Mpango wa Sykes-Picot wa kugawanya nchi unatumbukiza Afrika kwenye Ghasia na Machafuko Zaidi  

 

Habari na Maoni 

Habari:Kufikia Machi 30, 2025, Sudan Kusini inakabiliwa na mvutano wa kisiasa na ghasia zinazoongezeka, zinazotishia amani tete iliyoanzishwa kwenye makubaliano ya 2018. Kukamatwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar mwishoni mwa mwezi Machi kumezidisha hofu ya kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kuzuiliwa kwa Machar, pamoja na washirika wake, kumepelekea chama chake kutangaza kuvunjika kwa makubaliano ya amani, kutokana na kukosekana kwa utashi na nia nzuri ya  kisiasa kuelekea amani na utulivu.

Maoni

Inafahamika vyema kuwa Marekani ilisukuma ajenda ya utekelezwaji wa kutenganisha Sudan Kusini na kuanzishwa kwa dola ndani yake. Marekani iliunda vuguvugu la kujitenga lililoitwa Sudan People’s Liberation Movement mwaka 1983, likiongozwa na wakala wake, John Garang, kufanya kazi ya kuwadhibiti waasi wote na harakati zao katika harakati moja. Zaidi ya hayo ni kweli Marekani ndiyo iliyomleta Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir madarakani mwaka 1989, na kumtaka awekeze ushawishi wake nchini humo, na kisha kutekeleza wazo la kutenganisha Kusini.

Izingatiwe kuwa Sudan Kaskazini na Kusini iligeuzwa kuwa ni eneo la ushawishi wa Marekani na Ulaya hasa Uingereza kwa sababu ya ushawishi wake katika Sudan ya zamani na mawakala wao huko, imeendelea kujaribu kuingilia kati kila inapowezekana, ili kurejesha ushawishi wake nchini Sudan, au angalau kushirikiana na Amerika, hata ushawishi mdogo huko.

Kwa muktadha huu, ushindani kati ya vibaraka wa nchi za magharibi yaani Rais Salva Kiir (a Dinka) na Makamu wa Rais wa zamani Riek Machar (a Nuer) umesababisha Sudan kusini katika machafuko. Nchi  hii imegawanyika sana kwa misingi ya kikabila, hasa kati ya jamii za Dinka na Nuer. Jeshi la Wazungu la Nuer (wanamgambo wa kikabila) hivi karibuni walishambulia vikosi vya serikali huko Nasir, na kusababisha kuhama kwa watu wengi. Maazimio yote yaliyofikiwa kati ya wapinzani wawili kama vile Makubaliano ya Amani ya Addis Ababa yamekiukwa, jambo ambalo limeifanya nchi kuwa na machafuko zaidi. Ushindani huu kati ya Kier na Machar unatokana na mvutano wa kimaslahi kati ya mataifa ya kigeni ambao ni wahusika wakuu wenye maslahi nchini Sudan Kusini. Nia yao ni kupora rasilimali pamoja na mafuta.

Fikra jumla ya kugawanya nchi ni mipango ya makafiri wa kikoloni ili kusambaratisha biladi zetu. Afrika ambayo ni makao ya vuguvugu kadhaa za wanaotaka kujitenga lazima itambue kwamba kupitia kujitenga itajimaliza yenyewe kwa kujisoza kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Sudan Kusini inapaswa kutoa ushahidi wazi wa hatari ya njama hii ya wakoloni. Wakoloni sasa wamejiingiza katika mpango mpya wa kutenganisha Darfur. Wasomi wa Kiafrika na Ummah kwa ujumla wanapaswa kusimama kidete dhidi ya njama za madola ya kikoloni ya Magharibi, hususan Marekani, na kuwazuia wale wanasiasa ambao wamejitia kwenye nira ya mabepari na wanatekeleza njama zao dhidi ya ardhi yetu.

Ni kupitia Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume ndio utakaoziunganisha ardhi zetu na kuziondolea ardhi zetu wakala au kibaraka yeyote aliyeshughulika na ardhi zetu. Kuleta hesabu kwa yeyote aliyeuza ardhi zetu kwa faida ya kidunia. Ni Khilafah pekee inayoweza kutuunganisha dhidi ya adui na ndipo tunaweza kutazama kuanguka kwao.

 

Imeandikwa kwa Niaba ya Ofisi kuu ya Habari ya Hizb ut- Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa vyombo vya habari Hizb ut-Tahrir Kenya.