a urani na mengine,bado utajiri huu haufaidhisha raia. Kiwanda cha uchimbaji wa madini haya hasa ule wa uchimbaji wa dhahabu ambao kwa Afrika ni wa tatu kwa ukubwa. Ufaransa inalinda maslahi yake huku Mali. Kampuni yake ya kawi Avera imekua ikiiba mafuta kwa miongo kadhaa katika nchi jirani ya Niger. Mradi huu muovu unafanikishwa chini ya kibandiko cha vita dhidi ya ngome za ugaidi nchini Mali vinavyopata ridhaa na serikali ya Bamako na ile ya Umoja wa mataifa!
Taifa la Mali ambalo zaidi ya asilimia 90 ya raia wake ni Waislamu imekua ikigeuzwa kutoka janga moja hadi janga jengine hali inayolifanya liwe siku zote liko katika hali ya taharuki. Taifa hili linakumbwa na matatizo ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi pamoja na ya kijamii yote haya yakitokamana na taasisi duni za kiutawala, serikali mbovu, mtafaruku wa kijamii na kubaguliwa kwa jamii zinazoishi kaskazini mwa nchi ambao serikali kuu imekuwa ikizitelekeza. Kuingilia katika kwa mataifa ya kimagharibi na mikakati yao ndiyo hutumbukiza nchi hii kwa majanga mengine zaidi. Hali hii ni yenye kutarajiwa kutokea kwani makafiri wakoloni ndio waliopewa nafasi ya kusimamia mambo ya Waislamu.Majadiliano na mazungumzo yanaendeshwa na jumuiya za kikanda; ECOWAS au za kimataifa kwa mfano OIF Muungano ya nchi zilizokoloniwa na Ufaransa na EU yote haya hayatotatua matatizo ya nchi ya Mali hasa ikizingatiwa taasisi zote hizi ni za kikoloni zenye kulenga kulinda maslahi ya wakoloni. Kwa hakika inakera mno kuona nchi ya Kiislamu inakua ikilengwa na wapipiaji mali mabepari hii ni kwamba Waislamu hawatawaliwi na Uislamu badali yake wanatawaliwa na mfumo wa Kirasilimali uliojaa tamaa zote.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na,
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa vyombo vya Habari Hizb ut-Tahrir Kenya
27/8/2020.