Ngono za wanafunzi: tunda jengine ovu la Urasilimali

Ngono za wanafunzi: tunda jengine ovu la Urasilimali. Baada ya kushuhudiwa kwa kuanguka chumi za mataifa mengi duniani ikiwemo za mataifa makubwa, kumeripotiwa kwa vitendo viovu vya kajamii kama vile mizozo ya majumbani na ngono kwa wanafunzi wa shule.

Ripoti za hivi majuzi kwa wasichana wengi wa shule wamepachikwa ujauzito tokea shule kufungwa yapata miezi mitatu iliyopita ni ya kutamausha. Ufuska huu umekuwa ukisuhubu shule nyingi  ziwe za mabweni na zile za kutwa. Tafiti za miaka ya hivi karibuni nchini Kenya, zinaonyesha kwamba takriban wasichana wa shule laki moja Hamsini na mbili elfu, mia nane na ishirini (152, 820) kote nchini wametiwa mimba tokea kufungwa kwa jaribio la serikali la kupambana na maradhi ya Corona. Takwimu hizi ingawa zimetiwa shaka na wadau wa elimu serekalini lakini kihakika ni ushahidi tosha kuwa zinaa ni moja wapo ya machafu yaliyosambaa kwa kasi kubwa ndani tawala za Kidemokrasia.

Janga hili limekua kubwa hata kabla ya janga la virusi vya Corona. Wasichana wa shule kujihusisha na ngono, makahaba wanaozunguka mijini, vitendo vya uliwati na usagaji yamekuwa ni mambo yaliyozoeleka leo katika jamii tunayoishi. Matokeo ya uchafu huu, vifo vingi vya wasichana na wanawake vinavyotokamana na maradhi yanayoambukizwa kupitia ngono kama vile Ukimwi na kaswende. Kutupwa kwa vijusi kwenye mapipa na miito kumeshuhudiwa. Katika hali ya kutamausha takriban ni kupatikana kwa vijusa takriban thelathini waliokotwa ndani ya mto wa Nairobi.

Kumekuweko mchezo wa kutupiana lawama kati ya serikali, walimu na wazazi kuhusina na tatizo hili. Wazazi wakitupia lawama usimamizi wa shule kwa kutowajibika vyema majukumu yao bali huku baadhi ya waalimu pia wakihusika na vitendo vya ngono na wanafunzi. Kwa upande wao, waalimu wakitaja kuwa ni kutokamana na utepetevu wa wazazi juu ya malezi ya watoto wao ndio kumechangia janga hili. Mbali na haya suala la kuondosha adhabu ya kuwapiga viboko wanafunzi shuleni limetajwa kuchangia ufuska huu. Itakumbukwa mwaka 2018 kuliposheheni uhuni wa wanafunzi wa kuchoma mabweni ya shule, baadhi ya wabunge kama vile mbunge wa Gem; Elisha Odhiambo na mwakilishi wa wanawake wa Nyandarua Faith Gitau waliitaka serikali kurudisha tena adhabu ya viboko shuleni ili kurudisha nidhamu.

Kwa jinsi ya mazingira ya janga hili, kwa hakika utakuta ni lenye kufungamana na mfumo kibepari na siasa yake ya Kidemokrasia unaotawalishwa katika jamii. Ubepari kupitia sera zake mbovu za kiuchumi zilizodhikisha  maisha ya watu wengi kwa mahisabu ya watu wachache, hivyo wanaweke na wasichana hubidi kujiuza miili yao kukimu maishani. Ubepari pia kwa kule kujaalia kipimo cha maisha duniani ni maslahi hali inayofanya mwanadamu afukuze maslahi kwa njia yoyote. Kwa msingi huu wa kimakosa wasichana wengi leo hughilibiwa na tamaa ya kimaisha kwa kujihusisha na ngono.

Mbali na haya, Demokrasia, siasa inayopigiwa debe na wamagharibi katika jamii ya Kiislamu kwa madai kuwa ndio siasa yenye ufanisi wa hali ya juu, imechangia janga hili. Demokrasia mbali ya kuwa ni utaratibu wa kisiasa unaovisha mwanadamu taji la kutunga kanuni kinyume na sheria za Mwenyezi Mungu, imepalilia janga hili kwa kumfungulia mwanadamu uhuru wa kila jambo. Kwa maana haya kupitia uhuru wa kibinafsi, uhuru wa kutangamana na miongoni mwa uhuru nyingine imefanya wasichana wakose haya kwa kutembea uchi huki wakidhani kuwa wamevaa! Mtindo wa mavazi haya  na kuanika peupe miili yao mitaani, huku idhaa nyingi zikishajiisha ngono kupitia vipindi vichafu mambo haya yamechochea pakubwa kwa hali hii.

Kwa uhalisia huu, katu janga la mimba kwa wanafunzi wa shule ni lenye kuendelea ndani ya mfumo usio na maadili hata chembe. Hivyo basi, kuepukana tatizo hili ni kupatikane mfumo mbadala nao si mwengine ila Uislamu. Sheria za Kiislamu kutekelezwa kwake duniani ndio huletea jamii kuishi katika mustawaa wa hali ya juu wa kimaadili. Uislamu umekuja na lengo la kuhiifadhi mwanamke asije kufanywa na kuwa chombo cha starehe hii ni kupitia kumkalifisha baba kusimamia mahitaji ya wanawe na hili huwuezekana ikiwa serikali kwa upande wake inawajibika katika kubuni nafasi za kazi kwa raia wake. Aidha, Uislamu umetaka rasilimali ziwafikie raia wote pasina ubaguzi.Uvaaji wa Hijab, na kuchungwa mipaka ya matangamano baina ya wanaume na wanawake yote hiyo ni miongoni mwa sheria tukufu za Uislamu zinazofanya mwanamke aweze kulindwa heshima yake.

Uislamu pia katika nidhamu yake ya Uqubat (Utaratibu wa kuadhibu wahalifu) umeweka bayana adhabu ya bakora mia kwa wale wanaohusika na matendo ya zinaa na utekelezwaji wa adhabu huwa ni kuzuia machafu haya kuenea. Pamoja na haya, ni muhimu kuelewa kuwa sheria hizi za Kiislamu haziwezi kutekelezwa na watu binafsi bali ni serikali ya Kiislamu ambayo kwa bahati mbaya leo duniani hakuna serikali hii. Kwa maana haya, inakuwa ni faradhi kwa Waislamu wote duniani kuisimamisha tena ili maovu haya na mengineyo yaweze kuzuiliwa kimsingi.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut-Tahrir Kenya
29/06/20.