Mwezi mtukufu wa Ramadhan(mwezi wa 9 katika kalenda ya kiislamu) yalitukia ndani yake matukio mengi ya kufurahisha, Isipokuwa tangu Khilafah ivunjwe, historia hii ilibadilika na kuugeuza mwezi huu kuwa ni mwezi wa majonzi na umwagikaji wa damu za waislamu. Mwaka huu Ramadhan imeingia ilhali ndugu zetu Gaza na Falastin kwa ujumla, hawana amani, maelfu wameuwawa mikonono mwa umbo la kiyahudi. Huku wamagharibi wakiongozwa na Mwamerika wakisaidia katika mauwaji haya.
Kwa hakika mwezi mtukufu wa Ramadhan umekuwa mwezi wa majonzi na huzuni nyingi mno, hasa ukizingatia ya kwamba ni Karne Moja tangu ngao yetu, #khalifah kuvunjwa Rajab 28, 1342 iliyoafikiana na Marchi 3 mwaka wa 1924. Ni Ramadhan ya Mia Moja ambapo waislamu tumebaki kuchaguwa ni hukmu gani tuitabikishe na ni ipi tuiwache. Ni Ramadhan ya mia moja ambapo twaishi na kutawaliwa na sheria sisizo za Allah (swt).
Ni Ramadhan ya mia moja ambapo twaishi pasi na kutabikishwa risala ambayo Allah (swt) asema ni rahma kwa walimwengu. Ni Ramadhan ya mia Moja tukiishi sio tu bila Khalifah bali twaishi bila kutekeleza faradhi ya kumtii kiongozi huyo.
Enyi waislamu; kumbukeni mwezi mtukufu wa Ramadhan ulikuwa ni mwezi wa kufanya kazi na kufungua miji. Vita vya Badr bali ufunguzi wa Makkah ulifanyika ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Bali siyo hayo tu! bali ni mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo Salahudeen Al Ayub aliweza kupambana na Masalabiyyun (Crusaders) na akausafishi masjid Al Aqsa kutokamana na uchafu wao.
Leo miji yetu yakaliwa na Makafiri, kunajisiwa na vibaraka waliopandwa na wamagharibi. Damu zetu zamwagwa sio Chechnya, Uighur, Sudan, Ethiopia, Gaza na kadhalika. Hayo yote yanafanyika ila kwa masikitiko makubwa hata tumeshindwa kutekeleza faradhi ambayo katika aya yaanza kama ilivyoanza aya ya kutuamrisha tufunge mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
Allah (SWT) asema katika Surah Al Baqarah 216
كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَنْ تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَكُمْ ۗ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
[Mmefaradhishiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui].
Haya yote yanafanyika kwa sababu ummah wa kiislamu umekosa mtawala wa kiislamu, Khalifah ambaye ataongoza waumini kuingia katika uwanja wa vita ili kutekeleza faradhi hiyo.
Kuna faradhi chungu nzima ambazo haziwezi kutekelezeka ila mpaka kuwepo na mtawala wa kiislamu. Hii ikiwa na maana suala la kumtafuta Khalifah ni faradhi juu ya kila Muislamu. Khilafah ni msingi ambao nguzo za Uislamu zalala juu yake.
Hivyo enyi waislamu, enyi ummah bora mliotolewa kwa ajili ya watu, kumbukeni huu ni mwezi sio wa kulala bali ni mwezi wa kufanya kazi na miongoni mwa kazi za kufanya ni kazi hii ya kurudisha maisha ya kiislamu, Khilafah. Mwezi huu tuirudishe historia kwa kufanya kazi huku tukielekea nyuso zetu kwa Allah (swt) tukimwomba atuharakishie Nusra yake.
Musa Kipngeno Rotich
Mwanaharakati wa Hizb ut Tahrir,
Kenya.