Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mnamo Jumanne, Machi 6, wanawake kutoka nchi 55 walitoka katika “msafara wenye utu” kuanzia Istanbul mpaka Hatay. Lengo lao likiwa ni kunyanyua rai jumla juu ya wanawake 6,736 wakiwemo wasichana 417 wanaoteseka katika magereza ya serikali ya Assad, wakisubiri kifo chini ya mateso na ubakaji wa kila siku. Magereza hayo yamejaa wanawake wazee, waja wazito na wanawake waliojifungua punde tu kabla ya vifungo vyao. Inajulikana kuwa wanawake wanaopitia uchungu wa ubakaji na mateso aghalabu hujiua wanapo pata fursa ya kufanya hivyo. Idadi ya watoto wanaozaliwa na kufa magerezani humo pasina na kuuona mwanga wa jua haihisabiki tena… Kwa mujibu wa Gülden Sönmez, naibu mwenyekiti wa Vuguvugu la Haki za Kibinadamu na Uadilifu (İHAK), na mmoja wa waandalizi wa “Msafara Wenye Utu”, serikali ya Syria, “inatumia ubakaji waziwazi kama silaha” katika vita hivi. Alisema, “Wanawake waathiriwa wa vitendo hivi viovu hawasikiki na nchi yoyote, shirika lolote la kimataifa wala jamii yoyote ya kimataifa kamwe. Kando na hayo, wanasibiwa na uhalifu dhidi ya kanuni ya kimataifa, uhalifu dhidi ya ubinadamu. Ni miaka saba sasa [tangu kuanza kwa vita hivi] na bado tungali tunasubiri mtu kuchukua hatua kuhusiana na hili”.
Kwa sisi Waislamu, utukufu wa mwanamke na kuhifadhiwa heshima yake – ima Muislamu au asiyekuwa Muislamu – ni agizo la Imani yetu. Hivyo basi serikali ya Assad inauchukulia ubakaji huu wa kiidara na mateso kwa wanawake Waislamu kama mbinu ya kuwaadhibu na kuvunja azma ya Waislamu na kuwalazimisha kuachana na mapinduzi yao ya Kiislamu. Rekodi rasmi zaeleza kuwa wanawake 13,581 wamo ndani ya magereza ya Assad tangu siku ya kwanza ya mapinduzi ya Kiislamu mnamo 2011, wengi wao wakiwa wamebakwa… zaidi ya hayo, imethibitishwa kwa dalili kuwa zaidi ya watu 65,000 wamepoteza maisha yao chini ya mateso yasiyo elezeka, dhulma za kimapenzi na kunyimwa chakula katika magereza ya serikali ya Assad. Kwa mujibu wa İHAK, zaidi ya watu 76,000, wakiwemo watoto 116 na wanawake 4,219 kwa ufupi “WAMEPOTEA”, habari zao hazijulikani. Na katika kipindi cha uchinjaji katili wa zaidi ya watu milioni 1, tulishuhudia kuwa wale wanaozungumzia kuhusu mistari miekundu ni vipofu wa rangi. Wakimbizi milioni 7 wa Syria, idadi sawa na wasio na makao ndani ya Syria, na takriban milioni 14 ya wanaohitajia misaada ya dharura wanaangamia kidogo kidogo kutokana na njaa na ukosefu wa madawa. Zaidi ya watoto 10,000 wasio andamana na jamaa zao wanaoufaulu kufika Ulaya wametoweka mikononi mwa walanguzi wa binadamu, ngono na viungo vya mwili.
Dola zote kuu za kikoloni zimeungana mikono kumlinda na kumsaidia Assad katika vita vyake dhidi ya Uislamu na Waislamu. Licha ya hili, Waislamu wa Syria, wanawake na watoto, hawako tayari kuwasujudia wanamslaba hawa, kwa Imani yao kwa ushindi wa Uislamu kupitia nusra ya Allah (swt) haitingishiki. Wako imara, hata ingawa viongozi wa Waislamu wamekaa kimya na kuwasaliti, ambao hawakubwaga tu majukumu yao, bali wametelekeza utu wao kwa wengine, na kuwaachia wale walio na chembe ya utu kujaribu na kuwaokoa wanawake hawa wasiokuwa na usaidizi kutokana na watesaji wao. Nyoyo za watawala hawa na serikali hizi za Waislamu ni mmuliko wa nyoyo za wakoloni wanao watumikia, na wameonesha kuwa hawajali chochote kuhusu heshima na usalama wa mabinti hawa waheshimiwa wa Umma huu mtukufu.
Enyi Waislamu! Hapana shaka kuwa Allah (swt), Mwingi wa rehma na Mwenye Kurehemu, anayaona mapambano yenu kwa ajili ya dada zenu, na Yeye (swt) anazisikia dua zenu. Lakini pia ni wajib kufanya kazi kwa juhudi zenu zote kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida katika njia ya Utume, nidhamu pekee itakayo itikia miito yenu mara moja, na kwamba haitawaokoa tu ndugu zenu na dada zenu nchini Syria pekee, bali ulimwengu mzima. Kuweni na uaminifu kwa Allah Azza wa Jalla kwani kwa yakini Yeye atawapa Waislamu ushindi juu ya maadui zao. Hii ndio njia msingi ya kufaulu kule munako kutamani na munako kutaka. Enyi maafisa na wanajeshi katika majeshi ya Waislamu! Chukueni jukumu lenu katika Dini yenu na Umma wenu tena! Kataeni watawala hawa wasokuwa na utu na toeni Nusra (usaidizi wa kijeshi) kwa ajili ya Khilafah ili iwakunfungulie nguvu zenu zote kuwaoka dada zenu Waislamu kutokana na magereza ya muhalifu Bashar al-Assad.
﴾يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ﴿
“Enyi mlio amini! Mukimnusuru Allah, Naye atawanusuru na ataithibitisha miguu yenu…” [Muhammad: 7]
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 28 Jumada II 1439 | Na: 1439 AH / 016 |
M. Ijumaa, 16 March 2018 |