Mauaji ya Polisi: Hulka ya Kibepari ya Ukatili na Kutokujali

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Maafisa watatu wa polisi nchini Kenya wameshtakiwa kwa mauaji ya mwanablogu mwenye umri wa miaka 31 aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi mapema mwezi huu. Kifo cha Albert Ojwang kimezua hasira nchini Kenya huku maandamano yakifanyika kudai haki.

Sisi katika Hizb ut Tahrir Kenya, tungependa kuangazia yafuatayo

Chini ya tawala za Kisekula za Kiliberali kama vile Kenya maofisaa wa usalama ni muendelezo wa uundaji wa enzi ya ukoloni ambapo  Waingereza walitumia kudhibiti idadi ya watu na kukomesha upinzani. Katika miaka ya 1950, Wakenya walipoanza kudai haki yao ya kujitawala, polisi na vyombo vingine vya usalama vilivyosimamiwa na Uingereza vilikusanya makumi ya maelfu ya Wakenya na kuwanyonga zaidi ya elfu moja. Inavyoonekana, jeshi la polisi linawaona raia wa kawaida kama tishio linalowezekana kwa utawala unaotawala njia ambayo ilianzishwa hapo awali ili kutekeleza utawala wa kikoloni-sio kulinda raia.

Kiaidiolojia, tawala za Kisekular za  kiliberali huona manufaa na maslahi kuwa kipimo kikuu kipaswacho kutukuzwa zaidi hata kuliko maisha ya binadamu na mali, Kwa vipimo hivi ndio hufanya ufisadi, kutokujali na kutekwa mamlaka ya dola na genge la watu fulani ada ya kisiasa. Kwa kuzingatia hili, mauaji ya vyombo vya dola bila kuadhibiwa ndiyo njia pekee ya kuzuia sauti yoyote ya upinzani na juhudi za kufichua ufisadi mkubwa. Ni muhimu kubaini kwamba  ukatili na utesaji unaofanywa na vyombo vya dola ni mtindo na tatizo la kiulimwengu wala haliko tuu kwa Kenya.

Tunasisitiza kwamba maisha ya binadamu au tuseme maisha yote ni matakatifu na hustahili kulindwa kabisa na serikali bila woga au upendeleo. Katika Uislamu, ulinzi wa maisha ya mwanadamu ni muhimu na unachukuliwa kuwa amana kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Uislamu unasisitiza utakatifu wa maisha, hivyo umeharamisha kuuwa huku ukitaka ulinzi wa maisha na heshima kwa wanadamu wote.

Tunasisitiza kwamba ni chini ya Khilafah Raashida tu (Ukhalifa ulioongoka) ambao utasimamishwa hivii karibuni juu ya mfumo wa wa Utume, jeshi la polisi litakuwa na jukumu la kudumisha utulivu wa umma, kutekeleza sheria, na kuchunguza uhalifu. Mateso ni marufuku kabisa na afisa polisi yeyote atakayepatikana na hatia ya kutekeleza unyanyasaji wa kimwili au mateso dhidi ya raia yeyote, Mwislamu au asiye Muislamu, atawajibishwa. Kwa hivyo, vikosi vya polisi vitajitolea kikamilifu kudumisha sheria na utulivu na kulinda maisha na mali za raia.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut Tahrir

Kenya