Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mnamo 1 Agosti, marufuku ya Niqab yalianza rasmi ndani ya Uholanzi, yakiwazuia wanawake Waislamu kutovaa kizuizi nyusoni mwao wanapokuwa katika taasisi za umma, ikijumuisha shule, hospitali na afisi za serikali pamoja na mabasi na treni. Mamlaka zinatakiwa kuwalazimisha wanawake waliovaa Niqab kuzivua wanapotaka kuingia katika jengo la umma. Lau watakataa hawatoruhusiwa kuingia napia wanaweza kupigwa faini ya takribani Uro 150. Kupitia kitendo hicho cha wazi cha kiubaguzi, serikali ya Uholanzi imejiunga na kikundi maalum cha mataifa ya kihuria yanayojumuisha Ufaransa, Denmark, Ubelgiji na Austria ambayo yamepitisha sheria ya ubaguzi dhidi ya wanawake Waislamu na kuwafanya kuwa ni wahalifu kwa kuwa tu wamevaa kwa mujibu wa imani ya dini zao. Inazidisha ubaguaji na uonevu wa wanawake Waislamu kwa kuchochea hasira na chuki za wanaouchukia na kuogopa Uislamu na kupelekea kuwapa kibali cha kuwatendea vitendo vya kuwahangaisha, kuwahofisha na vurugu. Kufuatia marufuku hayo, gazeti la Uholanzi la Algemeen Dagbland liliandika kwamba wale walio ‘sumbuliwa’ na mwanamke Muislamu kwa kuvaa mavazi yaliyozuiwa wanaweza kumtia korokoroni kama raia napia wanaweza kumlazimisha avue niqab na hata kutumia nguvu lau ‘mwenye kuvaa’ hivyo atajaribu kukataa. Kwa kuongezea, ni nidhamu gani isiyokuwa na ubinadamu inayomlazimisha mwanamke kuchagua baina ya kujifunga na imani ya dini yake na kutafuta matibabu, elimu, ajira na hata kuripoti uhalifu dhidi yake katika kituo cha polisi? Inabeba alama ya tawala za kidikteta na kikomunisti.
Uholanzi ni dola ambayo inatambulikana kwa ‘uhuru’ wake na ulegevu katika mtazamo wake katika uchaguzi wa mwenendo na imehalalisha vitendo vichafu na fisadi zaidi ikijumuisha ukahaba, mahusiano baina ya wanachama wa familia, uvutaji wa bangi katika maduka ya kunywa kahawa na hata kumiliki na kusambaza ‘Muongozo wa Kunajisi watoto’–kitabu kiovu kinachoelezea kwa kina namna ya kuwavuta, kuwa karibu na kuwanajisi watoto. Na bado, serikali inachagua kuharamisha mavazi ya kidini yasiyokuwa na madhara. Ni nidhamu aina gani inayoruhusu vitendo viovu ilhali inaharamisha muonekano wa stara? Inathibitisha kwa mara nyingine kwamba ubaguzi wa dini umekita mizizi katika nidhamu ya kisekula ya kihuria na hivyo Waislamu hawatakiwi kuwa na imani nayo katika kulinda haki za dini yao kwa kuwa daima inawakilisha wale ambao wanafuata mchoro wa kisekula wa kihuria. Kwa mfano, Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu, mahakama kuu ndani ya Ulaya ambayo imetwikwa jukumu la kulinda haki za raia wake ikatoa hukumu inayounga mkono Ufaransa na Ubelgiji kupiga marufuku ya Niqab, ikikataa hoja za kwamba imekwenda kinyume na uhuru wa dini na kusema kwamba hawakwenda kinyume na Mkataba wa Ulaya Juu ya Haki za Binadamu! Kwa kuongezea, marufuku ya kizuizi cha uso ndani ya Uholanzi yalipendekezwa mnamo 2005 na mwanasiasa wa mrengo wa mkono wa mbali wa kulia na anayepinga Uislamu, Geert Wilders. Hivyo basi, badala ya madai ya urongo kwamba Niqab inaweka kizuizi katika mawasiliano au ni tishio la kiusalama, marufuku hii kiuwazi ni jaribio la serikali ya muungano ya Mark Rutte kujaribu kupatiliza fursa dhidi ya mrengo wa vyama vya mbali vinavyopigia debe ubaguzi kwani vilikuwa vinaongeza kupata umaarufu katika uchaguzi wa Uholanzi. Mashindano hayo ya kisiasa ambapo vyama vinashindania nani atakayekuwa yuko juu katika kuupinga Uislamu na Waislamu ndio uhalisia uliopo ndani ya dola nyingi za kisekula na zinaashiria hatari iliyoko ndani ya nidhamu ya kisekula ya kidemokrasia ambapo wachache hawapati nafasi ya ushindani sawa katika kugombania uongozi.
Kama Waislamu ni muhimu kufahamu kwamba, sio Niqab inayolengwa na serikali ya Uholanzi au serikali nyingine huko Magharibi ambao wameiharamisha. Bali ni msimamo wa Uislamu ndani ya dola za kisekula za kihuria ndio unaoshambuliwa na ima imani yake inaweza ‘kuvumiliwa’ ndani ya mujtama zao. Leo ni Niqab, kesho inaweza kuwa ni Khimar (kitambaa cha kichwa) kama ulivyo mwito wa hivi karibuni wa Geert Wilders na mfano wake, au kitendo cha Kiislamu au imani yake ambacho hakiendani na mpangilio wa kihuria. Ajenda ni kutuingiza kupitia kututisha na kutulazimisha kuibeba thaqafa ya kihuria. Kama Waislamu, hivyo basi tunatakiwa kusimama thabiti kwa kukatikiwa na kuungana katika kupaza sauti zetu kwa kupinga vikali marufuku haya na mengine juu ya imani ya Uislamu na kupambana na urongo dhidi ya Dini yetu! Mwenyezi Mungu (swt) asema,
﴾إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿
“Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu; kisha wakatengenea, hawatakuwa na khofu, wala hawatahuzunika.” [Al-Ahqaf:13]
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 9 Dhu al-Hijjah 1440 | Na: 1440 H / 041 |
M. Jumamosi, 10 Agosti 2019 |