Sera za Ovu za Marekani Hazitaokoa Kenya na Afrika kwa Jumla kutokana na Msukosuko wa Ubepari

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

(Imetafsiriwa)

Ziara ya siku nne ya rais William Ruto nchini Marekani imekamilika. Hii ilikuwa ni ziara ya kwanza ya Kiserikali kwa kiongozi huyo wa Afrika katika kipindi cha miaka 16. Kuhusu ziara hiyo, sisi, katika Hizb ut Tahrir/Kenya, tunaeleza yafuatayo:

Ziara hiyo haitaokoa Kenya kwa vile Marekani imekuwa katika upande mbaya wa historia dhidi ya maslahi ya uchumi wa Kenya na ule wa Afrika kwa jumla. Majadiliano kati ya Rais Ruto na mwenzake wa Marekani Rais Joe Biden kuhusu Demokrasia, biashara na usalama si kingine ila shinikizo linaloongezeka kwa Kenya katika kutekeleza sera ovu za kibeberu ambazo zitaendelea kudhuru nchi hii. Hivyo, kupata fursa za kifedha kutoka kwa Marekani kwa uchumi wa Kenya ambao tayari unaugua chini ya mzigo mkubwa wa deni na shida ya gharama ya maisha kunaongeza masaibu zaidi. Sera za biashara za kibepari zinazopigiwa debe na Marekani kama vile soko huria zimesababisha maafa ya kiuchumi ambayo yameiacha Kenya na Afrika kwa jumla zikiwa zimeharibiwa na viwango vya kuzorota vya umaskini, njaa na magonjwa.

Marekani haina njia ya kuzungumzia usalama kwani ndiyo mdhamini mkuu wa ukosefu wa usalama na ugaidi duniani. Kama watangulizi wake, Joe Biden amekuwa akiunga mkono umbile la Kiyahudi linaloua watu huko Gaza. Hasa, tangu kuundwa kwa umbile la Kiyahudi mwaka wa 1948, Marekani imekuwa daima mshirika imara na “Israel” ikitoa silaha, vifaru na ndege ili kuendelea kushambulia Palestina ikiwa ni pamoja na Gaza. Tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana, Biden amelipa umbile hilo haramu takriban dolari milioni 250 na uhamisho mia moja wa msaada wa kijeshi. Zaidi ya hayo, kwa kisingizio cha ‘vita dhidi ya ugaidi’, Marekani imechukua fursa ya wanajeshi wa mataifa mengi barani Afrika kuwaweka chini ya mshiko wake; na kuanzisha kambi za kijeshi katika mikakati yake ya kuchukua nafasi ya Uingereza na Ufaransa ili iweze kuwa na sehemu kubwa ya uporaji wa Afrika. Nchini Kenya, Wamarekani wanaendesha kambi ya kijeshi huko Kambi ya Simba, Lamu, na Kambi nyengine ya Operesheni ya Mbele katika Kaunti ya Wajir.

Tunadumisha kwamba ziara hii ni kwa ajili ya kuimarisha zaidi utawala wa Marekani katika nchi ambayo historia yake ya hivi majuzi imeshuhudia mapambano ya Uingereza na Marekani yakidhihirishwa kupitia serikali tawala na upinzani wa kisiasa. Katika kilele cha uhasimu wa kikoloni (kati ya Marekani na Uingereza), Kenya inajikuta mikononi mwa ajenda za kikoloni kama vile ‘vita dhidi ya ugaidi’ ikipeleka majeshi yake nchini Somalia, DRC na hivi majuzi Haiti.

Kenya kama nchi nyingine yoyote barani Afrika bado iko chini ya nira ya ukoloni mamboleo, kwa hiyo haiwezi kustahamili shinikizo la kisiasa la Marekani. Ni katika muktadha huu ambapo Kenya mara nyingi imeitambua ‘Israel’, inaunga mkono suluhisho la mwisho la Dola Mbili kwa Palestina na dola ya Kiyahudi. Hatimaye kwa kutegemea dola za magharibi, Kenya na Afrika kwa jumla inajiweka katika machafuko. Ni kwa kuondolewa tu ushawishi wa kikoloni na kugejea kwa Dola ya Khilafah ndipo utulivu wa kiuchumi, kisiasa na kijamii utaregea kusini ya dunia.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya