Mikataba Batil na Fasid katika Ndoa

Ufupisho wa Suali na Jawabu – 10

Suali

Ni nini tofauti kati ya masharti ya kuswihi na masharti ya kufunga ndoa? Je yana athari gani katika mkataba huo, ni wakati gani yanaifanya ndoa kuwa Batil na ni wakati gani yanaifanya ndoa kuwa fasid?

Jibu

  1. Tumeelezea haya na kufafanua kwa kina kwenye kitabu cha Nidhamu ya Kijamii katika Uislamu kuwa …Ndoa ina fungwa kupitia ijabu na kabuli sahihi. Ijabu ni yale maneno yanayotamkwa mwanzo na mmoja wa wanaofunga mkataba huo. Na kabuli ni yale maneno yanayotamkwa baada ya ijabu na yule mwengine kati ya wanaofunga mkataba huo.

Kufungwa kwa Mkataba wa ndoa, unalazimu masharti manne (4):

Kwanza: Kupatikane Ijabu (ombi) na Kabuli (kukubali) katika mkao mmoja. Yani mkao ambao Ijabu ilitolewa uwe ndio mkao ambao Kabuli ilipatikana. Hii ni ikiwa wote kati ya wanandoa wako sehemu moja. Lau wanaofunga ndoa hawako sehemu moja mfano wako nchi mbili tofauti na mmoja kati yao akumuandikia mwenzake barua ya Ijabu (ombi la ndoa) na mpokeaji wa barua hiyo akakubali basi utakuwa mkataba wa ndoa umefungwa. Lakini katika hali hiyo ni sharti aisome barua hiyo au ampe mtu aisome mbele ya mashahidi wawili ambao wameitwa kusikia yaliyomo ndani ya barua hiyo. Au anaweza kuwaambia, mtu fulani wa fulani amenitumia barua akitaka anioe na nimewaita katika mkao huu huu kuja kushuhudia kuwa nimekubali kuolewa na yeye.

Pili: Wanaoingia katika mkataba wa ndoa lazima kila mmoja wao aisikie kauli ya mwenziwe na amuelewe kuwa anataka mkataba wa ndoa. Lau hatojua ima kwa kuwa hakumsikia au hakuelewa, ndoa hiyo haitokuwa imefungwa.

Tatu: Kabuli isipinge sehemu ya Ijabu au Ijabu yote. Yani anayekubali asikatae ombi, ima ombi lote au sehemu ya ombi.

Nne: Shari’ah iwe imeruhusu mmoja kati ya wana ndoa kumuoa mwengine. Yani ndoa iwe kati ya mwanamke muislamu au mwanamke kutoka kwa Watu wa Kitabu na mwanamume muislamu.

Ikiwa mkataba wa ndoa umetimiza masharti haya manne (4) basi utakuwa umefungwa. Lau moja katika masharti hayo hayakutimia basi kutakuwa hakuna mkataba wa ndoa, itakuwa ni batil kuanzia msingi wake.

Baada ya kufungwa mkataba wa ndoa, ni lazima mkataba wa ndoa uwe sahihi kwa kutimiza masharti ya usahihi ya mkataba wa ndoa ambayo ni yafuatayo:

Kwanza: Mwanamke awe anastahili mkataba wa ndoa. Mfano isiwe ni kuwaoa madada wawili kwa wakati mmoja.

Pili: Ndoa hiyo haitakuwa sahihi bila msimamizi (wali) maanake mwanamke hana haki ya kujiozesha au kuwaozesha wengine. Napia hawezi kumpendekeza mwengine yeyote mbali na msimamizi wake, lau atafanya hivyo ndoa itakuwa haiko sahihi.

Tatu: Kuwepo na mashahidi wawili waislamu wenye akili timamu, walio baleghe watakaosikia kauli za wanaofunga mkataba wa ndoa na kuelewa lengo la ombi na kukubaliwa kwa ombi ni mkataba wa ndoa.

Ikiwa mkataba wa ndoa umetimiza masharti haya matatu (3) basi utakuwa sahihi. Lau moja katika masharti hayo hayakutimia basi utakuwa ni fasid.

Hivyo basi ikiwa masharti ya kufunga mkataba wa ndoa hayakutumia, mkataba huo unakuwa batil. Na ikiwa masharti ya kuswihi mkataba wa ndoa hayakutimia basi mkataba huo unakuwa fasid.

  1. Tofauti kati ya Fasid na Batil. Batil ni chochote ambacho kinakwenda kinyume na Shari’ah katika msingi wake. Yani kimekatazwa au kile ambacho kinapokosekana katika mkataba kama sharti basi kukosekana kwake kuna kosesha kitendo chenyewe, mfano ndoa kwa mujibu wa suali hili. Fasid ni chochote kinachokubaliana na Shari’ah ki msingi lakini sifa yake inagongana na Shari’ah.

Katika ndoa, Mikataba Batil na Fasid ni kinyume na Shari’ah, lakini Mkataba Batil una vunjwa kuanzia mwanzo wake. Lau itakuwa watu wameingiliana, itachukuliwa hukm ya zina (kufanya kitendo nje ya ndoa), na mtoto hatohusishwa na mwanamume aliyefanya zina; hakutakuwa na Idda wala mahari wala kuharamishwa kwa wanawake katika ndoa maanake Asili ni Batil.

Ama Mkataba Fasid, uko kinyume na Shari’ah katika masharti ya usahihi na sio masharti ya kufungwa mkataba.

Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye Hekima.

Link ya Kiengereza: http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/jurisprudence-questions/14810.html

Chanzo: Hizb ut Tahrir Kenya

24 Shaaban 1439 Hijria

10 Mei 2018 Miladi