Nini Mwaka Mpya?

Hili ni suali ambalo kila binadamu anaweza kulijibu kwa mtizamo wake. Au kwa maana nyingine anaweza kulijibu kutegemea na fikra anazobeba ndani ya bongo lake. Usahihi wa Fikra zake hutegemea itikadi anayoiamini binadamu. Hivyo basi itikadi ikiwa sahihi fikra zake zitakuwa sahihi natija yake ni ufahamu (majibu) sahihi. Kinyume chake ni kuwa itikadi ikiwa ya kimakosa basi fikra zake zitakuwa za kimakosa na natija ni ufahamu (majibu) ya kimakosa.

Hivi leo itikadi iliyoko mamlakani/inayotawala ni ya kiilmaniyya/kisekula inayotokana na akili za wanadamu na imekitwa katika kutenganisha dini na maisha. Itikadi ya kisekula mfumo wake ni urasilimali kwa kuwa kipaombele chake ni nidhamu yake ya kiuchumi inayotokamana na uhuru wa kumiliki. Itikadi ya kisekula imelifanya lengo la binadamu kuweko maishani ni kujistarehesha kwa upeo wa juu. Na kipimo cha vitendo vya binadamu ni maslahi/faida/hasara. Mwanadamu anajitungia mwenyewe sheria za kuendeshea maisha jumla kila nyanja ya maisha kiuchumi, kisiasa, kijamii, kielimu n.k. Itikadi ya kisekula imemdhamini binadamu uhuru sampuli nne: uhuru wa kuabudu, uhuru wa kumiliki, uhuru wa maoni na uhuru wa kibinafsi. Na Jukumu la Serikali ni kuhifadhi kwa hali na mali uhuru hizi nne. Itikadi ya kisekula inapigiwa debe na wamagharibi wakoloni wakishirikiana na watawala vibaraka wanaowamiliki kote ulimwenguni wakiongozwa na kiongozi wa ulimwengu hivi sasa Marekani. Kwa kuwa itikadi hii inatokana na akili za binadamu basi jibu lake litakuwa la kimakosa. Nalo ni kuwa “Mwaka Mpya ni fursa ya kuweka mikakati mipya ya kimada itakayokupelekea kujistarehesha zaidi ya mwaka uliopita!”

Kinyume chake ni mfumo wa Uislamu na itikadi yake ya Laa ilaha ila llah Muhammad Rasulullah (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wake). Itikadi ya Kiislamu imetoka kwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Itikadi hii imewafanya wanadamu kuwa watumwa wa Mwenyezi Mungu ambao lengo lao maishani ni kutafuta radhi za Muumba wao. Daima wamefungwa na kipimo cha Halal na Haram katika vitendo vyao. Kwa kuwa itikadi hii inatoka kwa Mwenyezi Mungu basi jibu lake litakuwa la sawa. Nalo ni kuwa “Mwaka Mpya ni fursa ya kujihesabu kuhusiana na umri wako (Umepungua tena kwa mwaka mmoja). Hivyo unakaribia kifo chako (ambacho ni wakati wowote). Na kujiuliza ikiwa umedumu katika muongozo wa Mwenyezi Mungu au la? Ikiwa umedumu ni wapi pa kuboresha zaidi na ikiwa hukudumu ni wapi pa kurekebisha kwa haraka kabla mauti yako?  

Lakusikitisha ni kuwa mfumo wa Uislamu hivi sasa hautawali ulimwengu na kinyume chake mfumo wa kisekula wa kirasilimali unatawala tena kwa njia ya uhadaifu. Imepelekea watu badala ya kujisikitikia na kujiuliza maswali hayo hapo juu; watu wanaandaa na kushughulishwa na sherehe za mwaka mpya! Waislamu nao wakiwa ni miongoni mwa waliotekwa nyara kutokana na wao kutawaliwa na kuwekwa mbali na mfumo wao wa Uislamu na badala yake kuachiwa nafasi tu ya kutekeleza masuala machache mfano kuswali, ndoa, talaka na mirathi lakini sheria jumla ni za kikafiri!

Zawadi bora ya kujipa ndani ya mwaka huu mpya ni wewe kujiunga na ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha tena Serikali ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah pekee ndiyo itakayo wasimamia raia wake kwa uadilifu kwa kuwa chimbuko lake ni Qur’an na Sunnah kinyume na dola za kisekula za kirasilimali zilizoko leo duniani. Khilafah itawajengea raia wake mazingira ya uchajimungu kiasi kwamba Mwaka Mpya itakuwa kama tulivyoelezea katika jibu hapo juu kwa mujibu wa itikadi ya Kiislamu.

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya