Muozo wa Kitabia na Kimaadili, ni Tunda la Mfumo muovu wa Kibepari.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Kitendo cha utekwaji wa mwanabloga wa Mombasa Bruce John,ambaye pia alilawitiwa na genge la watu, kimeibua hisia katika jijii la Pwani Mombasa na Kenya kwa ujumla. Mwito wa kutaka haki itendeke kwa wahusika wa kitendo hicho umesikika kila mahala huku marafiki, familia na watetezi wa haki za binadamu wakikongamana kumuunga mkono mwanabloga huyu chipukizi. Sisi katika Hizb ut Tahrir Kenya tungependa kutaja yafuatayo:

Ni jambo linalotamausha kuona kiwango cha kutisha cha mmomonyoko wa kiakhlaqi kilipofikia ngazi ya kimataifa. Hali hii imetokamana na fikra huria / tamaduni za Kisecular jinsi zilivyounda jamii kiasi cha kuiona ikichukua matendo maovu kama vile unyanyasaji na matusi kuwa ndio njia zao za kuelezea misimamo yao ya kisiasa.

Kiulimwengu, ni ukweli unaojulikana kwamba matendo ya ubakaji na uliwati yamekua yakitumika  kisiasa na kijeshi zinazotumika kama chombo moja wapo ya kuabiri/kuelezea chuki za kisiasa. Hata hivyo, hali hii inapaswa iwakumbushe wanadamu wote kwa ujumla na hususan Umma wa Kiislamu kufilisika kitabia na kimaadili kwa itikadi ya kisecula ambayo kwa hakika haina mwelekeo wa maadili. Tofauti na Uislamu, Usekula hutoa mwelekeo wa matendo yake kutokana na falsafa ya utilitiarinism inayolingania matendo maovu kwa lengo la kukuza “furaha au starehe” na kupinga matendo yanavyosababisha kutokuwa na furaha au madhara pindi kunapokabiliana na hali ya kufanya maamuzi ya kijamii, kiuchumi au kisiasa. Kwa yakini chini ya mfumo uliokosa maadili wa kibepari,jamii ya kibinadamu leo imekua mbaya zaidi hata kuliko wanyama kama Allah alivyosema ndani ya Quran

﴿ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ﴾

“Halafu Tukamrudisha  kuwa chini kuliko walio chini”

[TMQ At-Tiin: 05].

 

Kwa karne kumi na tatu, tokea kusimamishwa kwa serikali yake ya kwanza Madina, hadi kuvunjwa kwake na wakoloni wa kimagharibi 1924,kwa muda huo wote ndani ya Uislamu wanadamu walikuwa na ustawi mkubwa wa kitabia na kimaadili. Na hili lilidhirika kutokana na Aqeeda ya Kiislamu ilio na mwelekeo wa kulinda na kukuza maadili mema hivyo kudhaminia ufanisi katika nyanja zote za maisha. Ni dhahiri shahiri kwamba Uislamu ndio hitajio kubwa kwa zama zetu kuliko zama zote katika tarekh ya umma wa Kiislamu katika kunyanyua jamii kuwa na mwelekeo halisi wa kiimadili.

﴿وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلاً. [TMQ Al-Isra’a: 70].

“Na hakika Tumewatukuza wanaadamuna Tumewapa vya kupanda barani na baharini na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawatukuza kuliko wengi katika wale tuliowaumba kwa utukufu ulio mkubwa kabisa”

 

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

 Hizb ut Tahrir, Kenya