Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
Polisi nchini Kenya wanaendelea na ufukuaji wa makaburi membamba kuitoa miili ya watu wanaoaminika kufa njaa katika eneo la pwani ya nchi. Idadi ya vifo hadi sasa imefikia 89 huku miili zaidi ikitarajiwa kutolewa. Pasta Paul Mackenzie – mhubiri matata wa kanisa linalojulikana Good News International lililoko katika la eneo la ekari 325 karibu na Mji wa Malindi, akiwataka wafuasi wake kukaa njaa kwa siku kadhaa wakiamini kufanya hivyo ni kuyapa mgongo maisha ya kidunia na ndio njiya ya kwenda kukutana na Yesu.
Hizb ut Tahrir Kenya imeshtushwa na kitendo hiki cha kikatili na ingependa kuangazia yafuatayo:
Mauaji haya ya halaiki sio ya kwanza kufanyika kwa ulimwengu wa kikikristo kwani katika historia yake kumesheheni visa kama hivi. Mwaka 2000, kulishuhudiwa mauaji ya Kanungu pale pasta mmoja wa Uganda kwa jina la Joseph Kibwetere alihusika na mauaji ya zaidi wakristo 900. Na mwaka wa 1978 kukashuhudiwa mauaji ya Jonestown huko Guyana ambapo kasisi Jim Jones aliwadanganya wafuasi wake waweze kujidunga sindano zenye sumu na mauaji mengi ya kutisha yaliyoegemea misimamo mibaya iliotokamana na itikadi za kihamasa na maigizo pasina na kukinaisha akili ya mwanadamu.
Kiasili mfumo wa kirasilimali umemkosesha mwanadamu matumaini ambayo huchukua nafasi kubwa sana katika kumuongoza maishani, nayo hali hii kwa urahisi ikapatilizwa na makasisi ambao wengi wao huwadaa wafuasi wao wajitoe uhai kwa madai ya kuupata uzima wa milele kwani tayari wamekwisha kata tamaa maishani. Mfumo huu wa kirasilimali umeshindwa vibaya katika kusimamia mahusiano ya kijamii na kupelekea utepetevu wa vyombo vya usalama, hali ngumu ya kiuchumi, hulka mbovu za kijamii na utawala fisadi wa Kidemokrasia hivyo kukatisha kabisa matumaini kwa jamii.
Kwa kuwa suala la imani lina unyeti mkubwa katika maisha ya mwanadamu, kwani ndio huunda mienendo yake kama mtu binafsi na kama sehemu ya jamii.Ni itikadi ndio inayompa mwanadamu fikra na fahamu zinazomfanya apate kuamka na kuendelea. Tunasema kwamba Uislamu ndio mfumo pekee ulio na itikadi yenye kuafikiana na maumbile ya mwanadamu na kumdhaminia utulivu, usalama, raha na matumaini hapa duniani na maisha ya Akhera. Katika mojawapo ya malengo ya Uislamu ni kulinda uhai na mali hivyo kitendo chochote kile kinachopelekea kuondosha uhai wa mtu au mali kimekatazwa na kukashifiwa vikali na MwenyeziMungu pale aliposema:
(وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ)
Wala msijitie kwa mikono yenu kwa maangamizo
[TMQ 2:195]
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut Tahrir Kenya