MWITO JUMLA KWA AJILI YA KUUNGA MKONO KADHIYA YA FILASTIN

MWITO JUMLA KWA AJILI YA KUUNGA MKONO KADHIYA YA FILASTIN

Kwa ndugu waheshimiwa Mshekhe na Maulamaa.

Kwa ndugu waheshimiwa Maduati, Makhatibu na Maimamu wa Misikiti.

 

Assalam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh

Baada ya maamkuzi Allah anasema :
{ إِنَّ هَـٰذِهِۦۤ أُمَّتُكُمۡ أُمَّةࣰ وَ ٰ⁠حِدَةࣰ وَأَنَا۠ رَبُّكُمۡ فَٱعۡبُدُونِ }
[سُورَةُ الأَنبِيَاءِ: ٩٢]
[Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi].

Na Mtume s.a.w asema: “Mfano wa waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kusikitikiana kwao ni mfano wa mwili, kikiuma kiongo mwili mzima huyumba kwa kukesha na homa.”
Hivyo basi ni wajibu kwetu katika hotuba za Ijumaa na katika hadhara zetu kukumbusha kadhia ya Waislamu, kadhia ya kibla chao cha kwanza, kuunga mkono kadhia ya Filastin na kupinga mashambulizi na uvamizi wa mazayuni. Tumetoa muongozo wa Khutba ya Ijumaa na tunaomba mufikishe ujumbe.
Twamuomba Allah awarahamu mashahidi na awapoze majeruhi na alete nasra ya karibu kwa Uislamu na Waislamu.

 

NUKTA MSINGI JUU YA KADHIA YA GHAZA:
1. Waislamu wa Filastin wameonyesha kwa mara nyengine ujasiri na ushujaa kiasi cha kuwaingiza hofu mayahudi. Asili ya Mayahudi ni madhaifu na makhawafu. Allah (SWT) asema katika Quran:

(ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ)
“Wamepigwa chapa ya dhila mahala popote wanapo kuwepo, (ila kwa kushika) kamba (dini )ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. [Aali-Imran 3:112]

Na Akasema:
(لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ)
“Hawatakudhuruni hao (maadui zenu khasa mayahudi) ila udhia mdogo tu. Na kama watapigana nanyi watakupeni migongo yao kisha hawatanusuriwa.” [Aali-Imran 3:111]

2. Kuwanusuru ndugu zetu Filastin waliodhulumiwa na kukaliwa kimabavu ni wajibu. Allah (SWT)
﴾وَإِنِ ٱسۡتَنصَرُوكُمۡ فِی ٱلدِّینِ فَعَلَیۡكُمُ ٱلنَّصۡرُ﴿
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfaal 8:72]
Kuitikia mwito huu wa kuwanusuru ndugu zetu Filastin ni lazima majeshi katika nchi za Kiislam ziende kuwanusuru waliokoloniwa na wasiomiliki silaha nzito kuweza kujikomboa na walowezi/wanyakuzi wa kizayuni. Viongozi katika nchi za Kiislamu pia wamekua ni kizuizi kikubwa na ndio waliowasaliti Waislamu wa Filastin kwa kuwekeana mikataba ya khiana na dola ya kizayuni na kuitambua uweko wake. Ummah ni lazima usimame dhidi yao na kuwaondosha katika viti vyao na kuweka kiongozi mmoja mukhlis atakae uhami/kuwanusuru Ummah wa Kiislamu popote walipo.

3. Unafiki wa nchi za kimagharibi pamoja na taasisi zao za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kufumbia macho maovu yanaofanywa na serikali ya kikoloni ya kiyazuni dhidi ya raia wa ki Filastin. Wenyeji wa Falastin wamekua wakiuwawa, kunyakuliwa ndani ya majumba yao, kufurushwa kwenye makaazi na kukalia ardhi zao huko taasisi hizo zikitijia hamanzo! …Kinaya ni kwamba wapiganaji wa Ukrain wamesifiwa kama wakombozi ilhali wapiganaji wa ki Filastin magaidi. Serikali nyakuzi ya kizayuni wanavunja maazimio ya UN kila siku bila yakuchukuliwa hatua yoyote lakini kwa nchi nyenginezo dhaifu huwekewa vikwazo

4. Kauli rasmi ya serikali ya Kenya kuunga mkono utawala wa kizayuni kwa kusema “…ina simama pamoja na serikali ya Israel dhidi ya magaidi…” si jambo la kushangaza kwani Kenya imawafungulia milango mashirika ya kijasusi ya nchi za kikoloni kama vile CIA, (Amerika) M16 (Uingereza) na Mossad (“Israel”) kuendeleza ukoloni na uwadui wao dhidi waislamu kwa kisingizio cha vita dhidi ya ugaidi.
Kabla kuamuliwa eneo gani Mayahudi watapewa kama makazi yao na mwisho kuamuliwa wapewe ardhi ya wa Filastin katika mkataba wa Balfour, Uganda ilikua ni moja wapo maeneo yaliopendekezwa. Jee yamaanisha Kenya ingeunga mkono walowezi wa kizayuni dhidi ya jirani zao?
Historia hapa Kenya, yatufunza kuwa katika miaka ya hamsini na sitini katika vuguvugu la kutafuta “uhuru” na kupigania ardhi zao walikua wakibandikwa majina ya magaidi ili kuhalalisha mauaji ya wenyeji na hao wakoloni ili kuwatia hofu wasiweze kutetea haki zao. Kati ya hayo makundi yalioitwa kuwa ni magaida walipokuwa watetea uhuru wao ni Mau Mau. Na huko Afrika Kusini nako ni vilevile waanzilishi wa chama ANC akiwemo Nelson Mandela aliitwa gaidi!

5. Sisi tulioko mbali twaweza fanya nini kwanusuru ndugu zetu? Kwa hakika tunawajibika kuwakumbuka ndugu zetu kwa dua kwenye swala zetu kibinafsi au za jama’a kama Ijumaa, kuwasaidia ki mali, kujijuza kuhusu qadhia yao na zote zinazowagusa Waislam ulimwenguni kwa kufuatilia matokeo ya kiulimwengu na kujua njama wanazo tupangia maadui zetu. Baada ya kujua basi ni kuwajuza Waislamu na kujijuza kwa wajuzi njia ya kujikomboa.

6. Mwisho, suluhu la kudumu ni kuleta umoja wa Ummah hata kama twakhtalifiana katika masala ya kifiqhi baina yetu. Walikhtalifiana waliokuwa bora katika karne za mwanzo wakiwemo maswahaba lakini walikua ni wamoja. Udhaifu wetu wadhihirika kwa kuwa tumegawanywa kimipaka, kabila, madhehebu nk… Huu umoja hautopatikana illa tuwe chini ya kiongozi moja ambae atatulinda na shari za makafiri maadui wa Uislamu. Mtume (saw) asema:
“Hakika ya Imamu (kiongozi) ni ngao, watapigana (waislamu) nyuma yake na atawakinga”

 

Kwa haya, twaomba Ijumaa hii tuleteni Qunuti kuwaombea ndugu zetu nusra.

 

Hizb ut Tahrir Kenya
11/10/2023 sawa na 26 Rabiul Awwal 1445 AH