Katika jamii yoyote ile ya wanadamu ni maumbile watu kutofautiana katika ustawi wa maisha na daima hukuepukiki kuweko na matajiri na masikini katika jamii. Hata hivyo, katika jamii ya kibepari leo mwanya wa matajiri na masikini hukuzwa na kuwa mkubwa mno hii ni kwa sababu asili ya mfumo huu ni kujali maslahi ya kipote kidogo cha watu. Gazeti la The Standard tarehe 17 Januari, 2017 lilichapisha habari kwenye ukurasa wake wa mbele kuhusu ripoti ya kutamausha ya shirika la Oxfam kuwa watu wa nane (8) duniani ndio wanao miliki utajiri wa watu bilioni 3.6! Hii ina maanisha wanane hawa wanamiliki mali za nusu ya idadi ya watu kote duniani!
Licha ya ukuaji wa kitekenolijia na uundaji wa sera za ‘kiustarabu’ bado kila kukicha pengo la masikini na matajri linazidi kukuwa zaidi. Baada ya vita vya pili vya Dunia kumalizika mwaka 1945, Marekani iliibuka kuwa na dhahabu nyingi jambo lililoipelekea kuhifadhi thamani ya sarafu yake ya dollar kwa dhahabu jambo lililofanya nchi nyingi nazo kuhifadhi thamani ya sarafu zao kwa thamani ya sarafu ya dola ya Marekani. Hatua hii iliipa nguvu Marekani kuliko nchi nyengine. Mwaka 1968 baada ya Marekani kujihusisha na vita baridi ilitumia dhahabu nyingi katika vita hivyo kiasi kulazimika kuchapisha pesa za ‘fiati’ au pesa zisizo kuwa na thamani ya dhahabu na kupelekea dola bilioni 900 hadi dola trilioni 3.5 kuwa katika mzunguko kwa miaka 2. Hali hii iliipelekea Benki Kuu za Serikali ambazo zinatumia sarafu ya dollar ya Marekani kwa thamani ya sarafu zao; kuchapisha pesa za ‘Fiat’ kuweza kununua dollar. Jambo hili lilipelekea serikali kuchukua hatamu ya usimamizi wa uchumi na sera mpya na nadharia zikaibuka.
Kenya ikiwa moja ya nchi ambazo huhifadhi sarafu yake kutumia dollar ya Marekani haikuachwa katika sera na natharia za kiuchumi ambazo zilibuniwa na wachache wenye nguvu ili kuhifadhi utajiri wa ambao unaathri kiuchumi.
Hizi ni baadhi ya nadharia zinazotumika katika kuendeleza unyanyasaji wa kiuchumi:-
- Uhaba wa Rasilimali: Huu ndio msingi wa uchumi ulimwenguni leo unaoashiria kuwa mahitaji ya wanadamu ni mengi na ni yenye kujirudiarudia na ati kuna uhaba wa rasilimali. Kwa hali hudaiwa kuwa rasilimali leo haziwezi kushibisha mahitaji ya watu. Na ili kutatua tatizo hili wanaloliita ‘tatizo msingi la kiuchumi’ husemwa kuwa juhudi nyingi zaidi ziielekezwe kwa uzalishaji rasilimali. Lakini wapi! Uzalishaji sio tatizo msingi la kiuchumi bali ni usambazaji wa zile rasilimali zinazozalishwa. Kwa mfano hapa Kenya rasilimali nyingi lakini wanaozalisha ni wachache na kubwa zaidi hazisambazwi kwa watu umasikini huzidi kila siku. Rasilimali kama vile Limonite inayochimbwa huko Pwani Kusini na makampuni ya kibinafsi ya Titanium Base iliweza kupata tani milioni 3 za madini hayo katika kipindi cha Mwezi wa Septemba na Disemba na inayouzwa tani moja kwa bei ya Sh 14000. Hii ikimaanisha kuwa kampuni hiyo iliweza kupata bilioni Ksh 42 ndani ya kipindi cha miezi mitatu 3 lau ingelikuwa ni serikali ingeli jipatia bilioni Ksh.168 ndani ya mwaka mmoja. Kwa mujibu wa habari zilizo peperushwa na shirika la Africa Oil, tathmini huru iliyofanywa na Gaffney, Cline & Associates mwaka 2014 ilikadiria zaidi ya pipa milioni 600 ya madini ya propabeli (2C) ambayo ina thamani ya mabilioni ya dola za Marekani. Mafuta zaidi yamekuwa yakipatikana tokea wakati huo. Zungumzia madini ya magadi kutoka ziwa Magadi kama Fluorspar huko Kerio Valley, Nobium, Lead na Shaba huko Si tu madini hayo bali hata ukulima na mengi zaidi ambayo yana uwezo wa kuzalisha mapato mengi yatakayotumika kwa miaka mingi bila kuomba misaada ya nje.
