Shahidi Mwengine Mikononi Mwa Dhalimu wa Uzbekistan

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا﴿

“Miongoni mwa waumini kuna wanaume waliosadikisha waliyomuahidi Allah juu yake. Miongoni mwao wamekwisha timiza ahadi yao kwa kifo na miongoni mwao wangali wanangojea, na wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [33:23].

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inaomboleza kwa Ummah wa Kiislamu kifo cha ndugu Saidmahmudov Saidaziz, aliyezaliwa mnamo 1971, baba wa watoto watatu na mwenyeji wa Tashkent, wilaya ya Almaza, barabara ya Kuksu 54.

Licha ya ukweli kuwa Hizb ut Tahrir inafanya kazi ya kimfumo na ya kisiasa, serikali zinapambana na Hizb kinguvu. Serikali ya Uzbekistan haina tofaouti. Punde tu I. Karimov alipofahamu kuwa Hizb ut Tahrir inafuata njia ya Mtume Muhammad (saw), na haifanyi miamala yoyote na madhalimu, Mashababu wa Hizb walianza kupata mateso. Lakini licha ya madhila yote haya, mashababu hawa hawakurudi nyuma kutokana na njia hii.

Ndugu yetu Saidaziz (Allah amrehemu) alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kubeba da’wah katika safu za Hizb ut Tahrir. Mwanzoni mwa mwaka wa 2000, Mashababu wengi walikamatwa, miongoni mwao alikuwa ndugu Saidaziz. Alitumikia kifungo chake katika korokoro ya Kiziltepe, kisha kupelekwa katika korokoro kali ya Karaulbazar. Hawakumuachilia huru Saidaziz kwa sababu tu alikataa kuachana na ubebaji da’wah ya Hizb ut Tahrir licha ya mateso yote aliyopitia.

Katika msimu wa masika wa 2018, baada ya kuugua kwa muda mrefu, Saidaziz aliwekwa katika gereza la Tashkent la Sangorod. Alikuwa na maradhi ya kifua kikuu. Ilipoona maradhi ya Saidaziz yanazidi na hayawezi kutibika na ili kuondosha takwimu mbaya, serikali ya dhalimu ilimuachilia huru ndugu yetu mnamo Mei. Mnamo Juni 23, 2018 Saidaziz aliaga dunia kwenda katika rehma za Allah (swt).

Sisi katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia ya ndugu yetu, tunamuomba Allah (swt) kuipa subra na faraja familia yake. Tunamuomba Allah Nusra na afueni, tunayaomba majeshi ya Waislamu kusimama kidete na kuulinda Uislamu na Waislamu na kuhuisha tena Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Tunamuomba Allah nguvu na uwezo ili kuwakomboa wafungwa wote wa Kiislamu – ndugu zetu na dada zetu kutoka katika magereza ya madhalimu. Allah (swt) ni muweza juu ya kila kitu.

Allah (swt) asema katika Kitabu chake Kitukufu:

 

إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿

“Hakika sisi ni wa Allah, na hakika kwake yeye tutaregea.” [2:156]

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

H.  22 Shawwal 1439 Na: 1439 AH / 029
M.  Ijumaa, 06 Julai 2018