Habari na Maoni
Habari: Siku ya Jumapili Mei mosi 2022 rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitangaza ongezeko la asilimia 12 kwa mshahara wa mfanyikakazi kuanzia tarehi 1 Mei ili kuwakwamua wafanyakazi ambao kwa sasa wanashuhudia mbano wa mfumko wa bei, hasa kwa bidhaa za vyakula na mafuta.
Maoni:Ulimwengu ulisherehekea siku ya kila mwaka ya wafanyakazi tarehe mosi Mei ambapo hapa Kenya raisi Kenyatta alitangaza ongozeko la kiwango cha chini cha mshahara kwa asilimia 12. Sekta ya ajira nchini Kenya imekua ikisuasua kwa asilimia 83% ya sekta isiyo rasmi almaarufu kama “Jua kali” na chini ya 17% katika sekta rasmi. Ongezeko hili lina maana ya Ksh 15,200 sawa na $129 kwa mwezi.
Utabikishwaji wa Sera za mishahara ya kiwango cha chini una athari zifuatazo kwenye sekta ya soko la wafanyikazi:
- Huzalisha uhaba wa kazi kwani baadhi ya waajiri hutaka kupunguza gharama za kazi kwa lengo la kujiongezea faida.
- Kuwapuuza wafanyikazi wasokuwa na ujuzi kwani waajiri siku zote hutafuta faida kubwa katika kuajiri watu kazi .
- Kwa sababu za kisiasa,mishahara ya kiwango cha chini huweza kutumiwa kwa lengo la kudharau sekta ya kazi ili kufaidisha kiuchumi tabaka fulani la watu na hii ni kama ilivyoshuhudiwa katika nchi ya Afrika Kusini kwani mshahara uko juu, jambo ambalo linawafanya waafrika weusi wakose njia m’badala kutokamana na kiwango kidogo cha elimu na kutokuwa na ujuzi.
Hivyo haya na mengine mengi yanaifanya sera hii kuwa ya kiunyanyasaji na zana ya kisiasa ya kupalilia ubaguzi wa rangi na utabaka katika jamii.
Ni muhimu sana kutambua kwamba kipimo cha mishahara cha kiwango cha chini na suala zima la mshahara kwa ujumla ndani ya sekta ya uajiri imejengwa juu ya msingi wa kiwango mustawaa wa kimaisha. Kipimo hiki ni cha kimakosa kwa kuwa maslahi anayoyapata yule mwajiri kinatofutiana na zile juhudi zinazotolewa katika uzalishwaji wa huduma na bidhaa.
Kwa ufahamu huu, kima cha chini cha mshahara ni kiwango cha unyonyaji kinachokusudiwa kutuliza uchungu wa watu huku mateso na hofu ikiendelea kushika kasi kutokana na mfumuko wa bei na kudhoofisha shilingi ya Kenya dhidi ya ile ya dollar ya Marekani.
Kwa upande mwengine wa mfumo wa kibepari ni suala la utozwaji ushuru na viwango vya riba ambavyo kiuhalisia hufanya maisha ya raia kuwa magumu kila uchao.
Enyi watu wenye ufahamu, ulimwengu unaweza kujinasua katika dhiki na shida za mfumo muovu wa kibepari usio na ubinadamu hata chembe .. na hili ni kwa kupitia kufanya kazi kuelekea kusimamisha Mfumo unaotoka kwa MwenyeziMungu unaohakikishia jamii mustawa wa hali ya juu ya kimaadili na kuwa na suluhu ya matatizo yote ya wanadamu. Aidha Mfumo huo una utaratibu bora wa kisiasa tena wa kipekee unaopima mishahara kutokana na manufaa yanayozalishwa. Utambuzi wa mfumo huu adhimu katika nyanja ya maisha ni kwa kusimamisha dola ya Khilafah. Mfumo unaozingatia mgawanyo sawa wa mali miongoni mwa wananchi.
مَّآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنْ أَهْلِ ٱلْقُرَىٰ فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ كَىْ لَا يَكُونَ دُولَةًۢ بَيْنَ ٱلْأَغْنِيَآءِ مِنكُمْ ۚ وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمْ عَنْهُ فَٱنتَهُوا۟ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ
Anacho kitoa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa mijini, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na jamaa wa karibu na mayatima na masikini na wasafiri, yasiwe ni biashara baina ya matajiri miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume basi chukueni. Na anachokataza basi jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika! Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
Imeandikwa kwa niaba ya Ofisi kuu ya Habari Hizb ut-Tahrir na
Ali Omar Albeity
Mwanachama wa Ofisi ya Habari Hizb ut-Tahrir In Kenya