Kwa hiyo nadharia hii iliwekwa ili rasilimali zote ziweze kumilikiwa na mashirika machache yanayomilikiwa na watu binafsi wachache na kuwaacha wengine wakiwa masikini wa kupindukia.
2- Kusambaza uchumi: Nadharia hii inaashiria kuwa wanapopunguziwa ushuru matajiri basi hupelekea kuwaajiri watu wengi zaidi na hivyo kupelekea kukua kwa uchumi wa eneo. Nadharia hii imeyarahisishia makampuni kupata faida zaidi kwa kulipa ushuru kidogo au kutolipa kamwe ilhali mwananchi wa kawaida ana beba mzigo wote wa ushuru ambao una mrudisha hatua ya kwanza kila anapojaribu kujikwamua kimaendeleo.
Nadharia hizi na nyenginezo zinategemea mashirika na wadhamini wake ambao huzitumia kuendesha uchumi. Uhaba wa ajira umekuwa kwa asilimia 60 miongoni mwa vijana na wale asilimia 40 walioajiriwa manuafaa yao yanazidi kudidimia. Idadi ya wafanyikazi walio na mpango walio na mpango wa pensheni kwa mujibu wa ajira zinadorora. Zaidi ya wafanyikazi 10,000 mwaka 2016 walisitishwa kazi ndani ya kampuni zaidi ya 20 ikiwa baadhi yao ni Kenya Airways (118), Benki ya Standard Chartered (300), Farm Karuturi (2,600), Benki ya Family (100), Telkom (500), Benki ya First Community (100), Benki ya Equity (400), Samir Africa (600), Portland Cement (1,000), Kenya Fluorspar (700), Uchumi (253), Airtel Kenya (80), Kenya Meat Commission (118) na nyengine zinatarajiwa kufuata.
Thamani ya shilingi imeanguka kiasi ikilinganishwa na dollar, hali hii imewepelekea wamililiki wa mitambo ya kusaga kutoa ilani ya kupungua kwa nafaka kutalazimisha kuongezeka kwa bei ambayo itawasukumia wananunuzi madukani kwani bei hiyo itapanda kwa muda mrefu. Licha ya haya yote, Mapato ya Taifa (GDP) la Kenya yalikuwa kwa asilimia 6.2 mwanzoni mwa robo ya pili ya mwaka 2016 na kuongezeka zaidi jambo linaloashiria hali nzuri ya kiuchumi kiasi cha Benki kuu ya dunia ikaiorodhesha Kenya kuwa nchi ya 3 katika nchi zilizoboresha hali ya kufanya biashara nchini mwake na kuongezeka kutoka 21 katika ya nchi 100 zilizonamazingira bora yakufanya biashara. Hii inaonyesha wazi tofauti kati ya nadharia za kiuchumi na uhalisia wa maisha magumu ya mwananchi wa kawaida.
Matajiri wachache wamefaulu kujilimbikizia idadi kubwa ya utajri na kuwafanya wananchi wa kawaida ni wanunuzi tu. Wanawakopesha ili waweze kununua bidhaa msingi ambazo wameziunda kisha kuwafanyisha kazi ili walipe mikopo waliyowakopesha. Njia ya kujinasua na hali hii ni kurudi katika kutumia dhahabu ili kuhifadhi thamani ya pesa za makaratasi na kubadilisha mfumo wa Urasilimali ambao ndio chanzo cha sera msingi za uchumi usiongiliana kiakili na nadharia zilizobuniwa ili kutoa nafasi kwa pengo kati ya masikini na matajiri kuzidi.
Bakari Mohamed Dziphengo– Mwanachama Katika Ofisi ya Habari
Hizb ut-Tahrir Kenya
Kutoka Jarida la UQAB Toleo 1