Sera za Kifedha za Kibepari hazina Maadili na Ubinadamu

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

(Imetafsiriwa)

Maandamano ya Kupinga Mswada wa Fedha nchini Kenya yameenea kutoka mji mkuu Nairobi hadi sehemu mbalimbali za nchi, huku walipa kodi wakiendelea kupinga mpango wa Rais William Ruto wa kufadhili Bajeti yake ya Ksh3.9 trilioni (dolari bilioni 31). Mnamo siku ya Alhamisi asubuhi, maandamano ya barabarani yaliregea katika barabara za Nairobi baada ya mapumziko ya saa 24, huku polisi waliokuwa wamejihami wakifyatua vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji.

Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kuangazia yafuatayo:

Bajeti na sheria za kifedha katika tawala za Kidemokrasia ni mazao ya mfumo mbovu wa Ubepari ambao unaasisi mfumo wa fedha uliojengwa juu ya riba na kusababisha mapovu na mizigo mikubwa ya mikopo pamoja na kupanda kwa kiwango cha deni. Ili nchi yoyote ya ulimwengu wa tatu kama Kenya ibaki kuwa taifa linalostahili kupata mikopo, IMF na Benki ya Dunia (taasisi za kikoloni za Magharibi) huitisha hatua kali za kubana matumizi na sera za juu za kifedha. Zaidi ya hayo, tawala za kibepari zinategemea sana ukopaji fedha huku ubwana wa serikali ukiwa kama dhamana ya kufadhili miradi ya serikali. Hata hivyo miradi hii inakabiliwa na ufisadi na ulafi wa viongozi wa serikali hivyo kiasi kikubwa cha fedha huporwa.

Makadirio ya sasa ya bajeti yanayofikia dolari bilioni 31 pamoja na mswada wa fedha unaonyesha maumbile yasiyo ya kimaadili ya siasa ya uchumi ya ubepari ambao huvua sera hiyo kutoka kwa data za takwimu bila ubinadamu. Ni muhimu kutaja kwamba sera zote za kifedha katika uchumi huria wa Kibepari hazina maadili na ubinadamu. Pato la Taifa kwa kila Mwananchi nchini Kenya linatarajiwa kufikia Dolari za Marekani 1865.00 kufikia mwisho wa 2024, kulingana na miundo ya kimataifa ya Uchumi wa Biashara na matarajio ya wachambuzi. Katika kipindi cha muda mrefu, Pato la Taifa la Kenya kwa kila mwananchi linatarajiwa kuimarika karibu dolari za Kimarekani 1973.00 mwaka wa 2025 na Dolari za Marekani 2098.00 mwaka wa 2026. Kulingana na data hii, hali ya kiuchumi na kifedha ya raia wa kawaida imechorwa kuwa ‘imara’. Ukweli wa maandamamo yaliyoenea, unathibitisha zaidi uongo wa nadharia ya mtiririko wa uchumi. (Mkono usioonekana) utajiri ukikusanywa mikononi mwa 1%.

Suluhisho msingi la masaibu ya kiuchumi nchini Kenya na duniani kwa jumla halitapatikana kupitia maandamano, badala yake, kupambana kwa ajili ya mfumo unaowachunga watu ipasavyo na kuwatendea wema. Mfumo unaomridhisha Mola wa wanadamu na kuamiliana nao kwa uadilifu kupitia kwa Ahkam (hukmu) za Uislamu. Mfumo ambao utaifanya dola yake Khilafah kuwa huru kiuchumi na kisiasa bila kuegemea zana za kiuchumi za kikoloni za ubeberu wa Magharibi.

Dola ya Khilafah, ambayo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt) kusimamishwa kwake tena kunakaribia zaidi siku baada ya siku, haitapoteza muda katika mahusiano ya umma kuandaa sheria za fedha kila mwaka. Mapato na matumizi yameteremshwa na kusuluhishwa na Mwenyezi Mungu kiwahyi, yaani, sekta zake katika bajeti ya Dola ya Khilafah huamuliwa na hukmu za kudumu za Sharia. Khilafah ina mapato aina mbalimbali kama vile Al-Ghana’im (ngawira za vita), Kharaj (kodi ya ardhi), Fai (ngawira zisizo za vita), na ushuru wa Jizya kutoka kwa wanaume wenye uwezo wasio Waislamu. Katika suala hili, Khilafah haitatoza kodi za adhabu kwa watu. Baada ya kusimamishwa tena, Khilafah itawakomboa watu duniani kutokana na udhalimu wa kupindukia na umaskini uliokithiri kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya