Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Huku umma unapoingia katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, Hizb ut-Tahrir Kenya ingependa kutuma risala zake za dhati kuwapongeza Waislamu wa Kenya na ulimwengu kwa ujumla.Tunamuomba MwenyeziMungu (SWT) atupe nguvu na afya za kuweza kuitekeleza ibada tukufu ya swaumu ambayo licha ya kuwa ni faradhi bali pia ni miongoni mwa nguzo tano za Uislamu.
Kwa bahati mbaya, Ramadhani ya mwaka huu inaanza ikiwa Waislamu humu nchini na duniani kote wamezuiliwa kutekeleza ibada ya swala ya Ijumaa na Swala nyengine za Jamaa misikitini.Wanavyouni wa kiserikali kama ilivyo mazoea waliifunga misikiti kwa haraka hata kabla ya serikali ilikuwa bado haijatoa ilani ya kuifunga. Kwa hakika hatua hiyo ya wanavyuoni sio ngeni ikizingatiwa kuwa tayari wamekuwa wakitoa fat-wa zinazongana wazi na Quran na Sunna. La kutamausha zaidi, ni kwamba baadhi ya fatwa mbovu zimekuwa zikitolewa kwa kuunga mkono utiaji saini wa mikataba ya kidhulma ambayo bado ni yenye kuletea umma udhalilifu umma mtukufu wa Kiislamu. Tunasema kuwazuia Waumini kutotaja jina la MwenyeziMungu ni kitendo cha kidhulma kinachokwenda kinyume na sheria ya Kiislamu.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا ۚ أُولَٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ
“Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kwamba humo lisitajwe jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo misikitini ila kwa kuogopa. (Yaani watieni adhabu kwa ubaya wao huo hata wawe katika khofu). Hao watapata fedheha katika dunia, na katika Akhera watapata adhabu kubwa.” [Al-Baqara: 114]
Tunasema, katika kipindi cha mkurupuko wa maradhi, kinachotakikana na sheria ya Kiislamu sio kuzuia Waislamu wote kijumla kuswali za jamaa bali kinachotakikana ni kuwatenga na kuwazuia wale wagonjwa kuingia misikitini.Kinachopaswa kufanywa kuzuia maambukizi ya maradhi, ni kuweka mikakati ya kujikinga na maambukizi kama vile udumishwaji wa usafi, kuvaa vitanzua (vibarakoa) kupima watu na kuosha mikono. Dalili ya haya ni hadithi iliopo katika Mustadarak ya Al-haakim kutoka kwa Twariq bin Shihab aliepokea kwa Abi Musa kutoka Kwa Mtume SAAW kwamba alisema:
الْجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلَّا أَرْبَعَةٌ: عَبْدٌ مَمْلُوكٌ، أَوِ امْرَأَةٌ، أَوْ صَبِيٌّ، أَوْ مَرِيضٌ»))
((Swala ya Ijumaa ni haki ya uwajibu kwa kila Muislamu katika jamaa ispokuwa kwa watu wanne: Mja anaemilikiwa, Mwanamke, mtoto na mgonjwa.))
Ama kuhusiana na swala za jamaa, Sheria imeeleza kwamba swala hiyo ni faradhi ya kutoshelezeana (Fardhul kifaya). Abu Darda radhi za MwenyeziMungu zimshukie amepokea kutoka kwa Mtume SAAW kwama alisema:
مَا ِمنْ ثَلَاثَةٍ فِي قَرْيَةٍ وَلَا بَدْوٍ لَا تُقَامُ فِيهِمْ الصَّلَاةُ إِلَّا قَدْ اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمْ الشَّيْطَانُ، عَلَيْكَ بِالْجَمَاعَةِ فَإِنَّمَا يَأْخُذُ الذِّئْبُ مِنَ الْغَنَمِ الْقَاصِيَةَ »
Hawawi watu watatu katika mji wala mashamba ndani yao ikawa haisimamishwi ndani yao Swala ispokuwa Sheitani huwa amewatawalia, jilazimishe na swala za jamaa kwani mbwa mwitu hula mbuzi aliekuwa peke yake. [Abu Daud]
Kiukweli Ramadhani huletea kheri umma mzima wa kiislamu lakini umma kwa sasa unakumbwa na janga la Covid 19 ambalo kwa mara nyingine limefichua utepetetevu wa viongozi wa kirasilimali. Udhaifu wa mfumo wa kibepari umewekwa peupe kwa kila mtu kuona. Mfumo huu uko duni zaidi kama nyumba ya buibui nyumba duni zaidi – mfumo ambao hata kabla ya kutokea majanga wenyewe tayari ni majanga. Mikakati ya watawala wa kirasilimali ya kujaribu kuokoa uchumi si lolote ila majaribu ya kutaka kuzuia maovu ya mfumo wao maiti unaosubiria tu tangazo la tarehe ya mazishi yake.
Huku tunaposoma Quran ndani ya Mwezi huu wa kheri, Waislamu wanawajibika kuelewa kwamba maafa yote wanayokumbana nayo leo yataaondoka ikiwa watatekeleza faradhi ya kusimamisha Khilafah kwa mfumo wa Mtume katika moja wapo ya nchi kubwa za Kiislamu. Na ni kwa sababu ya kutoitekeleza/kuitabikisha Quran katika maisha yao ndio Waislamu wanaonja maafa na majanga yote katika maisha yao jumla.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir in Kenya
REF: 1441/09 AH
Jumapili, 26th Shaaban 1441 AH/
19/04/2020 CE