Habari&Maoni
Habari:
Madaktari katika hospitali za umma nchini Kenya wako kwenye mgomo wa nchi nzima, wakishutumu serikali kwa kukosa kutekeleza safu ya ahadi kutoka kwa makubaliano ya pamoja ya mazungumzo yaliyotiwa saini mnamo 2017 baada ya mgomo wa siku 100 uliosababisha watu kufa kwa kukosa huduma za matibabu. Muungano wa Madaktari na wahudumu wa afya Kenya walisema waligoma kudai matibabu kamili kwa madaktari hao na kwa sababu serikali bado haijatuma wahudumu wa matibabu 1,200.
Maoni:
Mgomo wa madaktari ambao sasa umeingia wiki ya tatu ni ushahidi wa wazi usiopingika kwamba sekta ya matibabu katika serikali za Kibepari ni yenye kupuulizia mbali. Athari za mgomo huo zinaonekana kote nchini huku wagonjwa wengi wakiachwa bila uangalizi au kuzuiliwa kutoka kwa vituo vya afya vya umma. La kutia machungu zaidi, vigogo wa kisiasa wakubwa hulipiwa kwa wepesi huduma zao matibabu ilhali raia wasojimudu hupuzwa! Hali hii ni ya kutamausha bali kufedhehesha kwa serikali yoyote inayodai kuhudumia raia wake ambao kiasili ndio hutwishwa zigo linalowalemea la ushuru; huku wakiwaacha wakiteseka katika hospitali za umma kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata matibabu.
Madaktari wanaogoma wanapaswa kutambua kwamba misingi miovu ya mfumo wa Kibepari ndiyo chanzo kikuu cha hali yao mbaya.Migogoro yote ya mara kwa mara katika huduma za umma inayosababisha migomo ya kudumu ya wafanyakazi wa umma inahitaji suluhisho la kimfumo ambalo kattu haliwezi kutokea ndani ya mfumo fisidifu wa Kirasilimali.
Huku ikiwa matakwa haya ni kweli lakini madaktari pia wameathirika pia akili ya kibepari.Ubepari umejikita utoshelevu wa kimada usio na uroho na ndio kigezo pekee maishani na huchochea wataalam wa matibabu kukuza hulka ya kupenda kujilimbikizia mali kupitia mikataba ya kifisadi. Madaktari wakorofi wamekuwa wakiwanyanyasa wagonjwa wa kike kingono.
Mfumo mbadala wa Ubepari si mwingine bali ni Uislamu ulioweka matibabu kama moja ya mahitaji ya kimsingi ya umma yanayopaswa kuwa na uangalizi wa umakini mkubwa. Uislamu hauoni huduma za afya au huduma yoyote ya umma kama fadhila bali huiangalia na kuipa kipaumbele ambapo serikali yapaswa iwape raia wake wote.
Uislamu umeeleza zaidi kwamba mshahara wa madaktari unapaswa kulipwa kutoka Hazina ya Serikali (Baitul Maal). Licha ya hayo, Uislamu pia ulipiga marufuku utozaji wa ushuru kwenye mshahara wa mfanyakazi, hii ni katika kuwawezesha kukidhi mahitaji yao ya kimsingi. Kwa kuzingatia hilo, tunasema bayana kwamba kwa kusimamisha tena dola ya Khilafah (Ukhalifa) juu ya mfumo wa Utume duniani, hukumu zote hizi tukufu zitatekelezwa kikamilifu hivyo basi haitakuwa migomo ya mara kwa mara ya wafanyakazi wa umma ni yenye kushuhudiwa.
Imeandikwa kwa Niaba ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya